TBS chunguzeni ubora wa majani ya chai ya kiwanda cha AFRI TEA AND COFFEE BLENDERS LIMITED.

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,669
22,256
Majani ya chai ya kiwanda nilichokitaja yenye nembo ya GREEN LABEL TEA na kuthibitishwa na TBS kwa TZS 728 ubora wake unamashaka. Pamoja na mashaka hayo sijui kama kiwanda hiki ndicho kile cha Tanzania Tea Blenders Limited kwani kifungashio chake ni kile cha kiwanda cha TTBL. Wengi wetu huwa hatujui kuwa majani ya chai yasiyo na ubora ni hatari kwa afya.
 
Unatumika vibaya,,majani ya chain ya kiwanda hicho na kahawa yake ni bora kabisa
Nimezungumzia majani ya chai, kahawa haihusiki pia ni jukumu la TBS kukagua ubora wa bidhaa zilizoko madukani ambazo wao walikwisha zipitisha. TBS hupelekewa sampo na mtengenezaji anapoanza kuzalisha na kinachofuatia ambacho huenda TBS hawakifanyi ni kuchukua bidhaa madukani na kuzipima tena ili kuona kama ubora bado unazingatiwa. Majani ya chain ni zao linalohitaji uangalifu sana kuanzia uchumaji yaani muda, upelekaji kiwandani na usindikaji inamaana yachumwe alfajiri mpaka yakiwa na umande na ni majani mawili na nusu ya juu ya tawi yapelekwe haraka kiwandani kabla hayajanyauka na yasindikwe haraka ili kupata ubora unaotakiwa. Endapo utachuma nani la tatu lililokomaa na mengine yanayofuatia hiyo chain haitakuwa na ubora, vivyohivyo endapo yatachumwa wakati jua limepanda hayatakuwa na ubora pia. Ninakumbuka miaka kadhaa iliyopita TTBL ilikuwa na majani ya chai hatari ambavyo yalitengenezwa kwa majani yaliyokomaa na ilikuwa ndani ya pakiti unakuta nyuzinyuzi kama nywele za majani yaliyokomaa.
Wataalmu wa chai wasema majani yasiyokuwa na ubora ni sumu.
 
Majani ya chai ya kiwanda nilichokitaja yenye nembo ya GREEN LABEL TEA na kuthibitishwa na TBS kwa TZS 728 ubora wake unamashaka. Pamoja na mashaka hayo sijui kama kiwanda hiki ndicho kile cha Tanzania Tea Blenders Limited kwani kifungashio chake ni kile cha kiwanda cha TTBL. Wengi wetu huwa hatujui kuwa majani ya chai yasiyo na ubora ni hatari kwa afya.
Pia TBS wachunguze kiwanda cha Rangi coral paints ,Rangi zimeoza na zinatoa harufu haifai hazifai kwa matumizi ya ujenzi
 
Back
Top Bottom