TBC1 wana matatizo gani leo?

TBC1 wana matatizo gani leo?

Hii nchi tunaongozwa na Matope, tena matope yenyewe ni yale ya kutoka chooni. Huwezi amini wakati watanzania wote wameamka na shauku ya kuona hatma ya ripoti ya Escrow bungeni leo. Bunge lilipoanza leo, Televisheni ya Taifa TBC ilikuwa inarusha kipindi wanaongea na wachekeshaji wa Bongo Movie JB pamoja na Mzee Majuto.

Hivi kweli kwa upuuzi huu tutaendelea kuwavumia viongozi hawa mpaka lini?
 
hata wakifa mkuu wa kaya huwa anaeendaga kushinda msibani hata siku tatu mfululizo.sisemi kuwa hayo nayo nimatope ya kutoka choonijapo yanaweza kufananishwa nayo.
 
Mnaotazama TBC mjiandae kisaikolojia pia. Mjadala ukifika kwenye chorus watakata matangazo wakisingizia hali mbaya ya hewa, au kukatika kwa umeme kule Kijitonyama! Shauri yenu.

waashachukua umeme dah!
 
Watacheza na akil zetu hadi lin.mana wanajua tungeangalizia picha kwenye runinga na sauti tungepata kwenye vituo vya radio kwa hlo bado hamjatukomoa
 
Wadau Mimi natumia Dstv na tangia asubuhi TBC 1 haina Saudi
Sasa sielewi ni hujuma nisisikie Escrow au la?
television ya taifa imekuwa na mafua sana.. wakati mwingine hata watangazaji wanashindwa kuwasiliana vema na watu Wa Picha za matukio.. sijui ndiyo Yale mambo ya kitu chochote cha serikali kisiposimamiwa kinakuwa ovyo ovyo tu.. shirika la utangazaji mnatukera sana.. TBC inapitwa hata na TV1!
 
Hati za kusafiria za washukiwa zikamatwe
baada ya mjadala watuhumiwa wawekwe sehem maalum kwa uchunguzi
 
Tundu lisu amaemlipua wakili wa PAP aliepeleka hoja ya kuzuia mjadala kujadiliwa kwamba ni kada wa CCM, anatoka mpanda na aliwahi kuua mke wake na kesi ikamalizwa juu juu, hii ni baada ya mbunge wa CCM kusema wakili wa PAP ni kada wa chadema, bunge limelipuka kwa vigelegele na makofi. Kuna watu wachafu na wanaendelea kutumika. Na bunge limeahirishwa mpaka saa 11 jioni kwa hiyo tuendelee kusubiri. Wabunge wa vyama vyote wamekubaliana ripoti ijadiliwe.
 
mlokuwa mbali na tv mnaweza fatilia mjadala huu kupitia capital fm 101.3
 
Back
Top Bottom