TCRA mnaihujumu hii nchi aisee

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Nasikiliza hotuba ya Magufuli hapa alipokuwa anaongea na ma-RPC, TCRA na TRA kwa uzembe wa kutokusanya kodi tena kwa makusudi kabisa mnaitia hasara ya kutisha serikali.

According to Magufuli transaction fedha ya mwezi mmoja tu, mwezi March katika makampuni ya simu ilikuwa ni Trillioni 5.5

Hivi kama hali ndio hivi kama serikali ingechukua kama 5% ya transaction nzima maana yake ndani ya mwezi march pekee ingeingiza Tshs Billion 275.

TCRA kwa kushurikiana na makampuni ya simu hizi mnazofanya ni uhujumu uchumi aisee.

Ni haki kwa mkrugenzi wenu kutumbuliwa kabisa na kuburuzwa mahakamani na ikibidi kukagua mali za hawa watendaji wa hizi mamlaka na fedha wanazomiliki katika account zao za benki.
 
Wakurugenzi na Bodi wanafaa hata kupelekwa mahakamani kwa uzembe uliosababisha Tanzania kukosa mapato yake halali.

Usishangae kuna watu wanawatetea sana wakisema Rais amewadharirisha kuwafukuza kazi kwa sababu wana familia zinazohitaji msaada wao!

Tanzania ni nchi ya ajabu sana!
 
voda walikuwa wameiweka TCRA mkononi hawakuweza hata kufurukuta , kwa kifupi voda ndio waliokuwa wanachagua watu wa kwenda TCRA ili maslahi ya akina RA , patel , piter noni yaendelee , ED yaaendelee kulindwa
juzi kwenye chanel 10 nimemsikia MENEJA wa VODA kwa kujivunia kuchangia 3B KWA MIAKA MITATU nikachoka kweli
nikakumbuka 400B za kwetu walizotuibia
 
Nchi imeoza kabisa ndiyo maana watu walikata tamaa kusoma masomo ya sayansi maana wenyewe hela ni wanasheria, wahasibu, watawala n.k.
 
Nchi imeoza kabisa ndiyo maana watu walikata tamaa kusoma masomo ya sayansi maana wenyewe hela ni wanasheria, wahasibu, watawala n.k.

kesho kutwa tutawepelekea ANCRA watulipe chetu utasikia lakin utasikia Pro Edo wakianza kulalamika et matajiri huwa wanabembelezwa kulipa kodi huwa hawa sumbuliwi
 
Ni kweli kabisa mkuu, kuna mambo yanakera sana hii nchi.

Hawa wakurugenzi ilitakiwa wawe wameburuzwa mahakamani tu mpaka sasa, Billionin zaidi ya 200 upotea kwa sababu ya uzembe wao, wakati ni wasomi waliobobea kwenye nyanja zao ni hujuma za wazi kabisa
 
kesho kutwa tutawepelekea ANCRA watulipe chetu utasikia lakin utasikia Pro Edo wakianza kulalamika et matajiri huwa wanabembelezwa kulipa kodi huwa hawa sumbuliwi
teh teh teh
hizi ndizo fikra zinazodidimiza hii nchi.

Tajiri abembelezwe wakati anatumia rasilimali na miundombinu yetu kufanya biashara??
 
Nchi imeoza kabisa ndiyo maana watu walikata tamaa kusoma masomo ya sayansi maana wenyewe hela ni wanasheria, wahasibu, watawala n.k.
Cha ajabu hata hao wachache walio baki kwenye sayansi wanaacha fani zao wanajikita kwenye siasa.
 
voda walikuwa wameiweka TCRA mkononi hawakuweza hata kufurukuta , kwa kifupi voda ndio waliokuwa wanachagua watu wa kwenda TCRA ili maslahi ya akina RA , patel , piter noni yaendelee , ED yaaendelee kulindwa
juzi kwenye chanel 10 nimemsikia MENEJA wa VODA kwa kujivunia kuchangia 3B KWA MIAKA MITATU nikachoka kweli
nikakumbuka 400B za kwetu walizotuibia
Unajua nimekaa nikajiuliza sana, kwa nini makampuni ya simu yanafumuka kila siku hii nchi, ukiangalia ni nchi ya ulimwengu wa tatu na kipato cha wananchi ni cha chini mno, kumbe wanajua kwa ukwepaji kodi wananufaika sana.

Juzi tena nimesikia kuna kampuni la simu jipya linaitwa cocoTel limeshaingia mjini, na kuna mengine manne yanaanza kazi kabla ya mwezi June.

Hii nchi hii kweli shamba la bibi..
 
Nasikia hawa jamma akina wa TCRA wameanza kubadili majina kwenye mali na biashara zao.
 
Hela ina njia zake na taratibu zake, ukitaka kuwa nazo ni sharti uumize akili
 
Back
Top Bottom