astalavista
JF-Expert Member
- Jul 7, 2014
- 261
- 304
Nafahamu weledi ni tatizo kwenye 'media' nyingi sasa hivi, imekuwa ni kawaida kutozingatia misingi na miiko ya taaluma ya habari. Mtama Fm ni miongoni mwa sehemu ya aibu kwa vyombo vyetu vya habari nchini.
Pamoja na uchanga wake lakini si sahihi kuacha watangazaji wenye makosa ya wazi ya matamshi, tatizo la R na L ni la kitaifa lakini kwenye chombo hiki cha habari ni zaidi.
Ipo wazi kwa mikoa ya kusini kuna changamoto ya kutamka M, kmv Mtoto/Ntoto. Makosa haya ya matamshi hayakutakiwa yaje kwenye radio, sehemu ambayo tunaamini makosa yatakuwa machache.
Rai yangu kwa TCRA tafadhalini kuweni karibu na hivi vyombo vya habari hasa vichanga ili kuhakikisha maudhuhi kwa hadhira yanaenda pasipo kunajisiwa kiswahili chetu.
Rai yangu kwa wahusika kiutawala Mtama Fm zingatieni weledi na miiko ya taaluma kwa kuwa na angalau mtu mmoja mwenye taaluma ambaye ataweza kuwashape wengine kwenye njia nzuri.