TBC taifa kwakweli inakera kuhusu vipindi vya bunge

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Hivi hii TBC taifa inayoendeshwa na kodi zetu mbona huwa inatangaza tu kipindi cha maswali na majibu bungeni na baada ya maswali kwisha wanakatisha matangazo na kutupigia miziki. Hii radio ina tofauti gani na TBC 1 ambayo hurusha matangazo yote ya vipindi vya bunge?

Huku ni kutotutendea haki na ina maana shughuli za bunge sio muhimu kwa watanzania kuzifuatilia kupitia radio yao na badala yake wanatunyima haki hiyo.

TBC badilikine maana huu ni utaratibu wa kila siku.Hivi bunge na muziki kipi muhimu?
Mambo ya siasa,uchumi,elimu na kijamii ni huko bungeni.
 
Back
Top Bottom