TCRA angalieni hiki kipindi cha redio wanakiita Shujaaz, watoto wadogo wanaongelea mapenzi

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,271
2,401
Ni kutoka radio frequency 90.0 cha saa tisa alasiri Jumamosi.

Ni vitoto vidogo lakini vinajadili masuala ya mahaba, muda usio sawa. Mbaya zaidi ni vitoto ambavyo havina uhalali wa kuwa katika mahusiano kwa umri wao, weka pembeni kuyaweka wazi, mbaya zaidi kwenye radio.

Angalieni hili. Pengine wana mada zingine nzuri ila kwa masuala ya mapenzi hawana vigezo na sababu ya kuzungumzia.

Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TV zinaonyesha uchafu,Magazeti ya udaku uchafu mtupu,, Nyimbo za matusi AKA wasanii/ Bongo fleva ;Radio,Mabasi, Daladala, matusi kila mahali ndio mwalimu wao.
TCRA ipo, viongozi wapo, watu wote tupo. Hakuna anayechukua hatua maadili ndio hayo sasa. Inasikitisha
 
Nadhani TBC FM Kama Nitakuwa Sahihi Ila Naweza Kusahihishwa Iwapo Siko Sawa
Ni Radio kibao zinarusha kuna EA radio, Aboody FM pamoja na hiyo uliyoitaja na zingine mbili.
.
Alafu hakuna mtoto pale Allan lucky ni mtu mzima sana ambae ndie mwenye kipindi baada ya kuachana na Skonga, Pendo sio mtoto nae.
.
Kwa ufahamu zaidi mleta mada tembelea Page ya Dj tee Facebook au page ya Pendo Facebook.
Au waweza kumfuata Allan lucky Instagram.
 
Mkuu naomba kujua ni radio gani hiyo allan lucky ni mtangazaji???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shujaaz na Niambie ni vipindi vya nje haviko chini ya radio moja ,viko chini ya mradi Fulani hivi unadhaminiwa na baadhi ya mashirika ya kimataifa

Lengo Kuu nadhani ni elimu kwa vijana, mahusiano na namna ya kujikinga na maambukizi

MTC | 101|
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom