TCRA toeni ufafanuzi kuhusu Beep Mbili wakati wa kupiga simu

Amalinze

JF-Expert Member
May 6, 2012
6,780
5,300
Habari wadau,

Kumekuwa na sintofahamu tangia Jana wakati mtu akitaka kupiga simu kwenda mtandao tofauti na anaotumia anasikia beep mbili.

Wengi wanahisi wanarekodiwa hivyo kuhofia kupiga simu na wengine wanahisi kwamba simu haijaenda hivyo akisikia beeps anakata.

Ukweli ni kwamba TCRA wameshaanzisha MNP kwa hapa Tanzania na imeanza kufanya kazi jana, hizo beep mbili ina kualert kwamba unapiga simu kwenda mtandao mwingine,ukipiga kwenye mtandao mmoja hausikii hizo beep.

Kwa Maelezo kuhusu MNP bonyeza link ya chini.

TRCA watatua mwiba wa mitandao mibovu ya simu hapo June 2015
 
Hizo beep 2 kabla ya vmu kuanza kuita nasikia wanarekod mazungumzo. So tuwe makini na mazungumzo yetu hasa ka unaisema sirikally
 
kweli nilipiga jana kutoka zantel kwenda voda nikahisi beep 2 nikakata nikajua simu imezimwa, nikapiga tena ikabeep mara 2 hapo hapo mara ikaita nikajiuliza kulikoni, kweli trca waje na majibu hapa, tusiwe watumwa ndani ya nchi yetu
 
tuwasubiri tcra watasema nini, wakikaa kimya, tutajua na sie tufanye nini, kuna maswala muhimu ya kufatilia kama makodi ya simu, unaweka vocha hujatumia data, hujapiga ukiuliza balance hapo hapo unaambiwa 200 kwenyu!! ishapuruliwa, watu tumelalamika lakini wao aah, wako biz na kukamata wanaotoa maneno ya kumkwaza mtukufu
 
We mtoa mada kuna unachokijua, Hebu dadavua kwa umakini.... Je hizo beeps hazina uhusiano na kurekodiwa???
tusubiri tcra waje kusema nini, manake ni kweli beep 2 au 1 kwa simu unapopiga huwa inaenda kwa recording machine, sasa nia yao hasa ndo nini, basi sie watu milion 45 tutaenda jela,
 
Hizo beeps mbili nafikiri zinawahusu watu wa mitandaoni mbona kuna mpangaji mwenzangu mpika vitumbua simu yake haina beep hata moja.
 
Kama unatongoza wewe funguka, kama unakasembe kako unataka kutoa maelekezo kakamwagwe baharini wewe funguka ili wanaosikiliza wafaidi vipaji vyako
 
Back
Top Bottom