TCRA wafuatilieni Vodacom

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Messages
1,328
Points
2,000

Koryo2

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2016
1,328 2,000
Mimi ni mteja wa Vodacom nikiwa na line yao na pia line yao ya internet. Nimekuwa nikinunua kifurushi chao kila mwezi kwa gharama ya Tshs. 35,000 na kifurushi hiki kwa siku za nyuma nilikuwa ninakitumia kwa mwezi mzima.

Nimeendelea kununua kifurushi cha GB10 kwa Tshs. 35,000 ili nikitumie kwa mwezi mzima lakini kwa siku za karibuni tarehe 27.11.2019 nilinunua kifurushi tena cha GB10 kwa Tshs. 35,000 ili nikitumie kwa mwezi mzima lakini cha ajabu tarehe 30.11.2019 nilipata taarifa kupitia simu yangu kuwa sina salio kwenye kifurushi changu yaani baada ya siku tatu sina salio?.

Serikali imewekwa na wananchi pale penye matatizo ni budi serikali isaidie wananchi wake. Kitendo kama hiki kinatakiwa kifuatiliwe na huu ni wizi wa mchana. Ninaiomba TCRA iingilie kati suala hili.
 
shamajengo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Messages
1,067
Points
2,000

shamajengo

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2015
1,067 2,000
Bro sidhani kama serikali watalifamyia kazi japo mimi pia ni mtumiaji wa vodacom na hayo maumivu pia nayaona. Ila nahisi ccm itakuwa na mkono wake juu ya huu uhuni kwani kama wanahisa kdhaa walizotoa kwa rostam unadhani pesa ha kununua wapinzani wanatoa wapi?
 
mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
10,205
Points
2,000

mwasu

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
10,205 2,000
Unaponunua kifurushi si unapata ujumbe kuwa VAT umelipa? Serikali hapo ndipo inapo sherehekea sasa ikiingilia kati unafikiri huo ukwasi wataupataje?, Tunaumizwa sana na mambo mengi kwa sababu tunataka kunua ndege nyingi na kufanya maajabu kwa kipindi kifupi..
 
binti kiziwi

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Messages
3,302
Points
2,000

binti kiziwi

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2014
3,302 2,000
Kilikuwa kifurushi changu pendwa hiki kwa Muda mrefu sana, nilikuwa nakaa nacho mwezi mzima, hivi karibuni kikawa hakifiki hata wiki. Nimeamua tu siku hizi naunga cha siku basi!
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Messages
4,676
Points
2,000

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2014
4,676 2,000
Lodge malalamiko kwa mtoa huduma wakizingua ingia kwenye website ya TCRA jaza fomu ya malalamiko au washtaki kwenye kamati ya malalamiko udai na fidia ikiwezekana wenzio wengine waliwahi fanya hivyo
 
Zabron Hamis

Verified Member
Joined
Dec 19, 2016
Messages
1,442
Points
2,000

Zabron Hamis

Verified Member
Joined Dec 19, 2016
1,442 2,000
Haya Mimi walinikata kivurushi changu cha wiki kuuliza salio Hamna kitu.
vodacom ni wapuuzi sijapata kuona. Tarehe 14 nov mwaka huu nilinunua kifurushi cha internet 2gb. Kwakuwa ilikuwa usiku na nilihisi kuchoka, nilizima data ili nipunguze usingizi kabla ya kuendelea na kazi (tofauti ya muda wa kununua na kuzima data ni chini ya dakika 2) na wakati huo nilikuwa na mb200 za yakwako tu ambaO sikuwa nimetumia. Ilipofika mida ya saa tisa usiku, nikaamka na kuwasha data 😲😲😲 nikakutana na kale kaalama kanakoonesha natumia free internet. Nilishtuka sana, na haraka sana nikawasiliana na huduma kwamteja. Muhudumu wa kwanza akaniambia haoni tatizo na hicho kifurushi kimeshatumika. Nikaona isiwe nongwa, nikarudia kupiga. Wa pili baada ya kumbana anieleze kifurushi kimetumikaje akaniambia kuna tatizo kwenye system hivyo nisubiri wakati wanashughulikia. Ikapita siku nzima na masaa kadhaa nikapiga tena. Mara hii nikaambiwa nitaunganishwa na kitengo husika kwakuwa ni kweli kuna shida, wakakata simu. Sikupigiwa. Nikarudia kupiga baada ya masaa 12, jibu likawa lilelile kuwa naunganishwa na kitengo husika ndani ya muda mfupi, wakakata simu. Sikupigiwa. Nikaamua kuawaacha kama walivyo.

Jana ndio ilikuwa kituko. Nimenunua kifurushi na ndani ya sekunde chini ya kumi bila hata ujumbe kale kaalama kakaja tena. Nikapiga simu nikaambiwa nimetumia kifurushi na kimeisha. Majibu yaliyoendelea ni aibu. Mara nenda vodashop nikawaambia nani analipa gharama za usafri (nauli ni 15000) wakasema kama nina shida niende au nikae, wakakata simu.

vodacom popote mlipo inueni mikono juu nq muimbe juu wimbo "sisi ni matapeli wa kiwango cha reli ya magufuli"

Nilikuwa nawatetea sana ila kuanzia jana mtu akisema anataka kusajili laini yenu, nampa ujumbe huo hapo juu.
 
evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Messages
2,254
Points
2,000

evonik

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2015
2,254 2,000
Voda net yao IPO vzr tatizo ndo hilo, wanaringa wana wateja wengi
vodacom ni wapuuzi sijapata kuona. Tarehe 14 nov mwaka huu nilinunua kifurushi cha internet 2gb. Kwakuwa ilikuwa usiku na nilihisi kuchoka, nilizima data ili nipunguze usingizi kabla ya kuendelea na kazi (tofauti ya muda wa kununua na kuzima data ni chini ya dakika 2) na wakati huo nilikuwa na mb200 za yakwako tu ambaO sikuwa nimetumia. Ilipofika mida ya saa tisa usiku, nikaamka na kuwasha data nikakutana na kale kaalama kanakoonesha natumia free internet. Nilishtuka sana, na haraka sana nikawasiliana na huduma kwamteja. Muhudumu wa kwanza akaniambia haoni tatizo na hicho kifurushi kimeshatumika. Nikaona isiwe nongwa, nikarudia kupiga. Wa pili baada ya kumbana anieleze kifurushi kimetumikaje akaniambia kuna tatizo kwenye system hivyo nisubiri wakati wanashughulikia. Ikapita siku nzima na masaa kadhaa nikapiga tena. Mara hii nikaambiwa nitaunganishwa na kitengo husika kwakuwa ni kweli kuna shida, wakakata simu. Sikupigiwa. Nikarudia kupiga baada ya masaa 12, jibu likawa lilelile kuwa naunganishwa na kitengo husika ndani ya muda mfupi, wakakata simu. Sikupigiwa. Nikaamua kuawaacha kama walivyo.

Jana ndio ilikuwa kituko. Nimenunua kifurushi na ndani ya sekunde chini ya kumi bila hata ujumbe kale kaalama kakaja tena. Nikapiga simu nikaambiwa nimetumia kifurushi na kimeisha. Majibu yaliyoendelea ni aibu. Mara nenda vodashop nikawaambia nani analipa gharama za usafri (nauli ni 15000) wakasema kama nina shida niende au nikae, wakakata simu.

vodacom popote mlipo inueni mikono juu nq muimbe juu wimbo "sisi ni matapeli wa kiwango cha reli ya magufuli"

Nilikuwa nawatetea sana ila kuanzia jana mtu akisema anataka kusajili laini yenu, nampa ujumbe huo hapo juu.
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
27,658
Points
2,000

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
27,658 2,000
Wasijisahau! wawaulize wenzao wa TTCL walivyokuwa wanaringa miaka ya nyuma but leo wanakata mauno barabarani eti wanatangaza huduma zao!
 
savage94

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2018
Messages
466
Points
1,000

savage94

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2018
466 1,000
Kiongozi kama una uwezo wa kuweka 35000/= kununua tu data na mauzauza ndio kama hayo si bora uhame tu! Jaribu hata airtel utapata unafuu, ukiwa na lain yao ya chuo unajiunga UNI kwa sh. 1000/= unapata 1GB ya kutumia siku tatu na sms na dk kibao! Binafsi mara nyingi najiunga kila baada ya siku mbili nimekusanya madakika yamefika laki sasa sijui nitayamaliza vipi! Tena na ukipata ikawa ya 4G ndo unastarehe kabisa! Huku ile umejiunga saa mbili then saa mbili na nusu unapokea ujumbe kwamba data zako zimeisha wakati ulizima data hakuna!

Japo nao mda mwingine wanazingua kama juzi hvyo vifurushi havikuwa hewani, lakn kero zao sio kama voda. Kwa hiyo 35000 yako huku utajiunga vya buku mwezi mzma na chenji itabaki utavirundika mpk utachoka!
 
At Calvary

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Messages
1,323
Points
2,000

At Calvary

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2018
1,323 2,000
V
Mimi ni mteja wa Vodacom nikiwa na line yao na pia line yao ya internet. Nimekuwa nikinunua kifurushi chao kila mwezi kwa gharama ya Tshs. 35,000 na kifurushi hiki kwa siku za nyuma nilikuwa ninakitumia kwa mwezi mzima.

Nimeendelea kununua kifurushi cha GB10 kwa Tshs. 35,000 ili nikitumie kwa mwezi mzima lakini kwa siku za karibuni tarehe 27.11.2019 nilinunua kifurushi tena cha GB10 kwa Tshs. 35,000 ili nikitumie kwa mwezi mzima lakini cha ajabu tarehe 30.11.2019 nilipata taarifa kupitia simu yangu kuwa sina salio kwenye kifurushi changu yaani baada ya siku tatu sina salio?.

Serikali imewekwa na wananchi pale penye matatizo ni budi serikali isaidie wananchi wake. Kitendo kama hiki kinatakiwa kifuatiliwe na huu ni wizi wa mchana. Ninaiomba TCRA iingilie kati suala hili.
Vodacom Tanzania sina hamu nao. Juzi tu wanifanyia kama hivyo.

Chukua halotel mkuu kwa 10k unapata GB 10 au 15 kwa mwezi ukinunua kwa halopesa megabando.
 
Baba Watoto

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Messages
372
Points
250

Baba Watoto

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2010
372 250
Sikuwahi kukumbwa na hii adha na nilifikiria watu wanawaonea tuuu au wanasahau kuzima data hadi jana. Kwa kweli namtafuta Mshana Jr awaoteshe busha woteee kabla sijarudi kijijini kwangu. buji buji naomba na contacts za mtu anipeleke ziwa Tanganyika.
 
Forum statistics

Threads 1,382,257
Members 526,314
Posts 33,823,311
Top