Ufwandunkanye
Senior Member
- Jan 7, 2017
- 123
- 193
Ukitazama TV ya Taifa, TBC, basi unaweza kuikinai muda mfupi. Kwani imegeuka kuwa chombo cha propaganda za kisiasa. Imegeuka kuwa filimbi ya Rais Magufuli na CCM. Yaani imemgeuza Rais Magufuli kama muumbaji wa nchi yetu, kwamba bila yeye hakuna maendeleo kama kwamba huko nyuma hakukuwa na marais wengine.
Kila jambo likifanywa zuri, utawasikia watangazaji kuwa asifiwe Rais Magufuli, yaani hata kama jambo halimuhusu. Hata kwenye kipindi ambacho jina la Rais Magufuli halistahili kutajwa, basi watalitaja. Huku nikujawa kwa nidhamu ya woga na unafiki, yaani wafia tumbo.
Katika awamu zilizopita hatukuwahi kuona unafiki huu wa hiki chombo, kwani kilitoa habari kwa kujiamini na bila kupendelea. Haiwezekani zitawale habari za Rais Magufuli na CCM tu, kwamba wengine hawapo ilihali inatumia kodi zetu. Tunakoelekea watapendekeza TBC iitwe Magufuli TV au CCM wataichukua kabisa na kuwa yao kama walivyopora mali za umma na taasisi za dini.