GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Nadhani sasa ni wakati muafaka wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuamua moja ama kubaki hapo TBC na kuendelea kujidhalilisha kama Mwana taaluma mbobezi wa Masuala ya Habari nchini Tanzania au aachane tu na hicho Cheo ili arudi kuendelea Kukufunzi, Kuandika, Kufanya tafiti na Kutoa ushauri wa Kitaalam.
Leo tena asubuhi nimemsikia mwenyewe tena mubashara kabisa Mkemia akipiga simu katika Mawingu na kuwapongeza tena kama kawaida yake kwa kazi nzuri wanayoifanya na nikajiuliza hivi ni kitu gani ambacho Mkemia amevutiwa nacho mno na Mawingu na ambacho hakipo TBC?
Ewe Mkurugenzi Mkuu wa TBC unaonaje labda ukimfuata Mkemia huko huko alipo sasa mapumzikoni ili umuulize anataka TBC iweje ili pengine mkifanyie Kazi ili asiwe anavutiwa na Mawingu na sasa awe anavutiwa nanyi TBC.
Binafsi nilijua kuwa Mkemia siku zote atakuwa namba wani fani wa TBC lakini kumbe wapi Mkemia ni nambari wani fani tena wa kindakindaki kabisa wa Mawingu kitu ambacho naona kama ni ajabu hasa ukizingatia Kiueledi na Kimfumo wa Kiserikali Mkemia ndiyo Mhariri Mkuu wa Vyomba vyote vya Habari vilivyo chini ya Serikali TBC ikiwemo.
Dkt. Ayub Ryoba jitathmini na TBC yako ila kama ni kukushauri tu basi nadhani ile Kalamu yako ya jicho la tatu na ule utaalam wako wa Kihabari tunauhitaji mno huku mitaani kuliko Wewe kuendelea kuwepo hapo TBC na kwa jicho la Kitaaluma kitendo cha Mkemia kila siku au kila mara kupiga tu Simu na kuwa pamoja na Mawingu huku akiwapongeza tena mubashara ni kama vile anakudhalilisha au anakuchora tu Wewe pamoja na Usomi wako wote huo mkubwa ambao hata Matajiri na Mabosi wote wa Mawingu wajikusanye na wajae ukumbi mzima wa Escape One hadi Two bado tu hawawezi kukufikia.
Nawasilisha.