TCRA: Hatutawalipa fidia wenye simu feki na wala hatutaongeza muda wa kuzima simu hizo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Wakati siku ya kuzimwa kwa simu feki ikikaribia,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA),imesema haina mpango wa kuongeza siku za kuzima simu hizo wala haitahusika kulipa fidia kwa watakaoathirika baada ya simu zao kuzimwa.

Jana Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Vijana CUF(JUVICUF),Mahamoud Mahinda,aliitaka serikali kubeba mzigo wa kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuruhusu uingizaji wa simu feki nchini.

Mahinda,alisema serikali ilishindwa kutimiza wajibu wa kuhakikisha simu hizo haziingizwi nchini,hivyo inapaswa kuwajibika,na kuwaacha wananchi kununua simu feki siku za nyuma bila ya kudhibiti uingizwaji wake nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi,mara baada ya semina ya kwa umma juu ya ufahamu wa mfumo wa rajisi wa namba za utambulishi wa simu za kiganjani mkoani Geita,Meneja wa TCRA nchini Innocent Mungy alisema mamlaka hiyo haina mpango wa kuwalipa fidia wenye simu feki.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TCRA James Kilaba,Mungy, alisema ifikapo Juni 16 simu hizo zitafungwa.

"Kipindi cha Mpito(Transition period) cha kuelimisha umma pamoja na zoezi la wateja kuhakiki simu walizo nazo au wakati wanataka kununua simu mpya lilianza mwezi disemba mwaka jana wakati huo mfumo ulipozinduliwa na itamalizika Juni 16"alisema Mungy.

Alisema,ikifika saa 6 usiku Juni 16,mwaka huu simu hizo zitafungwa,na wala TCRA haikusudii kuongeza muda wa kuzima simu hizo ,na mtu atayekaa na simu feki akikamatwa atachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: Mwananchi online
 
Wamezuia bunge laivu,wanazima na simu tena,sijui ninunue simu au sukari kwanza?simu yangu na mama.watoto.haipingui laki mbili, anyway ngoja tununue zenye Wasap ili tuhamasishane kuiondoa CCM madarakani kupitia ma group ya Wasap,tuzipate clip za Lema,Lisu,Msigwa,Sugu....CCM wanafikiri wanatukomoa kumbe wanapanda mbegu ya kuwaondoa
 
Nani ambae hataisoma namba?
Wafanya biashara ambao wamehifadhi simu nyingi ambazo ni feki na watakuwa wameshindwa kuziuza kabla ya June 16, 2016; na walionunua simu feki maana itawapasa kununua simu nyingine kwa bei ya juu zaidi.

Hata hivyo wenye simu original watapiga hela ya ukweli kwa kupandisha bei bei ya simu original.

Japo kwa muda mfupi watanzania wengi wataumia lakini hatimaye mambo yatakuwa mazuri.
 
Wakati siku ya kuzimwa kwa simu feki ikikaribia,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA),imesema haina mpango wa kuongeza siku za kuzima simu hizo wala haitahusika kulipa fidia kwa watakaoathirika baada ya simu zao kuzimwa.

Jana Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Vijana CUF(JUVICUF),Mahamoud Mahinda,aliitaka serikali kubeba mzigo wa kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuruhusu uingizaji wa simu feki nchini.

Mahinda,alisema serikali ilishindwa kutimiza wajibu wa kuhakikisha simu hizo haziingizwi nchini,hivyo inapaswa kuwajibika,na kuwaacha wananchi kununua simu feki siku za nyuma bila ya kudhibiti uingizwaji wake nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi,mara baada ya semina ya kwa umma juu ya ufahamu wa mfumo wa rajisi wa namba za utambulishi wa simu za kiganjani mkoani Geita,Meneja wa TCRA nchini Innocent Mungy alisema mamlaka hiyo haina mpango wa kuwalipa fidia wenye simu feki.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TCRA James Kilaba,Mungy, alisema ifikapo Juni 16 simu hizo zitafungwa.

"Kipindi cha Mpito(Transition period) cha kuelimisha umma pamoja na zoezi la wateja kuhakiki simu walizo nazo au wakati wanataka kununua simu mpya lilianza mwezi disemba mwaka jana wakati huo mfumo ulipozinduliwa na itamalizika Juni 16"alisema Mungy.

Alisema,ikifika saa 6 usiku Juni 16,mwaka huu simu hizo zitafungwa,na wala TCRA haikusudii kuongeza muda wa kuzima simu hizo ,na mtu atayekaa na simu feki akikamatwa atachukuliwa hatua za kisheria.
Vipi mamlaka yaliokuwa yanakagua ubora wa simu kabla ya kuingia nchini?
 
kuzima simu feki ni haki kwa serikali kwani ziliingia kwa magendo, wewe simu inaitwa panyasonic, nokla, sungusungi sonyo ericton alafu utakuta videmu vimebeba lisimu kubwa eti kanachati, tarehe 16 june ndio mwisho wa nyodo za kuchati.
usiseme hivo mkuu,watu wana mengi moyoni ya kusema ww hujui tu,maisha haya watu tunatoka sehemu tofauti na kipato tofauti
 
Wana JF,

TCRA imesistiza kuwa haitaongeza muda kwa wale wenye simu feki, hata hivyo haijafafanua zaidi kwa nini simu nyingine kama halotel zinazouzwa na kampuni zinaonekana kutotambulika.

June 16 huenda ukawa mwisho wa nyodo kwa wale wenye simu kubwa tablet ambazo walikuwa wanalingia wanapokuwa kwenye usafiri wa umma, utakuta mdada ana simu inamshinda kwa uzito lakini akiwa kwenye basi ufungua begi lake na kuanza kuchati, simu hizo uonekana za gharama kumbe vinauzwa tshs 120,000/= kwa vijana pale kariakoo au posta, kuna watu wamepigwa sana na iphone feki, sony z1, z3 , htc na LG ambazo huwezi kuzijua , watu wamepigwa sana kwa samsungi, serikali imeamua kuingilia kati kwani watu wengi wamepata hasara sana , hata mafundi wameshindwa kufanya kazi zao kutokana na kufoji simu kuliko pitiliza.
 
kuzima simu feki ni haki kwa serikali kwani ziliingia kwa magendo, wewe simu inaitwa panyasonic, nokla, sungusungi sonyo ericton alafu utakuta videmu vimebeba lisimu kubwa eti kanachati, tarehe 16 june ndio mwisho wa nyodo za kuchati.
hahahahahahah, eti panyasonic
 
Kwa hiyo hapa ni wivu au ndio hasira inayosababishwa na kukosa sukari mwilini?
 
Wamezuia bunge laivu,wanazima na simu tena,sijui ninunue simu au sukari kwanza?simu yangu na mama.watoto.haipingui laki mbili, anyway ngoja tununue zenye Wasap ili tuhamasishane kuiondoa ccm.madarakani kupitia ma group ya Wasap,tuzipate clip za lema,lisu,msigwa,sugu....Ccm wanafikiri wanatukomoa kumbe wanapanda mbegu ya kuwaondoa

angalia usiishie jela kwa sheria ya mtandao kupitia hiyo whatsapp
 
kuzima simu feki ni haki kwa serikali kwani ziliingia kwa magendo, wewe simu inaitwa panyasonic, nokla, sungusungi sonyo ericton alafu utakuta videmu vimebeba lisimu kubwa eti kanachati, tarehe 16 june ndio mwisho wa nyodo za kuchati.

Bwaaaahahaaaaa, nimecheka ile mbaya, halafu hizo simu fake nasikia eti zinaita hata zikiwa off!!
 
Hakuna kuongeza siku kwani imetuasiri sana wafanya biashara wa sim wengine tunauza OG lakini hatufanyi biashara coz watu wanaogopa kununua kwahiyo hali zetu ni mbaya sana serikali kama ikiongeza muda basi ije utulipie kod za frem mana tutashindwa kulipa kodi
 
Back
Top Bottom