Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Katika taarifa ya habari ya SAA Saba mchana, habari iliyohusu bungeni ilikuwa ilikuwa habari ya swali lililoulizwa na Mhe. Freeman Mbowe (KUB) kuhusu wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuingilia shughuli za halmashauri na maamuzi ya Baraza la Madiwani, kwamba kwanini serikali kuu isitoe tamko kuwakataza wakuu wa mikoa/wilaya kufanya hivyo.
TBC mmeona ni tabu sana kulionesha swali lilipokuwa likiulizwa na Mhe. Mbowe, badala yake mmeifanya habari hiyo kama vile ni maelekezo ya serikali ilhali ni jibu la serikali kuhusu swali la msingi kutoka kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni.
Huu upendeleo wa kisiasa mnaoufanya unazidi kuchochea chuki baina ya serikali na wananchi, kwani kodi za wananchi hazitumiki kwa usahihi, badala yake zinatumika kukinufaisha Chama cha Mapinduzi CCM.
Kifuatacho ni kampeni kuwa watu waache kukitazama chombo hicho cha habari.