webondo
JF-Expert Member
- Apr 29, 2012
- 1,713
- 382
Hiyo ni hypothesis yako au ni fact?
Kitu unachokizungumzia hapa ni kigumu sana kuliko unavyodhania. Siyo rahisi manufacturers (there are lots, lots of them) wawasilishe IMEI numbers kwa TCRA kwa sababu hawana sababu ya kufanya hivyo na hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo. Chukulia kwa mfano Apple, hawauzi kabisa (Yes, hawauzi) simu Tanzania, uwaambie Apple Inc. wawasilishe IMEI za simu zao zote TCRA itakuwa kichekesho! Lakini eventually iPhone zinaingia Tanzania, na hauwezi kuzizuiya zisiingie!! Wenye uwezo wa kublock IMEI ya simu isipate mawasiliano ni carrier, lakini kwa simu hizi za mchina carrier ni ngumu kujua simu fake na halali kupitia IMEI peke yake. Simu nyingi "fake" au clone zinamajina ya kwa juu tu, lakini IMEI zake ziko associated na identity zake halali, yaani jina la board!
Sijuwi ni uvivu wa kufikiria tu au kukwepa majukumu, lakini anayetakiwa hasa kudhibiti simu clone, na simu zilizo chini ya viwango siyo TCRA, ni TBS. TBS ndiyo wenye dhamana ya kuhakiki viwango vya bidhaa zote zinazotengenezwa na zinazoingizwa ndani ja JMT. Ukikutana na vitasa, redio, televisheni, fenicha, simu, au kitu chochote kimeingizwa nchini na kinauzwa sokoni wa kulaumiwa na TBS. Huwezi kuanza kupiga hodi nyumba kwa nyumba kutafuta viti "fake" na kuvikamata kwenda kuvichoma moto, mlaji wa mwisho amekikuta tu sokoni, akaona bei nafuu akanunua, ukimuuzia lawama wakati wewe umeshindwa kutimiza wajibu ni ufinyu wa fikra usiomithilika!
Habari ndugu zangu,
Ninachoelewa ni kuwa kutakuwa na utaratibu wa ku-track simu zote za mikononi zilizo katika matumizi kujua kama imesajiliwa na kupewa International Identification (IMEI) na la. Utaratibu huo ambao utatumia kwa sasa haujawekwa wazi kwetu sisi walaji. Lakini mimi binafsi naamini inawezekana kufanya hivyo. Tukumbuke kuwa simu zote ambazo ziko katika matumizi service providers (Kama Tigo, Vodacom Airtel na wengine) wanafahamu huyu mlaji/mteja wetu anatumia simu yenye huo usajili (IMEI) au la, lakini kama mteja/mlaji huyo anatumia simu yenye utambuzi huo basi wanajua ni IMEI gani.
Kwahiyo sasa, pia TCRA nao wana uwezo huohuo na zaidi ya hapo. Lakini haimaanishi kuwa watengenezaji wa simu (manufacturers) wataleta orodha ya simu zao na IMEI zao na kuwakabidgi TCRA.. NO doesn't work like that. Hawa service providers wote wanaitambua kila handset kwa IMEI yake kwa zile zote zenye IMEI. Na wanajua kuwa mteja huyu anatumia simu ambayo hana international identification (IMEI) au la. Ndio maana leo hii kama una kumbukumbu ya IMEI ya simu yako then ikaibiwa popote au kupotea.. kisha ikienda tu hewani (yaani mtu mwingine akawa anaitumia) basi inaweza kuwa tracked. Inakuwa tracked kwa kutumia IMEI hiyo. Kwahiyo mfumo wa kum-track mtu huyo ni kwamba IMEI hiyo inakuwa linked na namba ya simu hiyo kisha tower zina-locate mtu alipo.
Kwa faida ya wasomaji wengi, mnaweza kuchungulia IMEI ya simu yako kwa kufungua mtandao huu Check IMEI - IMEI.info ingawa nitahadhalishe kuwa huu mtandao hauhusiani na mfumo wa TCRA kuhakiki IMEI ya simu yako.
Lugha ya kienyeji wanasema "watazima simu zote" haimaanishi simu ambazo IMEI zake haziko registered zitazimika, No.. ila zitakuwa disabled, wakifanya hivyo hazitaweza kuunganisha na service provider hata kama ina SIM card.
Asante kwako.