TBS Vs Coca Cola, Pepsi & Azam Cola

Enzymes

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
4,334
3,004
Wadau: Je afya zetu ziko salama?

Kwasa nchini Tanzania kuna makampuni mbalimbali yanayo zalisha vinywaji kama Juice, Soda, na vitafunwa kama pipi, jojo, PK, nk.

Maajabu ya Tanzania, Viwanda hivi vyote hamna hata kimoja kinacho miliki shamba la matunda wala kuhamasisha wakulima au kuwekeza ktk kilimo cha malighafi zao.

Kwa sasa radha ya Soda X ya mwaka 2000 na radha ya soda X (hiyohiyo) ya mwaka 2015 nitofauti kabisaaa!!

JK kapandisha uchumi hadi sasa tuna Juice hadi za Tshs 100!!! Maajabu kwelikweli!! Na juice hizi hutumiwa sana na watoto. Na bidhaa hizi nyingi hazina Nembo ya TBS!!

Pia kuna uingizwaji wa Juice mbalimbali wa Juice kutoka Uarabuni huku zikiwa zimeandikwa kwa kiarabu na kukosa tafsiri ya Kiingereza au Kiswahili!!

TBS, acheni kufanya kazi kwa mazoea! Jengeni maabara kila mkoa (mmekalia Dar tu utadhani Kagera, Ruvuma, Kigoma, Mara, Moshi, Mbeya si midomoni mwa bidhaa feki).

Au mnang'ang'ania kupiga madili bandarini?

Je hii ni ishara kuwa TBS mmeamua kutumaliza au?
 
Inategemea umekuja lini Mjini
Na lini umeacha kunywa Soda ya Kugawana enzi hizo tena mnaongezewa na Maji ili watoto woote mtoshe.

Halafu Hoja zako kama zinajichanganya vile,yaani umeziunga ki vurugu mechi kamanda.

Halafu inategemea pia lini umenunua Soda kwa pesa yako.Maana asikudanganye mtu Soda ya kununuliwa ni tam kweli kuliko ukitoa pesa mwenyewe.Na ukitaka kujua Soda kama Tamu uwe umefulia halafu upigwe offer.Aisee hapo hata ladha hujui unaona kama Wine vile.
Na ukitaka kujua kwamba Soda mbaya basi uwe umeshiba na una pesa,basi wala huwezi kuona ladha yoyote ya Soda.
Zaidi:Kama ulikuwa sio mnywa Bia ukaanza kunywa bia,basi soda zote utaona kama zinazingua tu na kuona tofauti kabisaa na za miaka hiyo ya 2000 unayosema.

Sasa tuambie umeandika ukiwa kwenye hali gani.

Namshukuru sana Mwalim wangu wa Secondary School kwa kutuandalia Study Tour kwenye Viwanda.Kweli nilijifunza meeengi sana.Na kama mleta mada hapo ungekuwa umefanya Study Tour ya kiwanda chochote cha vinywaji basi wala usingekuja na Swali hilo.Maana hakuna Kampuni iliyo nyepesi na wakarim kama Kampuni ya Coca Cola na wenzie ukiwaomba kufanya Study Tour,unaelekezwa kila kitu kuanzia Soda inavyochanganywa yaani hatu ya mwanzo hadi ya mwisho.Nakumbuka tuliambiwa kwamba haturuhusiwi kutoka na soda,ila tunywe kadri ya uwezo wetu.Aisee zilipangwa kreti teleeeeeee,watu full furaha,mwisho kila mmoja alichemka.Yaani acha

TBS wapo sawa,ila pia wanategemea informers,kama unaona kuna product ipo sokoni,wasaidie kwa kutoa taarifa wao watafuatilia.
Kuhusu Juices kutoka Nje,hata kama zimeandikwa kiingereza bado ni changamoto vile vile.
Kuna watu wanazipiga humuhumu na kuweka chupa kwamba zinatoka Nje.
Ila muhim ni wewe mwenye kutoa taarifa,TBS sio Malaika kwamba watajua kila kitu kinachoendelea kila sehem
 
Hizo tabia inaonesha ni zako!!
Pia acha utoto, kuku ww.
 
Hizo tabia inaonesha ni zako!!
Pia acha utoto, kuku ww.

Utamwitaje mwenzako kuku? Nadhani ametoa ushauri mzuri mwishoni ofcourse minus issue ya soda za utotoni. Narudi kwenye mada, Na wasiwasi hizi concerns zako zinatakiwa zipelekwe TFDA siyo TBS.
 
Hivi Azam Kokwa za Embe huwa anazitupa wapi? Atakaye survive Hapa ni yule wa kijijini tu wengine wote tunakula Sumu.
 
Hivi Azam Kokwa za Embe huwa anazitupa wapi? Atakaye survive Hapa ni yule wa kijijini tu wengine wote tunakula Sumu.

Kinywaji Bora ni kile unachotengeza nyumbani mwenyewe ambacho hakikai ndani zaidi ya siku mbili au tatu.
Vilivyosalia lazima viwekwe Chemical inavyoweza kufanya visiharibike kwa muda mrefu,na ni wastan wa mwaka mzima.
Sasa hapo unapata picha kwamba ukiwa unakunywa unakunywa na nini.Ndio maana inashauri saaana watu kupata Glass ya maziwa angalia moja kwa siku mbili ili ku neutralize mabaki hayo.

Na ukitaka kujua Umekaribioshwa vizuri kwenye nyumba ya mtu,basi ni kwa yule mwenyeji anaekukaribisha kwa Juice ya Matunda alietengeneza mwenyewe.Ila sio kwamba vinywaji hivyo sio vibaya kutumia ila ujue pia unakunywa nini na upange lishe yako ili uwe kuwa unapunguza makali ya mabakia ya hizo Chemical

Kuna nchi moja ya Scandinavia Redbull imepigwa marufuku kabisaaaa,kwakuwa na athari kwenye moyo.Ila hapa tunapeta tu.Sasa muhim ni kujitambua
 
Hivi Azam Kokwa za Embe huwa anazitupa wapi? Atakaye survive Hapa ni yule wa kijijini tu wengine wote tunakula Sumu.

Mimi kwa hili ntasavaivu kaka, sinywi soda wala juice yoyote ila, huu mwaka wa 4. Mimi nakunywa maji tu kiongozi, kinywaji kinachoingia kinywani mwangu ni maji tu pamoja na juice ya kutengeneza nqenyewe home. Labda na zile juice zetu(mate) toka kwa vidosho.
 
Kwa kweli inatia huruma wtz lazima tubadilike. Zipo product za uga zenye ladha ya matunda mbalimbali wanatengezea juisi gm 5 kwa lita 2 za maji. Naona huruma wanafunzi wa shule wanavyozigombea.
 
Back
Top Bottom