Nachoshanaga ni kuwa kuna template nzuri za joomla zinazozofaa mashirika ya utangazaji. zipo za bure na ipo nzuri zaidi za kununua kwa $50.
Sasa wewe anagalia eti TBC haina clip au archive za video au Audio hata moja ya hotuba si ya JRais wala wa kiongozi yeyote. Haina clip ya video ya latest news. Sasa tovuti ya TBC inatofautihswa vipi na Tovuti ya Dailynews. Yaaani maudhui ya TBC ni nini?
YAaani hata huo mpangilio wa Tovuti ulivyo mhhh . Then ukite una mtu anakula milioni kadhaa kila mwezi kuwa yeye ndio webmaster wa hii tovuti..
Tatizo la mashirika yetu ya umma ni kwamba hawabadiliki na kwenda na wakati, kazi kugombania vyeo tu hata kama uwezo hawana, si hilo tu hawataki kabisa kuajili watu weledi wanasahau kwamba mambo ya sayansi ni facts and figures siyo siasa wala ngojela ukiyapuuzia yatakuja kuku-haut - unayoshuhudia sasa hivi ni matokeo ya kupuuzia ukweli kwamba mambo haya ya modern technology yanaitaji watu weledi mkubwa na siyo wababaishaji au kusubiri wachina ndio waje kuwasaidia as if hakuna watanzania wenye huwezo wa kuzifanya hizi kazi.
Wakati mwingine wanashindwahata kurekebisha kitu kinacho julikana kama "Lip Synch" ukisikiliza sauti na kulinganisha na mdomo wa mtangazaji unaona havilandani kabisa, je naiyo inaitaji mchina kuirekebisha! Serikali yetu isipokuwa makini kwa recruit watu wenye ujuzi wa kweli na ubunifu kwa kutafuta consultant wa kuwafanyisha usahili wataalamu bila kuleta mambo ya kujuana/urafiki/undugu, shirika hilo la TBC na mashirika mengine ya umma yataishia kuchukuwa ruzuku chungu mzima kutoka Serikalini kuziendesha vile vile wakurugenzi wa Board nao wanachangia sana katika ukosefu wa ufanisi katika mashirika yetu ya umma wanasoma board papers siku moja kabla ya mkutano ni wachache sana wako makini kuona mashirika yetu yanaendeshwa kiufanisi. Kuzolota kwa mashirika haya kunatokana vile vile na kubweteka kwa management ambayo haina incentive ya kuchakalika au kuwa wabunifu maana wanajuwa wawe wabunifu wasiwe wabunifu mshahara huko pale pale - kwa nini wangaishe vichwa vyao - na hiki ndicho kimemaliza mashirika yetu ya umma, ukienda kwenye kampuni za watu binafsi mambo ni tofauti kabisa kule huwezi kuleta mambo ya umangimeza ukavumiliwa hawana mchezo kabisa wanabadirisha wafanya kazi kama bolts in a machine.
Nimeona humu members wanazungumzia tivoti ya TBC mimi sishangai chochote, ukienda kuhulizia hapo si hajabu ukahambiwa yuko Mkurugenzi wa ICT yaani kuna kitengo kamili kinacho shugulikia mambo hayo ya ICT kama ndiyo hivyo ni kitu gani kinawashinda kudesign, ku-host na ku-update TIVOTI yao kwani si wataalamu wanao? kama wapo kazi zao ni nini hasa! jaribu kuhuliza huyo aliye design website yao alilipwa kiasi gani utashangaa. Si hajabu hata hiyo TIVOTI hiko hosted kwenye makampuni mengine wakati wenyewe wana uwezo wa kufanikisha hilo, wahulize hizo kampuni zinalipwa kiasi gani kwa mwezi/mwaka ku-host TIVOTI yao, kama wanashindwa kulifanya hilo kwa nini wasiombe msaada kutoka kwa vijana wa humu kwenye jamii forum wakawasaidia ku-redesign TIVOTI ya TBC na kuwapa tricks za kudesign site inayolingana na hadhi ya TBC bila malipo. Tatizo hili la kutojali haliko cofined kwa TBC tu karibuni mashirika mengi ya UMMA yana udhaifu huu hawajali tax payers' money.
Badilikeni jamani haya mambo ya kudhani miaka yote itakuwa business as usual hayatatufikisha mbali, tutabakia kulalama sijuhi Serikali haitohi fedha za kutosha kununulia hiki na kile, visingizio chungu mzima. Mwisho mnaweza kunieleza watu wa AGAPE (ATN) wametumia kiasi gani cha fedha kufanikisha mitandao ya "CUTTING AGE TECHNOLOGY" karibu TANZANIA nzima ki-mahili kweli kweli na ni watu wachache tu dedicated na kwao every PENNY COUNTS they didn't robe a bank kufanikisha hilo, je na sisi tuna spirit hiyo kweli?
Hapa nazungumza kama mzalendo wa kweli siwalengi watu fulani, lakini hatuwezi kunyamazia mambo yanayo dhalilisha Serikali na Nchi yetu, tukiona mambo yanaenda mzobe mzobe tutasema TU, Mungu ibariki URT.