TBC1 Wanatumia teknolojia gani?

TBC1 Wanatumia teknolojia gani?

Towned

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2018
Posts
226
Reaction score
300
Hakika TBC1 kama chombo cha Taifa kinasikitisha sana. Leo imebidi niongee maana sijui kuna shida gani.

Leo nilikuwa mimi na mdogo wangu tunaangalia mechi kati ya Valencia vs Sevila. Baada ya game hiyo nikaweka habari TBC1, dogo akaniuliza bro hawa TBC mbona hawaoneshi anachoongea mtangazaji. Sikumyelewa, nikamuuliza kivipi? Akasema wewe angalia mdomo wa mtangazaji na sauti mbona sio sahihi.

Nikamuelewa maana picha na sauti vinatofautiana mno. Yani picha inatangulia then ndio sauti inafuata yani vinatofautiana mno. Nilimwambia hayo ni maswala ya teknolojia. Dogo ana miaka 9.

Kimsingi hili swala lilinifedhehesha sana. Hivi hadi lini tutaendelea kuwa na chombo cha taifa cha namna hii? Hivi hadi lini tutakosa cha kujivunia hata mbele ya jirani zetu hasa pale utani wa nchi na nchi unapojitokeza?

Mh. Rais naomba inusuru TBC. Umetoa mil 400 (kila kituo) za ujenzi wa vituo vya afya nchi nzima, umetoa mil 500 (kila wilaya) za ujenzi wa Hospitali za wilaya, pia mara kadhaa umetoa fedha za utekelezaji wa miradi mikubwa najua hili lipo ndani ya uwezo wako. Iokoe TBC. Naomba wape hela walau nao wapate vifaa vya kisasa.

Nilijua Ryoba ataleta mabadiliko lakini wapi.

Huko ni kwenye muonekano na sauti pekee. Bado hujakutana na watangazaji wenye siha na wajihi wa ajabu. Yani mtu yuko studio anatangaza taarifa ya habari lakini hayupo smart kabisa. Unajua usmart na mvuto ni kivutio pia kwa watazamaji. Najua TBC hapo kuna watu smart wawekeni kwenye utangazaji waungane na Elizabeth Mramba na Sam Mahela. Pia undeni couple za kueleweka. Kina Mwasyoke, Zakaria, Ganzel, Bwigane wabaki huko kwenye redio.

Na kama hamna basi chukueni kutoka vituo vingine waje kuiinua TBC yetu
 
Sijaelewa unamuomba Mh. Rais atoe pesa ili kuboresha muonekano(usmart) wa watangazaji, ubora wa wa vifaa au what exactly was your point there?
 
Wao wanasema wameanza kufunga vifaa vya kisasa zaidi kuanzia jana
 
Kilichonishangaza ni kwamba dogo mwenye miaka 9 ameona kasoro wakati huo jamaa mmoja na lundo lake la miaka hajaona kasoro yoyote.
Natania tu Mkuu.
 
Hakika TBC1 kama chombo cha Taifa kinasikitisha sana. Leo imebidi niongee maana sijui kuna shida gani.

Leo nilikuwa mimi na mdogo wangu tunaangalia mechi kati ya Valencia vs Sevila. Baada ya game hiyo nikaweka habari TBC1, dogo akaniuliza bro hawa TBC mbona hawaoneshi anachoongea mtangazaji. Sikumyelewa, nikamuuliza kivipi? Akasema wewe angalia mdomo wa mtangazaji na sauti mbona sio sahihi.

Nikamuelewa maana picha na sauti vinatofautiana mno. Yani picha inatangulia then ndio sauti inafuata yani vinatofautiana mno. Nilimwambia hayo ni maswala ya teknolojia. Dogo ana miaka 9.

Kimsingi hili swala lilinifedhehesha sana. Hivi hadi lini tutaendelea kuwa na chombo cha taifa cha namna hii? Hivi hadi lini tutakosa cha kujivunia hata mbele ya jirani zetu hasa pale utani wa nchi na nchi unapojitokeza?

Mh. Rais naomba inusuru TBC. Umetoa mil 400 (kila kituo) za ujenzi wa vituo vya afya nchi nzima, umetoa mil 500 (kila wilaya) za ujenzi wa Hospitali za wilaya, pia mara kadhaa umetoa fedha za utekelezaji wa miradi mikubwa najua hili lipo ndani ya uwezo wako. Iokoe TBC. Naomba wape hela walau nao wapate vifaa vya kisasa.

Nilijua Ryoba ataleta mabadiliko lakini wapi.

Huko ni kwenye muonekano na sauti pekee. Bado hujakutana na watangazaji wenye siha na wajihi wa ajabu. Yani mtu yuko studio anatangaza taarifa ya habari lakini hayupo smart kabisa. Unajua usmart na mvuto ni kivutio pia kwa watazamaji. Najua TBC hapo kuna watu smart wawekeni kwenye utangazaji waungane na Elizabeth Mramba na Sam Mahela. Pia undeni couple za kueleweka. Kina Mwasyoke, Zakaria, Ganzel, Bwigane wabaki huko kwenye redio.

Na kama hamna basi chukueni kutoka vituo vingine waje kuiinua TBC yetu
Hapo inaonyesha jinsi gani ulivyo kiazi yaan dogo wa 9yrs ameona kasoro ila wewe kubwa jinga hujaona kasoro yoyote zaidi ya kuunga mkono juhudi za muheshimiwa
 
Wamezifunga zile chanel zingine utafikili walikuwa wanatulipia vifurushi wako kumbe yanatuingiza kwenye utawala wa kidikteta
 
Wengi wao wanasema Negative kama wewe, TBC ni shirika la Uma hata wewe unaweza kufanya reasach nini na nini kinatakiwa ukafahamu na ukaipeleka, na ikatokea Reseach yako haija fatwa njoo ulalamike kwa hoja. Reseach sio mpaka uende wapi hata kwenye Simu uliyo tumia hapa unaweza kufanyia Reseach.

Tunaitaji mabadiliko na haya ndio mabadiliko ya kweli kama Taifa. Be POSITIVE
 
Si walisema wamefunga mitambo mipya ambayo kwa africa wao ndo wanayo.. Au ilikua ni mitambo feki
 
images (1).png

Labda warudi huku ndo ntavutiwa nayo
 
Hata picha zao mbaya sijawahi kuona. Ziko faint sana.....
 
Back
Top Bottom