TBS kusimamia masuala ya Chakula na Vipodozi

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
713
1,000
Serikali ya Tanzania imependekeza marekebisho ya sheria ya viwango sura 130 ili kuhamisha majukumu ya kusimamia masuala ya chakula na vipodozi kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo inasimamia majukumu hayo kwa sasa.

Kutokana na kubadilishwa kwa majukumu hayo, imependekezwa kuwa badala ya kuitwa TFDA, iitwe Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Kufuatia pendekezo hili, TBS itachukua jukumu la kuunganisha utaratibu wa usajili wa majengo, bidhaa, udhibiti wa bidhaa na udhibiti wa bidhaa kutoka nje.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Juni 26, 2019 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati akiwasilisha bungeni muswada wa sheria ya fedha mwaka 2019.

“Inapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi sura ya 219 ili kuiondolea TFDA jukumu la kusimamia chakula na vipodozi.”
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
5,567
2,000

Wale wale walio pitisha kuanzishwa kwa tfda kwa mbwembwe na ndiyooo ndio hao hao watakao pitisha tena hayo marekebisho na kusifu na kuabudu. Sijui hawaangalii hansard za vituko vyao au vipi..
 
Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
1,127
2,000
Kwa hyo wale wafanyakaz wa tfda waliokuwa wanadeal na chakula tu watahamishiwa tbs bila Shaka
 
obseva

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
535
1,000
Ningefurahi sana kama ningepata sababu kwanini majukumu haya yamehamia TBS, naona kama TBS ni dudu kubwa sana na linaongezewa majukumu ambayo ni muhimu sana kwa afya za walaji. Naona kame mbele tunaliita giza.
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,638
2,000
Ningefurahi sana kama ningepata sababu kwanini majukumu haya yamehamia TBS, naona kama TBS ni dudu kubwa sana na linaongezewa majukumu ambayo ni muhimu sana kwa afya za walaji. Naona kame mbele tunaliita giza.
Tuliwahi kusema hapo kabla, kuwa kwa sababu ya tamaa ya kukusanya tozo mbalimbali, TFDA iliingilia majukumu ya TBS na kusababisha mkanganyiko ktk kutoa huduma. TFDA badala ya kujikita katika majukumu yao ya USALAMA (Security) wa Chakula na Madawa, (kuzuia madhara kwa jamii) wakaingilia kuhakiki VIWANGO (Standard) kazi inayotakiwa kufanywa kisheria na TBS. Wakaanzisha na maabara zao kubwa kabisa kushindana na TBS na kusababisha mgongano. TFDA walitakiwa kujikita ktk kulinda usalama wa afya za jamii, viambata sumu, muda wa matumizi wa bidhaa za vyakula na dawa. Viwango vya kitaifa na kimataifa vinavyotakiwa ktk kutengenezaji bidhaa ni kazi ya TBS. Kwa sheria hii kila mtu anarudishwa kwenye jukumu lake.
 
obseva

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
535
1,000
Tuliwahi kusema hapo kabla, kuwa kwa sababu ya tamaa ya kukusanya toxo mbalimbali, TFDA iliingilia majukumu ya TBS na kusababisha mkanganyiko ktkmkuto huduma. TFDA badala ya kujikita katika majukumu yao ya USALAMA (Security) wa Chakula na Madawa, (kuzuia madhara kwa jamii) wakaingilia kuhakiki VIWANGO (Standard) kazi inayotakiwa kufanywa kisheria na TBS. Wakaanzisha na maabara zao kubwa kabisa kushindana na TBS na kusababisha mgongano. TFDA walitakiwa kujikita ktk kulinda usalama wa afya za jamii, viambata sumu, muda wa matumizi wa bidhaa za vyakula na dawa. Viwango vya kitaifa na kimataifa vinavyotakiwa ktk kutengenezaji bidhaa ni kazi ya TBS.
kwa mtzamo huo unazani TBS wataweza kulinda afya ya mlaji zaidi ya TFDA?
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
1,791
2,000
Mipango ya hovyo hovyo juzijuzi tfda wameajiri zaidi ya wataalamu zaidi ya 10 Kama ma food inspector kupitia sekretarieti ya ajira
 
chamakh

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
725
500
Tuliwahi kusema hapo kabla, kuwa kwa sababu ya tamaa ya kukusanya tozo mbalimbali, TFDA iliingilia majukumu ya TBS na kusababisha mkanganyiko ktk kutoa huduma. TFDA badala ya kujikita katika majukumu yao ya USALAMA (Security) wa Chakula na Madawa, (kuzuia madhara kwa jamii) wakaingilia kuhakiki VIWANGO (Standard) kazi inayotakiwa kufanywa kisheria na TBS. Wakaanzisha na maabara zao kubwa kabisa kushindana na TBS na kusababisha mgongano. TFDA walitakiwa kujikita ktk kulinda usalama wa afya za jamii, viambata sumu, muda wa matumizi wa bidhaa za vyakula na dawa. Viwango vya kitaifa na kimataifa vinavyotakiwa ktk kutengenezaji bidhaa ni kazi ya TBS. Kwa sheria hii kila mtu anarudishwa kwenye jukumu lake.
Ndugu umejaribu kuandika lakini umeandika bila ya kuelewa.
Kifupi Serikali imeshauriwa vibaya na imesikiliza Wafanyabiashara badala ya kulinda Wananchi. TBS is a failed Organization maana hata wakurugenzi wake wamebadilishwa Mara kadhaa na JPM. Sasa kuhamishia bidhaa za Chakula na Vipodozi kwenye Taasisi yenye mifumo dhaifu ni kuweka rehani Afya za Watanzania.
Mbaya zaidi ili kuondosha muingiliano baina ya Taasisi mbali mbali Serikali ilileta Blue print. Mapendekezo ya Blue print ilikuwa kuinyanganya TBS masuala mengi inayoingiliana na TFDA na kuyapeleka TFDA. Hata hivyo Serikali hiyo hiyo imeikiuka Blue print na kuja na kitu tofauti. Ni suala la muda tuu kabla masoko yetu hayajawa flooded na substandard and fake products. Nakupa miezi Sita tuu pita masokoni uje useme
 
Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,643
2,000
Serikali ya Tanzania imependekeza marekebisho ya sheria ya viwango sura 130 ili kuhamisha majukumu ya kusimamia masuala ya chakula na vipodozi kwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo inasimamia majukumu hayo kwa sasa.

Kutokana na kubadilishwa kwa majukumu hayo, imependekezwa kuwa badala ya kuitwa TFDA, iitwe Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Kufuatia pendekezo hili, TBS itachukua jukumu la kuunganisha utaratibu wa usajili wa majengo, bidhaa, udhibiti wa bidhaa na udhibiti wa bidhaa kutoka nje.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Juni 26, 2019 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji wakati akiwasilisha bungeni muswada wa sheria ya fedha mwaka 2019.

“Inapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi sura ya 219 ili kuiondolea TFDA jukumu la kusimamia chakula na vipodozi.”
Maamuzi ya kimiemuko. Nchi nyingi masuala ya chakula yanasimamiwa na taasisi moja kama iluvyo sasa TFDA. TBS wanapewa na wanafanya majukumu yasiyowahusu. TBS wamekuwa wafanya biashara badala ya kuweka viwango vya nchi! Wabakazana na enforcement hata kwa vitu ambavyo hawajaweka viwango vya taifa!
 
Ze Heby

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,512
2,000
Walikua wanafanya vizuri pia kwenye chakula,vipodozi na vifaa tiba

Yani ukishakua stringent huwezi baki salama.
tfdatanzania-20190627-0001.jpeg
 
Apr 28, 2019
9
45
Jambo hili linaweza kupelekea kuongezeka kwa mzigo kwa wafanyabiashara. Yawezekana mfanyabiashara wa kawaida anayeuza duka la kawaida lenye mchanganyiko wa vipodozi na vitu vya kawaida akatakiwa kuwa na vibali vya TBS pamoja na TMDA
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom