TCRA mko wapi mpaka hiki kinatokea ?

TCRA mko wapi mpaka hiki kinatokea ?

how comes zingekuwa sms za pesa kutoka ktk hizo kampuni??

natania tu jamani.....hata mimi nakereka na hiyo mi sms though nabet
 
Ni kweli kabisa haistahiki kutumiwa vitu tusivyovitaka hususan kamari katika simu zetu. Na hapa inaonekana kuna biashara kati ya makampuni ya simu na haya makampuni ya kamari katika kufikisha taarifa zao kwa watumiaji wa simu. Hiki kitu hakifurahishi na kinapaswa kukomeshwa na TCRA!
 
Blazaeee chi ungeacha kwancha wamaliche ile moja ya kuonyecha TV za ndani bulee!? chacha unawaogechea lingine wakati ile amli yao ya tv cha ndani halijatekelechwa?
 
Basi mi kila nkiamka asubuhi nakuta wameshantumia,mchana nkishika cm nakutana na msg zao,jioni wapoo yan doh!!!hate bebe hanitumii msg kiasi hicho loh!
 
Hao moja bet wananikera hakuna mfano.......... Hadi Saa saba usiku wanakutumia huo ujinga wao, ukiamkaa tu asubuhi unakutana na upuuzi wao tena.

Bora wangekuwa wakikutumia hizo SMS wanaweka na namna ya kujitoa ili usiwe unatumiwa huu UJINGA.

TCRA waamke sasa tumechoshwa na huu upuuzi.
Absolutely
 
Blazaeee chi ungeacha kwancha wamaliche ile moja ya kuonyecha TV za ndani bulee!? chacha unawaogechea lingine wakati ile amli yao ya tv cha ndani halijatekelechwa?
Nimecheka Sana
 
Ujumbe wa aina hiyo pia ni lazima uwe na namba ya mtu kujiondoa asipokee ujumbe wao tena na pia iwe bure kufanya hivyo..
 
Kumbe tupo wengi tunao kereka na hawa matapeli,unasikia mlio wa msg unaacha shughul zako ,unakuta ujumbe wa kipuuzi,me na kamali wapi na wapi?cku hizi wala sisomi nafuta juu kwa juu bila kujua wanasemaje maana wana bore.
 
Mkuu MUUZA NGADA fahamu kwamba hayo makampuni ya simu yanafanya biashara ya kutangaza matangazo ya hayo makampuni ya kamali. Hiyo ni biashara ya matangazo na hizo sms zimeshalipiwa tayari ndiyo maana VODACOM au kampuni yoyote ile ya simu hawawezi kuzizuia. Hii biashara inawaingizia pesa mingi sana ndiyo maana wewe ulipoenda kuwauliza wamekuzungusha tu, lakini wanajua ukweli wote kuwa wao ndiyo waliotoa hizo namba za wateja kwa makubaliano maalumu ya kulipwa.

Kiutaratibu ninavyo fahamu mimi namba ya simu unayoimiliki siyo mali yako, bali ni mali ya SERVICE PROVIDER uliyejiunga naye kama ni VODACOM, AIRTELL, HALLOTELL n.k. hawa ndiyo wamiliki halali wa hizo namba za simu. Literally tunaweza kusema namba za simu ni mali yetu, but technically zinamilikiwa na makampuni ya simu.
 
MUUZA NGADA Jibu la swali lako ni baadhi ya wafanya kazi wa makampuni ya mitandao. Huu mtindo uko karibu dunia nzima na sio tatizo la Tanzania tu.

Baadhi ya wafanya kazi wa makampuni hayo ya mitandao wana access kwenye data za wateja kwa hiyo wao ndiyo wana wanawauzia hizo data hao wachezeshaji wa kamali. Makampuni ya mitandao haiwezi kufanya upuuzi kama huo wa kuuza data za customers wao na kuingiza kampuni kwenye risk.

Usihangaike sana nasikia kuna njia ya ku-block wahujumu hao. Uliza kwa wataalam wa IT watakusaidia.
 
Jibu la swali lako ni baadhi ya wafanya kazi wa makampuni ya mitandao. Huu mtindo uko karibu dunia nzima na sio tatizo la Tanzania tu.

Baadhi ya wafanya kazi wa makampuni hayo ya mitandao wana access kwenye data za wateja kwa hiyo wao ndiyo wana wanawauzia hizo data hao wachezeshaji wa kamali. Makampuni ya mitandao haiwezi kufanya upuuzi kama huo wa kuuza data za customers wao na kuingiza kampuni kwenye risk.

Usihangaike sana nasikia kuna njia ya ku-block wahujumu hao. Uliza kwa wataalam wa IT watakusaidia.
Hakuna mwanasheria hapa atutengezee shitaka tuburuzane kisutu! Tatzo wanasheria wetu ni tofaut na nchi zilizoendelea vitu sensitive hata huwaoni

elewa kwanza
 
Kwao hili sio kosa, kosa ni kuikosoa serikali tu, vinginevyo mtu anaweza kufanya anachotaka kwa namba yako
 
Back
Top Bottom