TCRA na jeshi la Polisi, ganzi ya kushughulikia uhalifu huu inatoka wapi?

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,193
1,434
Moja ya majukumu ya kisheria ya Mamlaka ya Uthibiti wa Mawasiliano (TCRA) kama ilivyopewa na Tanzania Communication Regulatory Act Number 12 ya mwaka 2003 ni kulinda maslahi ya mteja (Protecting Consumer Interests). Kuna meseji ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsapp uliosema "Mates, you can always check/confirm your BVR details on your phone by dialing *152*00# and fololow instructions".

Ukifuata hayo maelekezo ama kupitia mtandao wa Vodacom au Tigo (sijui mitandao mingine ya simu) mwisho utapokea ujumbe unaosomeka "Ombi lako linashughulikiwa, utajulishwa kwa ujumbe mfupi (SMS) hivi punde. Kama taarifa sio sahihi fika na kadi yako wakati wa zoezi la uhakiki katika kata uliyojiandikisha" na nimeambiwa hiyo SMS haitakuja.

Baadae taarifa zimesambazwa kwamba kuna jinai inafanyika au itafanyika kupitia taarifa za kadi ya BVR ambayo mtu atatuma. Sijasikia kauli kutoka mamlaka husika (TCRA, Jeshi la Polisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi) juu ya hii sintofahamu dhidi ya wateja wa mitandao ya simu. Tanzania Cybercrime Act of 2015 ndio kazi yake.

Nakumbuka wakati wa kampeni za Uchaguzi mwaka 2010, kulikuwa na SMS za kampeni kwa CCM kwenda kwenye namba za simu za wateja bila ridhaa yao na pamoja na wateja kulalamika sana, mamlaka husika hazikuchukua hatua yoyote hata pale gazeti la Mwanahalisi lilipotoa hadi mtaa, namba ya nyumba na jina la mmiliki wa hiyo namba (mtoto wa mmoja wa wagombea urais mwaka huo) bado mamlaka husika hazikuchukua hatua yoyote.

Nakumbuka ile namba ni ya nchi fulani (nafikiri Finland) lakini tracking ilionyesha ina-operate kutokea Upanga,jijini Dar.

Juzi tumeshuhudia jeshi la Polisi likimkamata na kumfikisha mahakamani mtanzania aliye-post kwenye mtandao wa tanuru la fikra kwa sababu ya alichokiandika kiliwaudhi wakubwa wa serikali na Jeshi hilo. Naamini, TCRA na Jeshi la Polisi likitaka kumnasa mmiliki wa *152*00# hakika litamkamata ndani ya siku tatu.

Hapa naamini TCRA na mamlaka husika hazishughuliki na uhalifu kama huu wenye kunufaisha Chama Tawala CCM.

Hii ni mbaya sana kwa amani na usalama wa taifa letu.
 
Hii namba ni halali na imetolewa na tume ya uchaguzi kwa ajili ya kuhakiki, isipokuwa itafanya kazi pale tu uhakiki utakapoanza. Kwa mfano kama unaishi na umejiandikisha DSM ukisikia wametangaza kuwa uhakiki umeanza kwa wakazi wa DSM basi huna haja ya kwenda kwenye kituo ulipoandikishwa isipokuwa utapiga namba hiyo kuhakiki taarifa zako
 
Back
Top Bottom