Mimi hili linanikera sana hasa pale TBC inapokuwa domo la CCM, na pale ninapokumbuka kuwa mkurugenzi wake ni moja ya waandishi aliyepata great exposure na kuvifunza jinsi vyombo vya umma katika nchi za wenzetu zinavyothamini umma, lakini bado kwa njaa yake au sijui analipa fadhila yeye ndio yuko mbele kuratibu propaganda za CCM kupitia TBC bila kujali kuwa wananchi ndio wanoiendesha na sio kila Mtz ni CCM! hawa Clouds tokeas walivyofanikiwa kudhulumu Joseph Mbilinyi haki yake, wakijifanya eti wanapiga kampeni ya kitaifa juu ya malaria na JK kuwa nao pamoja siku ile ya onesho basi ndio wameona ni loop hole ya wao kuwa karibu na muungwana, sasa wanapiga kampeni za wazi kabisa, na mbaya zaidi kwa kuwa hawana hata shule basi radio yenyewe imekuwa kama "kijiwe" flani hivi cha umbeya!