TCRA wakoroga pia wametuchanganya kabisa.

TCRA wakoroga pia wametuchanganya kabisa.

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Posts
1,002
Reaction score
278
Kama kuna mwanajf aliyekuwa anafuatilia kipindi cha malumbano ya hoja jana kilichokuwa kinarushwa na Itv atakubaliana na mimi.Jana hiyo timu ya viongozi toka Mamlaka ya mawasiliano Tcra walianza vizuri kwa kutueleza kuwa Makampuni yaliyopewa leseni ya kusambaza mfumo huu wa digitali ni matatu yaani,STARTIMES,TING,na BASIC TRANSIMISION(zuku) na moja ya vitu walivyokubaliana ni kuwa wawe wanarusha zile chaneli tano za Tanzania bure bila kulipia kwamba muda wa malipo wa hewani ukiisha hizo chaneli zinaendelea kuonekana.Sasa mwisho wakati wanahitimisha kuna mhusika mmoja wa Tcra anaitwa Mungi akaanza kusema tena kuwa kampuni ya zuku haitakuwa inaonyesha chaneli zile tano bure,kwa sababu mkataba wao hausemi hivyo.Pia akasema anawashauri wananchi wanapokwenda kununua ving'amuzi wanunue vile vilivyoandikwa DVB-T2 yaani Digital Video Broadcasting via Terestial,na wasinunue vile vilivyoandikwa DVB-S Yaani Digital Video Broadcasting via Satellite.Sasa swali langu nawauliza kama walijua hivyo kwa nini walitoa leseni kwa makampuni hayo au ndio kuipigia debe kampuni yao ya startimes wakati haifanyi vizuri inabagua maeneo? Zuku popote pale ulipo nchini inafanya kazi.Naomba Tcra watoe ufafanuzi ulio wa wazi kwanini waseme wametoa vibali kwa makampuni matatu halafu tena waseme mengine hayawezi kuonyesha zile chaneli tano.Hapa sijazungumzia kabisa DSTV kwa sababu hata ktk kipindi cha tuambie viongozi haohao walikwishasema huu mfumo wa digitali hauwahusu hao dstv.
Nawasilisha.
 
Mkuu hao trca wanakula mishahara ya bure 2! We unazungumzia la local channels ulizia tatizo la tigo kukata network siku nzuri na sio mara 1. Hakuna onyo wala karipio. *** tcra

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sasa wao sio ndio regulator si ndio wanatakiwa waeleze ni ving'amuzi gani vinatakiwa viwepo nchini ,je kweli sisi watu wa kawaida hayo mambo tutayajuaje kuwa king'amuzi aina hii kinafaa au hakifai.Pia kuhusu Zuku kwa nini waende kinyume na sheria,na walipoomba kibali ina maana watalamu wa TCRA hawakuona hayo mapungufu?ndio maana huwa wakati wote nakosa imani na hawa watu waliowekwa kutusaidia sisi wananchi ,ukiangalia kwa undani koote huko ni kuzunguka tu,uozo huo wote asili yake ni neno moja tu RUSHWA baaasi,rushwa ni kansa katika taifa hili kila sehemu ni rushwa ,rushwa tu
 
Jamani mleta mada anachanganya,basic transimision sio ya ZUKU hii ni kampuni ya ITV ikishirikiana na STAR TV.
 
Sijaona Mkorogo wowote

Sasa wewe King'amuzi cha Satelite ubataka Upokee Mawimbi yanayorushwa na Minara ya Ardhini? Ni sasa na Mtu anayetaka kupokea Television kwenye Redio ya Mkulima
 
Mimi ninavyoelewa ni kuwa ifikapo tarehe 31/12/12 saa 6 na dak 1 usiku mitambo yote ya analogue itazimwa afrika ya mashariki nzima hivyo kufanya kuwa bila king'amuzi huwezi kuona tv. Ilikuweza kuweza kuangalia tv inabidi uwe aidha na dish au kutumia antena kupitiaDVB. Makampuni yaliyopo ndiyo hayo yaliyopewa leseni lakini haizuii makampuni mengine yatakayokuja.
Ingawa mimi siyo mtaalam lakini DSTV na Zuku TV hizi ni DVS ambapo utahitaji dish pamoja na king'amuzi.
ili watanzania wengi wafaidi kuangalia tv zao hadi vijijini inapaswa ving'amuzi viuzwe bei rahisi sana na wawele package kwa wale ambao wanataka kuona package za nyumbani tu [iwe sharti kwa yeyote anayeomba leseni] asilipe chochote kile ila kwa wale ambao wanataka zaidi ndiyo watakaolipa zaidi.
 
mimi najiuliza ni kwanini tz ili adopt system ya dvb t badala ya dvb s,ni zaidi ya miaka mitatu sasa tangu startimes iingie dar lakini mpaka leo hata kwenye miji mingi ambayo ni makao makuu ya mikoa haijapata huduma hii ya dvb t sijui hata wilayani huduma itafika lini,achilia mbali kwenye tarafa na vijijini.kama tz inge adopt dvb s, leo hii huduma hii ingesambaa nchi nzima mfano halisi angalia zuku. jana niliona hicho kipindi na nilishangazwa na kauli ya msemaji wa tcra kwamba ifikapo dec 31 mitambo yote ya analogy itafugwa nchi nzima,hii ni sawa na kusema kwasababu dar arusha mwanza dodoma moshi na tanga mijini tu ndiyo wana signal basi miji mingine,wilayani, miji midogo na vijijini sio issue tuzime tu, mwisho kabisa labda ningemuliza swali rahisi yule msemaji wa mamlaka ni lini wanategemea huduma hizi za dvb t zita cover nchi nzima ya tanzania hii ni pamoja na vijijini.
 
Hakika sijui kama Tcra wanalijua hili.
 
Back
Top Bottom