TCRA na mfumo wao mpya wa kutumia laini 1 kuhamia mtandao mwingind.

Singidan

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
880
937
Habari wadau!
Huu mfumo wa TRCA ambao wanadai mtu ataweza kuhama kutoka mtandao 1 kwenda mwingine nauona ni mfumo ambao hautufai kabisa na una mapungufu. Nimemsikia mtu 1 kutoka TCRA redion akisema mtu ili ahame inabidi aende kwa wakala kwanza. Pia ukihama mtandao A kwenda B, Utakaa siku 30 ndiyo uweze kurudi A au kwenda C au D. Pia ukihama A Kwenda B basi utakuwa hupatikan A. Pia amedai kutakuwa na gharama ambazo watatoza pale unaposhifti. Yaani kiukweli mimi naona wamenichanganya sana, oa kama ndiyo hivyo ni bora watuache kabisa kama tulivyozoea.
 
Upuuzi tu na kujiongezea gharama za usumbufu.

Kwa mfano umeisajili line ya mtandao x na NMB mobile au Sim Banking, ukihama na baadae kutaka kurudi si ni kujitafutia usumbufu mwenyewe?!

Nowdays, sina muda wa kwenda kupanga foleni ATM, nafanya kila kitu kwa simu yangu.
 
Kuna mambo mengi ambayo TCRA wangeyafanya kuboresha huduma Tanzania tena ambayo sio very costful ila wamekaa wanahangaika na vitu kama hivi ambavyo effect yake ni negligible. Hivi wanaofanya kazi TCRA ni akina nani? I'm very curious maana I seriously doubt their ability.
 
Wandugu,

Hiki wanachotaka kuanzisha TCRA ni teknolojia ambayo kwa wenzetu iko siku nyingi na haina mlolongo. Kama una line ya kampuni A na unataka kuhamia Kambuni B, unachotakiwa kufanya ni kupiga simuvKampuni A unapopata huduma na kuwaambia wakupe Porting Authorization Code (PAC). Kambuni A wanatakiwa wakupe PAC number yako bila kukuhoji ama kwa simua au wakutumie text message. kwa mfano, nchini Uingereza provider anatakiwa kukupa PAC number yako muda huohuo au ndani ya masaa mawili.

Baada ya kupata PAC number yako unawapigia kampuni B unayotaka kuhamia na kuwapa number yako ya simu na PAC number kisha unakua activated kwenye mtandao wao. Hakutakiwi kuwe na gharama yoyote kwa kuhama maana mtu hulazimishi kuwa mteja wa kampuni usiyoitaka. Kama sisi tutachajiwa inaleta maswali kidogo maana mantiki ya kuchaji mtu kuhamisha number yake kwende mtandao mwingine haiko wazi na bado wewe kama mteja wa simu utaendelea kutumia fedha kwa huduma za simu utakazopata.

Hii huduma ni ya msingi sana maana mara nyingi watu wamelazimika kuvumilia huduma mbovu za kampuni waliyoko kama vile wanavumilia ndoa kwa sababu tu wasingependa kupoteza number zao. Wakati mwingine soko la ushindani linakupa fursa ya kupata huduma bora na ya nafuu zaidi kwa kuhamia kwenye kampuni nyingine lakini kizuizi kinakua number yako. kuna wakati pia unaweza kuhamia eneo ambalo kampuni uliyoko hawana coverage nzuri. Kwa mfano ukihamishiwa kazi wilaya ya Kwimba kikazi na line yako ya Tigo unayopipenda kama yangu ujue matumizi ya data utasahau..wakati ungeweza kuhama nayo kwenda Voda au Halotel na kufaidika.

Hata hivyo kwa nchi kama yetu, ni vema TCRA wakaweka masharti fulani ya kuwafanya watu wasifanye mchezo wa kuhama kila siku bila sababu zua msingi. Na kuweka gharama inaweza kuwa mbinu mojawapo lakini ifanyike pale ambapo mtu atakua anataka kuhama mara ya pili na kuendelea.


Tatizo unaangalia kinacho fanyika sijui uingereza (na utafauti kati ya hali ya uchumi kati ya Nchi hizo mbili pia utafauti wa data plans kati ya Nchi hizo mbili) pia consider kuwa haya makampuni pia unayapunguzia mapato na wao kwa mfano haya makampuni yameshaagiza,kulipia na kupokea bulk order za sim-cards na haya mauzo ya sim card yanachangia mapato yao.. Sasa sahivi mtu anakuja out of nowhere anakupunguzia Njia yako moja ya kuiongeza mapato kwa kuwezesha watu kuhama mtandao wako bure kwa kupiga tu simu.



Sasa hiyo yako ya haitakiwi kuwa na gharama wakati hiyo process inawafanya waingie gharama maybe kuset up hiyo number transfer system (kama awakuwa nayo before) kuanzisha system ya kupokea simu kutoka kwa watu wa mitandao mingine kwa customer call Centre zao and etc. Hao kule data plans zao zipo juu to the point kuwa utakuta hizo expenses zote zinaweza kuwa zimemezwa ndani yake hence azi haribu profit margins.
 
Elimu bado inahitajika juu ya hii huduma,hata kampuni za simu hawako wazi kuielezea hii huduma.

Lakini naona ni busara ingewekwa kuwa mtu uhame muda wowote yaani kama ni hizo namba za utambulisho kampuni ziwape wateja wake.

Hii ni huduma nzuri sana kwa watu wanaotafuta maisha kwa kutegemea kusafiri sehemu mbalimbali mfano vijijini ambako siyo rahisi mitandao yote kupatikana
 
Ndugu yangu utakuja,

Sijajua kwa nini wewe umeona mchango wangu ni tatizo. Mimi nimtoa mchango/maoni yangu kwa uzoefu na uelewa wangu na wewe ungeweza kutoa wako kwa hoja. Pia tambua exposure yetu ina-limit uelewa wetu wa mambo na ina-determine our line of thinking hivyo usishawishike kwamba what you know/think ndio the best approach. Hebu tuwe practical kidogo tuachane na assumptions:

Moja, unaweza kunipa kielelezo cha ukubwa wa gharama za data kati ya UK na Tz ili kuthibitisha claim yako? And how comes gharama za data ndio ziwe compensation ya huduma ya kubadilisha providers? Nadhani wewe na mimi tunajua kwamba kwa sasa sisi kama nchi hatutengenezi teknologia yoyote kwenye soko la telecom. Vifaa, teknolojia, na huduma zinazotelewa vyote tume-imported toka mataifa yaliyoendelea na kama UK. Hivyo kusema huduma hiyo iko siku nyingi kwenye telecom industry ni sawa tu ningesema kutumuia 4G wenzetu walishaanza kabla yetu. Sikua na maana nyingine.

Pili, swala la gharama kwa maana uliyoisema wewe halina uhalisia. Sijawahi kuona kampuni ya huduma karne hii ambayo haina customer centre inayoweza kupokea simu za wateja na wasio wateja hivyo kulazimika kuanzisha kitengo kwa lengo la kupokea ismu za wanaotaka kuhamia tu. Na hata kama ingekua hivyo, kuna shida gani wakati unapokea wateja wapya? Kupata wateja si ndio kipato chenyewe kwenye huduma za telecom?

Tatu, hoja ya kwamba makampuni yatapunguza mapato haina mashiko maana indirectly unasema kwamba kuna makampuni yataendelee kutoa huduma mbovu au ghali na hivyo kulazimika kukimbiwa. Hivyo kuweka huduma ya mteja kubadili provider bila kubadili number ni hatari kwao. Ungeweza kutazama upande wa pili kwamba hii huduma itaongeza competitiveness kati ya watoa huduma kila mmoja akiboresha huduma yake na kutoa services kwa affordable cost zaidi na hivyo kuendelea kuhifadhi wateja wake na kuongeza wengine. Kwa nini uwaze kwamba watakosa wateja? Ni kampuni gani hiyo yenye hofu ya kukimbiwa na kwa nini wawe na hiyo hofu?

Nne, Ukitazama data za TCRA utaona kwamba trend ya mobile phone subscribers ya mwezi kwa mwezi kwa mwaka 2015 na 2016 inapanda na kushuka na sometimes inashuka significantly. Kwa mfano utaona kwamba January 2016 kulikua na wateja wengi kuliko March 2016..pia October 2016 kuna wateja zaidi ya laki 3 ukilinganisha na Dec 2016 huku Nov ikiwa na wateja kariu laki 4 zaidi ya Dec. Swali, unadhani ni kwa nini kuna hii fluctuation wakati miaka ya huko nyuma kumekua na significant increase ya wateja kutoka mwezi mmoja kwenda mwingine? Ni wazi kwamba moja ya sababu kubwa ni watu kununua kadi na kuzitupa pale wanapoona huduma ya kampuni fulani haiwafai na wengine walikua wamezinunua tu lakini hawaziwekei credit na kuzitumia huku Provider anapata hasara ya kuzilipia kuwa hewani. Kwa uelewa na uzoefu wangu wa soko la ICT (sio telecom peke yake) provider hawategemei cost of installation equipments (eg SIM in this case) kama strategic source of income bali wanategemea subscription fees mteja atakazolipia huduma. Hivyo kuniambia SIM ni source kubwa ya mapato hiya itakua ni poor strategic approach. Hakuna kampuni serious ya Telecom itategemea mapato ya kuuza SIM as a strategic source of income generation. Ukipiga hatua ukavuka mipaka ya Tz utagundua kwamba nchi zingine SIM haiuzwi bali mteja anapewa bure kama vile Tanesco wasivyokuuzia mita yao.

Kwa minajili hii ni bora kwa Providers kuwa na huduma ya watu kubadili providers with the same SIM kuliko provider kuwa na "Wateja Hewa" huku akizilipia lines kuwa hewani. It is logical kwamba mteja anayehamia kwako na line yake ana probability kubwa ya kuwa mteja wa kutegemewa (kununua huduma) kuliko mpya anayenunua line na usijue atakaa nayo muda gani. Kuuza lines nyingi sio determinant pekee ta income kwa provider bali ni hwo much subscribers are loyal in purchasing the services you provide.

Tano, una uelewa mpana kiasi gani kuhusu technical know how za mitambo ya telecom? Unaweza kuniambia kifaa/vifaa wanavyotakiwa kununua kufanikisha hili ni vipi na ni vya gharama gani? Na je, hizo gharama ni one time cost au watakua wanalipia for lifetime ya huduma.

MM

Nakushukuru kwa kunielewesha yote haya from a telecommunications perspective na lengo langu halikuwa kusema kuwa mawazo yako sio sahihi lakini nilipenda kukuonyesha kabla ya kupingana na issue ya kutoa malipo kuhama mtandao mwingine (mada yako kubwa) jaribu kuangalia hicho kitu kutoka upande wa kibiashara.

Kwa sababu nimeongea kinagaubaga bila kushika financial statements za haya makampuni hizo cost drivers zao nisingeweza kuzielezea vizuri ndio maana nikatoa theoretical expenses ujue kwa nini kuweka service charge ni kitu cha lazima but in short haya makampuni hayatengenezi faida kubwa sana mfano utaona kwa hali ya Tigo kufanya retrenchment na kubadili corporate structure yao kuokoa mapato hii inaonyesha tu dhahiri kuwa lazima kila service wanayoweka iwape faida hence kuweka charges maana kampuni isiyo na lengo la profit maximization in any way shape or form especially haya makampuni yenye investors basi hayafanyi kitu cha maana.

Kwenye hiyo moja ndio inayonihusu sana , hichi ni kitu dhahiri kuwa Tanzania has the lowest per data (per gigabyte) charge in Africa and ranks higher on the globe on Internet affordability. Kwa kusema UK hawana charges za kuhama mtandao na mimi kusema utakuta hizo service charge zime kuwa blanketed ndani ya Data plans simaanishi kuwa zipo ndani ya bei ya internet, la hasha nimemaanisha vipo ndani ya data plan in a sense kuwa vipo kwenye hivyo vifurushi vyao amabavyo ni monthly vinavyo include data, texts na talk (na hivi vifurushi sio affordable kwa Majibu ya matangazo ya 3, Vodafone n.k hata prices kwenye website yao) huwezi kusema charges hazipo wakati wanazi blanket unlike Tanzania na tayari kila kitu ni as affordable as possible (low cost model ) lazima hivi vitu sasa ucharge directly mfano mdogo wakukuonyesha hii low cost model na implementation of direct charges ni kwa mfano wa Precision Air au South African airlines na Fast Jet: Precision air au South African Airlines ukinunua ticket hata iwe mapema utakuta umelipia mzigo, na chakula lakini kwa Fast jet na low cost model yao ili ku recoup costs the former ni vya kulipia extra.. Sasa hii ni kama wewe kulalamika umelipia ticket bei ndogo na kumwambia muhudumu "Mbona nikinunua ticket Precision au SAA chakula ni bure!!" ndio hichi unachofanya sasa.
 
Kuna mambo mengi ambayo TCRA wangeyafanya kuboresha huduma Tanzania tena ambayo sio very costful ila wamekaa wanahangaika na vitu kama hivi ambavyo effect yake ni negligible. Hivi wanaofanya kazi TCRA ni akina nani? I'm very curious maana I seriously doubt their ability.
Kweli mkuu, wafanyakazi wa TCRA nahisi wanabahatisha sana.
 
Mkuu hawa watu wa mitandao ukiwapigia simu now hata hwapo haraka kupokea, sasa sijui ktk hyo itakuwaje. Tena ww umesema ndan ya masaa 2 wakati juzi TCRA walikuwa wanasema hadi siku 30 ndo utaweza kuhama.
 
Back
Top Bottom