Tchangirai:Uchaguzi 'Kichekesho Kikubwa'

Tchangirai:Uchaguzi 'Kichekesho Kikubwa'

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,477
Reaction score
21,039
130801131400_morgan_vote_counting_304x171_bbc_nocredit.jpg
Uchaguzi wa Rais nchini Zimbabwe ulikuwa ‘kichekesho kikubwa,’ Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema, akituhumu udanganyifu wa kura uliofanywa na kambi ya mpinzani wake Rais Robert Mugabe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Tsvangirai alisema uupigaji kura wa Jumatano ulikuwa ‘upuuzi na si halali’.
Kundi kubwa la waangalizi mapema lilisema kufikia hadi watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Chama cha Bw Mugabe ambacho kinadai kushinda, kimekanusha tuhuma hizo kikisema upigaji kura ulikuwa shwari.
Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, alisemsa kwenye tathimini yao ya awali kuwa upigaji kura ulikuwa huru na haki.
Makundi mengine ya waangalizi yalisifia hali ya amani katika uchaguzi huo.
Kuhesabu kura ulianza kulianza usiku na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) ina siku tano za kutangaza nani mshindi katika uchaguzi huo.
Tayari polisi wameonya kuwa watachukua hatua dhidi ya yeyote atakayejaribu kuvujisha habari za matokeo. Ni kinyume cha sheria kutangaza matokeo yasiyo rasmi.
Vikosi vya ziada baadhi vikiwa na vifaa vya kupambana na waandamanaji tayari viko mjini Harare.
Hatua za kisheria huenda zikafuata sasa, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Andrew Harding akiripoti kutoka Johannesburg.
Lakini megi yatategemea iwapo majirani wa Zimbabwe watapitisha uchaguzi huo, mwandishi wa BBC anaongezi.
[h=2]'Uchaguzi umekumbwa na kasoro kubwa'[/h] Akizungumza kwenye makao makuu ya chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) mjini Harare, Bw Tsvangirai alisema: "Hitimisho letu ni kuwa uchaguzi huu ni kichekesho kikubwa.’
"Uhalali wa uchgauzi huu umeharibiwa na ukiukwaji wa sheria na shughuli za kiutawala ambazo zimeathiri matokeo yake.”
"Ni utani ambao hauonyeshi matakwa ya watu."
Bw Tsvangirai alizungumza muda mfupi baada ya mtandao wa waangalizi (Zimbabwe Election Support Network-ZESN) kusema kuwa uchaguzi huo ‘umekumbwa na kasoro kubwa".
Katika taarifa yake rasmi ZESN limesema wapiga kura muhimu kufikia asilimia 82 walizuiwa katika vituo vya kupigia kura maeneo ya mijini ambako ni ngome ya Bw Tsvangirai.
Katika maeneo ya vijijini am, ambako ni ngome ya Rais Mugabe ni asilimia 38, kundi hilo limeongeza.
Jumatano wanavijiji, mawakala wa MDC kwenye vituo vya kupigia kura na ZESN walisema kumekuwa na kasoro kadhaa katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Masvingo.
Walisema viongozi wa jadi na wakuu wa vijiji waliwapanga watu kwenye mistari na kuwalazimisha kutembea kuelekea vituo vya kupigia kura na kuwapa namba za kupigia kura kama vile kuwahakiki wamempigia kura nani.
Wanatuhumu kuwa kwenye maeneo haya baadhi ya watu wasomi walilazimishwa kujifanya hawajui kusoma na kuandika na wakasaidiwa kupiga kura ambazo zilikuwa ni kwa Zanu-PF.
Msemaji wa Zanu-PF Mtaalam wa Saikolojia Maziwisa alikanusha kuwa wapiga kura wengi wamezuiwa makusudi kujiandikisha.
Amekiri kuwa kulikuwa na kasoro kadhaa lakini akafafanua kuwa vyama vyote vimeathirika.
"Ni muhimu kumbuka kuwa hiyo kwa sehemu ilisababishwa na ukweli kuwa baadhi ya vifaa muhimu Waziri wa Fedha Tendai Biti, anayetoka chama cha MDC alikuwa," Bw Maziwisa aliiambia BBC.
"Ukiaangalia hali ya Zimbabwe utakuwa na hitimisho moja tu. Na hii ni juu ya zaidi ya miaka mine iliyopita tumefanya jitihada za kutosha kufanya mazingira ya Zimbabwe yawe mazuri inavyowezekana ili uchaguzi uwe huru na hali.."
BBC swahili
 
Tsvangarai alipopewa uwaziri mkuu alienda UK akawaambia wazimbabwe a.k.a wazimwi walioahamia UK kuwa they must come back home kwa sababu sasa mambo ni mazuri. Jamaa walimzomea live mpaka mkutano ukavunjika. Yaani Tsangarai yeye kupata uwaziri mkuu ndio anaona kwamba maisha sasa yamekuwa mazuri!

Hawa ndio wanasiasa wetu. Hivi sasa anaanza kulalamikia uchaguzi ili apewe kinafasi kingine cha uongozi serikalini kimvutevute kimaisha.

Hata Tanzania wapo wagombea ambao wanajifanya hawamtambui Rais ili wabembelezwe kwa kupewa power sharing deal. Lakini bahati nzuri hawakufanikiwa. Hata hivyo tujiandae kuwa huko mbele watarudia tena tabia yao ya kukataa maamuzi ya wapiga kura.

Msikilize hapa anavyozomewa kwa kauli yake ya kibinafsi Tsvangirai in london cathedral 20 june 2009 - YouTube

Hata Dr. Slaa baada ya kufahamika kuwa ni fisadi na mbinafsi mwenye uroho watu wengi wameacha kumuamini. Tsangarai watu walimuamini sana wakamuona ndio tumaini la Zimbabwe, lakini alivyoonja shavu tu kawaangusha. Matokeo yake ndio kama uchaguzi unavyoonyesha...​


"To greed, all nature is insufficient"
 
huo utafiti umefanya lini na kina nani walihusika na yako wapi matokeo ya huu utafiti.Nakumbuka nimeshawahi kukusauri usome kitabu kinaitwa logic thinking and reasoning naona bado hujasoma

Hata Dr. Slaa baada ya kufahamika kuwa ni fisadi na mbinafsi mwenye uroho watu wengi wameacha kumuamini. Tsangarai watu walimuamini sana wakamuona ndio tumaini la Zimbabwe, lakini alivyoonja shavu tu kawaangusha. Matokeo yake ndio kama uchaguzi unavyoonyesha...​
"To greed, all nature is insufficient"

 
huo utafiti umefanya lini na kina nani walihusika na yako wapi matokeo ya huu utafiti.Nakumbuka nimeshawahi kukusauri usome kitabu kinaitwa logic thinking and reasoning naona bado hujasoma.

Kujua kusoma hajui........
 
Mpaka Mugabe atakapopata cheo kipya cha HAYATI, Tvangirai hawezi kitu Urais kupata sababu kama wafanyavyo ccm hapa bongo ndo wafanyavyo ZANU PF ya Mugabe. Wizi mtupu tena wa waziwazi kibabe. Ati watatawala milele, hakuna mwingine awezaye kutawala mbali na wao kwa kadiri ya imani yao.
 
Back
Top Bottom