TCRA mko wapi mpaka hiki kinatokea ?

TCRA mko wapi mpaka hiki kinatokea ?

Yani hizo sms zao zina kera mimi na pata sio chini ya sms 8 kila siku nimejaribu kuziblock ila sija fanikiwa. TCRA tunaomba mwangalie hili swala halija kaa vizuri sana
 
Kwa sheria ya TCRA iliyofanyiwa marekebisha miaka miwili iliyopita ni kweli unayo haki ya kuwashitaki wote wawili yaani; mtandao wa simu na kampuni ya waendesha kamali wenyewe.

Tatizo, lipo hapa
Kwanza, Je, una uhakika hakuna mtu ulimpatia simu yako akacheza kamali kwa namba yako!?

Pili, Wamiliki wa kampuni nyingi za simu ni vigogo , je uko tayari kulipwa let's say 10/=M au zaidi halafu tukuokote coco beach kwenye kiroba ukiwa tayari umeoza!?

Japo, matangazo yanaudhi sana.

Tusisahau hili ;

We need an immediate justice for our daughter Akwilina B.

Management ya NEC na DED wa Kinondoni watumbuliwe, wakamatwe na wafungwe kwa kusababisha kifo cha Binti Akwilina B.

CCM must go...

Kagame must be stopped visiting Tanzania

R.I.P, Binti yetu , Akwilina B
Ndoto zako zote zimezimwa ghafula kama vile mshumaa uzimwavyo.

Daima tutakukumbuka Binti, Kristo Yesu akuangazie mwangaza wake wa milele. Amina.
 
Mi nimeziblock hizo sms zotee,sms yoyote ikiingia inayohusu mambo ya kubet nablock hapohapo
 
Kwao hili sio kosa, kosa ni kuikosoa serikali tu, vinginevyo mtu anaweza kufanya anachotaka kwa namba yako
Sisi ndo tunaiweka madarakani, iweje tukose wajibu wakuikosoa? Kwani katiba inatuzuia kuikosoa inapokengeuka? Wanashera wa nchi hii chomeni vyeti vyenu kwani havina tija. Watu wanaingizwa madarakani na wananchi lkn hawana ubavu wa kukosoa!!
 
Ndugu yangu;Namba ya simu ya mtu kupatikana sio lazima kutoka vodacom.Inawezekana namba yako imepatikana kwa bahati tu kama ilivyo kamari ni bahati.
 
Kaka unaonaje tufungue kesi mahakamani...

Ni kweli kuwa sisi tunaoudhiwa na wapuuzi hawa tungeliweza kufungua kesi mahakamani lakini sasa tumshitaki nani?? Ndo maana tumeomba TCRA wawakataze watu hawa tena kwa njia ambayo hata sisi tutatambua kuwa tiyari wesha onywa hivyo wakikaidi ndio sasa tuweze fungua hayo madai.

We wadhani ni huyu bwana tu kachukia lakini kumbe tupo wengi. Mtu hudanganywa na hizo meseji hadi siku moja anasema; Ngoja nami niijaribu bahati. Fikiri kama kiila siku, utapata meseji 2 baada ya muda utaacha kughafilika?? Kwa nini basi wasi tusaidie hata kutulipia sms 10 kwa siku?
 
Labda tuwaulize makampuni yetu ya mitandao kua je kuna chochote wanapata au kufaidika kutoka kwenye haya makampuni ya bahati nasibu? Je wanatangaza biashara zao bure?
 
Mkuu MUUZA NGADA fahamu kwamba hayo makampuni ya simu yanafanya biashara ya kutangaza matangazo ya hayo makampuni ya kamali. Hiyo ni biashara ya matangazo na hizo sms zimeshalipiwa tayari ndiyo maana VODACOM au kampuni yoyote ile ya simu hawawezi kuzizuia. Hii biashara inawaingizia pesa mingi sana ndiyo maana wewe ulipoenda kuwauliza wamekuzungusha tu, lakini wanajua ukweli wote kuwa wao ndiyo waliotoa hizo namba za wateja kwa makubaliano maalumu ya kulipwa.

Kiutaratibu ninavyo fahamu mimi namba ya simu unayoimiliki siyo mali yako, bali ni mali ya SERVICE PROVIDER uliyejiunga naye kama ni VODACOM, AIRTELL, HALLOTELL n.k. hawa ndiyo wamiliki halali wa hizo namba za simu. Literally tunaweza kusema namba za simu ni mali yetu, but technically zinamilikiwa na makampuni ya simu.
Absolutely
 
Kwa sheria ya TCRA iliyofanyiwa marekebisha miaka miwili iliyopita ni kweli unayo haki ya kuwashitaki wote wawili yaani; mtandao wa simu na kampuni ya waendesha kamali wenyewe.

Tatizo, lipo hapa
Kwanza, Je, una uhakika hakuna mtu ulimpatia simu yako akacheka kamali kwa namba yako!?

Pili, Wamiliki wa kampuni nyingi za simu ni vigogo , je uko tayari kulipwa let's say 10/=M au zaidi halafu tukuokote coco beach kwenye kiroba ukiwa tayari umeoza!?

Japo, matangazo yanaudhi sana.

Tusisahau hili ;

We need an immediate justice for our daughter Akwilina B.

Management ya NEC na DED wa Kinondoni watumbuliwe, wakamatwe na wafungwe kwa kusababisha kifo cha Binti Akwilina B.

CCM must go...

Kagame must be stopped visiting Tanzania

R.I.P, Binti yetu , Akwilina B
Ndoto zako zote zimezimwa ghafula kama vile mshumaa uzimwavyo.

Daima tutakukumbuka Binti, Kristo Yesu akuangazie mwangaza wake wa milele. Amina.
 
i) Haya Makampuni Yanapewa na Nani Namba Yangu mpaka Wakaweza Kumudu Kunitumia Ujumbe??

Aliyekuambia namba ya simu unayotumia ni ya kwako ni nani? Someni kwanza zile karatasi za makubaliano utajua unachomiliki wewe ni handset yako tu. Wenye namba ni mtandao.
 
Aliyekuambia namba ya simu unayotumia ni ya kwako ni nani? Someni kwanza zile karatasi za makubaliano utajua unachomiliki wewe ni handset yako tu. Wenye namba ni mtandao.
Ok, Kwahyo Wanaweza Kutoa Kwa Mtu Yeyote Muda Wowote?
 
Halafu ukiandika ONDOA ukatuma kwenye hiyo namba uliyopewa wanakujibu HUJAJIUNGA bado hivyo wanaendelea kukutumia, inaumiza sana kwa nini tulazimishwe kila kitu? Kila kitu Mungu nisamehe naipenda nchi yangu lakini sipendi yanayoendelea sasa, hawa TCRA wamebaki ukiropoka wanakudaka mengine hawayaoni kabisa maana hizi Meseji nina uhakika hata wao wanatumiwa lakini sidhani hata kama kuna anayeona ni usumbufu kwa raia, TV watu wamelalamika warudishie zile channel za bure wametulia kama hawasikii malalamiko ya watu kwani hawa TCRA wapo kwa faida ya nani? Tujue moja ili tusizidi kuwasumbua
 
Hiwezi pata sms Kama hujawai cheza wewe ni zuzu
Mimi pia napata, nadhani Zuzu ni wewe uliyekurupuka kutetea upuuzi mnaotufanyia, Mimi nicheze hiyo mitakataka kwa Kipi? Japo sina uwezo kipesa lakini kutupa pesa yangu kipuuzi hivyo nimetoka kwetu kutafuta pesa sio kutupa pesa, Meseji zimekuwa usumbufu wewe unatetea tena kwa lugha chafu! Unawaambia ONDOA majibu ni kama hapo juu sasa kama sijajiunga wananitumia ya nini?
 
Itakua sheria inawaruhusu kucheza na namba zetu za simu wanavyotaka? Kwa sababu kuna waganga wa jadi nao hunitumia sms
 
Hapa ni kwamba haya makampuni ya bahati nasibu na ku-bet pamoja na mengineyo yanayotumia sms kutangaza bidhaa zao wanayalipa hayo makampuni ya simu ili kutumia platform zao.
So hii ni biashara kati ya mwenyebidhaa na mtoa huduma ya matangazo. Hapa lazima TCRA waingie kutulinda walaji maana watu wanafanya biashara zao kwa gharama za mlaji.
 
Siku hizi pia kuna matangazo ya waganga wakienyeji nayo ni kero nyingine
 
Back
Top Bottom