TCRA mnafahamu utapeli huu mpya kutumia simu za mikononi?

TCRA mnafahamu utapeli huu mpya kutumia simu za mikononi?

bomouwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,149
Reaction score
800
Jamani habari za siku nyingi na niwatakie heri ya mwaka MPYA.

Ndugu zangu nimeona niwashirikishe juu ya utapeli na wizi wa kimtandao unaotumika sasa na mimi nikiwa muhanga wake.

Ninajishugulisha na biashara kadhaa ikiwemo ya hotel maeneo ya Ilala Bungoni, sasa manager wangu anayesimamia Hotel akapokea meseji toka kwenye namba yangu ya tigo ikimwambia "hujambo Sesi (jina si halisi), ebu tuma laki nne 400,000 katika hii namba (akapewa namba ya kutuma hiyo hela) halafu umwambie ni mimi nimekutuma, nipo kwenye kikao fanya haraka umtumie.

Hiyo msg ilikuwa majira ya saa 12:32pm kwakuwa namba ilikuwa yangu kabisa iliompa maelekezo manager wangu akatuma hiyo hela kwenye namba alioelekezwa, lakini ilipofika majira ya saa 03:18pm namba yangu tena ikatuma msg kumtaka aongeze laki 4 zingine kwenye namba ile ile.Bila kusita manager akatuma kwa hiyo jumla ikawa ni Tshs 800,000 zimetumwa ndani ya saa 12-03pm.

Sasa mimi sina habari juu ya lolote lililotokea, kwakuwa kila baaada ya siku mbili au tatu huwa naenda, siku hiyo nikaenda mida ya saa mbili na nusu usiku kufanya ukaguzi wa mahesabu sasa nikakuta laki 8 zimetoka na imeandikwa kabisa bosi.

Ikabidi nimuite anieleze hiyo hela imetokaje ndio akaanza kuniambia mambo ya msg kwa kweli sikumuelewa lakini ni mtu ambae nimekuwa naye kwa miaka 5.

Yani jamani msg niliiona ni namba yangu kabisa na ujumbe nilivyosoma hata kama ni mie ndio ningekua manager ningetoa hiyo hela. Sasa nikaongea na polisi mmoja akaniambia niende kituoni na manager then tukapata RB then wakatupa karatasi tukaenda tigo.

Sasa pale TiGo wakasema huu wizi upo na tahadhari yake ili kujua kwamba hiyo namba si ya huyo unaemjua hii namba ya matapeli haianzi na PLUS SIGN(+) YAAN ITAKUA 255XXXXXXXX LAKINI namba orijino itakuwa +255xxxxxxxxxx.

Ndugu zangu wa TCRA pamoja na kitengo cha wizi wa mitandaoni cha jeshi la polisi hali inakuwa mbaya na raia wengi wataumia.

Naomba kuwasilisha
 
Pole sana sasa hivi kila sekta kuna ufisadi
 
Ndugu yangu bomouwa sina lakusema, inasikitisha POLE sana.... mezea tu ndo biashara hasara na faida!!
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru nimejaribu kuwajuza tu ili muwe makini tusilie wengi
 
Mswada wa sheria ya uhalifu wa mitandao umekaliwa tu na serikali, mwaka wa tatu sasa wanaupiga tu danadana halafu eti naibu waziri wa wizara husika anajifanya ni mchapa kazi kiasi cha kutaka kupewa kiti cha uraisi wa JMT kwenye uchaguzi mkuu ujao.
 
Hizo ulizipata au ikawaje? main huk mwish cjakuelew....after all pole sann
hakuna nilichopata zaidi ya rb kumtafta mtu alieingiziwa hizo hela maana jina lilionyesha lakini namba haipatikani na tigo wakasema wanafungia hiyo namba lakini kimsingi nimemuachia Mungu
 
Ahsante sana kwa kutujuza.

Pole sana.

TCRA wako pale kula tu.
 
Na mbaya zaidi wanajua na namba za kitapeli lakini wanashindwa kudhiti.
 
Alafu kwanini ni tigo tu ndio huwa sakata hili la wizi wa kimtandao linahusika zaidi
 
hakuna nilichopata zaidi ya rb kumtafta mtu alieingiziwa hizo hela maatna jina lilionyesha lakini namba haipatikani na tigo wakasema wanafungia hiyo namba lakini kimsingi nimemuachia Mungu
Wacha ujinga wewe kilichotumwa ni meseji ya kuhamisha pesa tu na siyo fedha taslimu. Hiyo haiwezi kutumika bila ya kutoa au kuhamishia kwenye akaunti nyingine. Na hayo yote yakifanyika lazima watoa huduma wawe na records na usalama wa pesa zako ni jukumu lao.Komaa urudishiwe pesa yako labda kama ni ya urithi au mgao wa xcrow ndiyo uiache. Tusiwe wajinga wa kuibiwa kizembezembe wakati kuna watu tunawalipa kuhakikisha usalama wa fedha zetu
 
Wacha ujinga wewe kilichotumwa ni meseji ya kuhamisha pesa tu na siyo fedha taslimu. Hiyo haiwezi kutumika bila ya kutoa au kuhamishia kwenye akaunti nyingine. Na hayo yote yakifanyika lazima watoa huduma wawe na records na usalama wa pesa zako ni jukumu lao.Komaa urudishiwe pesa yako labda kama ni ya urithi au mgao wa xcrow ndiyo uiache. Tusiwe wajinga wa kuibiwa kizembezembe wakati kuna watu tunawalipa kuhakikisha usalama wa fedha zetu
mungu akubariki
 
Pole sana. Sio TCRA pekee bali pia nadhani watunga sheria bado hawajawa tayari na haya mambo ya mitandao. Kunatakiwa kuwe na sheria ambazo zitamlinda mtumiaji. Hapo kimantiki, hasara ilitakiwa iwe ya tigo na sio ya mtumiaji. Tena hata wao hawana hasara kama sheria zinawalazimisha kuwekea bima mambo kama hayo. Wanalipwa na bima na bima wanakuwa hawajapata hasara kwa kuwa wanarudisha kidogo kati ya kikubwa walichopewa. Na kukiwa na kulipishana lazima watakuna vichwa na kubuni nia mbalimbali za kupambana na uhalifu wa mitandaoni.
 
Back
Top Bottom