Kobaba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 492
- 344
Anibariki kwa lipi? Mbona sihusiki huko? Mimi Sijaiba wala kuibiwa
Jina linaenda sambamba na maneno yako.
Anibariki kwa lipi? Mbona sihusiki huko? Mimi Sijaiba wala kuibiwa
Jamani habari za siku nyingi na niwatakie heri ya mwaka MPYA.
Ndugu zangu nimeona niwashirikishe juu ya utapeli na wizi wa kimtandao unaotumika sasa na mimi nikiwa muhanga wake.
Ninajishugulisha na biashara kadhaa ikiwemo ya hotel maeneo ya Ilala Bungoni, sasa manager wangu anayesimamia Hotel akapokea meseji toka kwenye namba yangu ya tigo ikimwambia "hujambo Sesi (jina si halisi), ebu tuma laki nne 400,000 katika hii namba (akapewa namba ya kutuma hiyo hela) halafu umwambie ni mimi nimekutuma, nipo kwenye kikao fanya haraka umtumie.
Hiyo msg ilikuwa majira ya saa 12:32pm kwakuwa namba ilikuwa yangu kabisa iliompa maelekezo manager wangu akatuma hiyo hela kwenye namba alioelekezwa, lakini ilipofika majira ya saa 03:18pm namba yangu tena ikatuma msg kumtaka aongeze laki 4 zingine kwenye namba ile ile.Bila kusita manager akatuma kwa hiyo jumla ikawa ni Tshs 800,000 zimetumwa ndani ya saa 12-03pm.
Sasa mimi sina habari juu ya lolote lililotokea, kwakuwa kila baaada ya siku mbili au tatu huwa naenda, siku hiyo nikaenda mida ya saa mbili na nusu usiku kufanya ukaguzi wa mahesabu sasa nikakuta laki 8 zimetoka na imeandikwa kabisa bosi.
Ikabidi nimuite anieleze hiyo hela imetokaje ndio akaanza kuniambia mambo ya msg kwa kweli sikumuelewa lakini ni mtu ambae nimekuwa naye kwa miaka 5.
Yani jamani msg niliiona ni namba yangu kabisa na ujumbe nilivyosoma hata kama ni mie ndio ningekua manager ningetoa hiyo hela. Sasa nikaongea na polisi mmoja akaniambia niende kituoni na manager then tukapata RB then wakatupa karatasi tukaenda tigo.
Sasa pale TiGo wakasema huu wizi upo na tahadhari yake ili kujua kwamba hiyo namba si ya huyo unaemjua hii namba ya matapeli haianzi na PLUS SIGN(+) YAAN ITAKUA 255XXXXXXXX LAKINI namba orijino itakuwa +255xxxxxxxxxx.
Ndugu zangu wa TCRA pamoja na kitengo cha wizi wa mitandaoni cha jeshi la polisi hali inakuwa mbaya na raia wengi wataumia.
Naomba kuwasilisha
Wale IT wa Tigo wanausika kwa 100%.
Wanaangalia namba yenye pesa then wanatafta namba inayopendelea kuipigia kisha wanatafta uhusiano baina ya hz namba. After all, pole sana but ukiwabana Tigo pesa yako inarudi.
Pole sana ndg niwasaidie tu kuwa sheria ya kupambana na uhalifu wa mtandao ni muhimu ila haitakusaidia kama hatuna mfumo mzuri na wa kisasa wa kimtandao kudhibiti huo wizi.Pili elimu kwa umma ndiyo itakayotusaidia kuwa salama na wizi wa kimtandao,usiwe mwepesi kutoa fedha,password au account yako,tena usijidanganye kuwa bila password hawataweza kukuibia.Cyber law ni muhimu sana pia elimu ni muhimu zaidi.Karibuni chuo kikuu mlimani tusome BALE mtayafahamu hayo yote.
Wacha ujinga wewe kilichotumwa ni meseji ya kuhamisha pesa tu na siyo fedha taslimu. Hiyo haiwezi kutumika bila ya kutoa au kuhamishia kwenye akaunti nyingine. Na hayo yote yakifanyika lazima watoa huduma wawe na records na usalama wa pesa zako ni jukumu lao.Komaa urudishiwe pesa yako labda kama ni ya urithi au mgao wa xcrow ndiyo uiache. Tusiwe wajinga wa kuibiwa kizembezembe wakati kuna watu tunawalipa kuhakikisha usalama wa fedha zetu
Nashukuru nimejaribu kuwajuza tu ili muwe makini tusilie wengi
Wale IT wa Tigo wanausika kwa 100%.
Wanaangalia namba yenye pesa then wanatafta namba inayopendelea kuipigia kisha wanatafta uhusiano baina ya hz namba. After all, pole sana but ukiwabana Tigo pesa yako inarudi.
hivi kwann asijilizishe kwa kukupigia kwanza ili ajue ni kweli umemtumia hiyo sms au huwa munatumiana kwa njia hiyo bila kuulizana???????????????????????
Anibariki kwa lipi? Mbona sihusiki huko? Mimi Sijaiba wala kuibiwa
Tunatamani ila ndo hivo hata qualification za kusoma veta hatuna mkuuPole sana ndg niwasaidie tu kuwa sheria ya kupambana na uhalifu wa mtandao ni muhimu ila haitakusaidia kama hatuna mfumo mzuri na wa kisasa wa kimtandao kudhibiti huo wizi.Pili elimu kwa umma ndiyo itakayotusaidia kuwa salama na wizi wa kimtandao,usiwe mwepesi kutoa fedha,password au account yako,tena usijidanganye kuwa bila password hawataweza kukuibia.Cyber law ni muhimu sana pia elimu ni muhimu zaidi.Karibuni chuo kikuu mlimani tusome BALE mtayafahamu hayo yote.