TBC na UKWELI NA UHAKIKA> | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC na UKWELI NA UHAKIKA>

Discussion in 'Sports' started by Jacobus, Jan 27, 2012.

 1. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,580
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nilitarajia kuwa waziri wa utamaduni............. Angejikita katika kuhakikisha vyombo vyetu vya habari (television, radio, magazeti nk.) vinathamini utamaduni wetu hasa katika kutuhabarisha habari za michezo.
  Nilitarajia waziri angesambaza waraka kuwaeleza kuwa umuhimu uwe kama zamani kwa
  1. Habari za nyumbani (nchi nzima na sio mzizima "dar"pekee),
  2. Habari za africa na mwisho,
  3. Habari za mataifa mbalimbali (hapa nasisitiza mabara yote na sio ulaya pekee hasa uingereza maana hapo huwa wanachukua muda mrefu mno kutueleza hata mambo ya kipuuzi.
  Sasa leo nimesikiliza taarifa ya habari ya saa saba mchana ya tbc1, mdada kamalizia kwa habari za michezo kwa kifupi tu kuhusu mechi ya barcelona na real madrid kwenye kombe la mfalme. Aliniacha hoi bin taaban aliposema (bila kusita) magoli ya real madrid yalifungwa na c. Ronardo na puyol.
  Simlaumu dada huyo kwa makosa hayo kwani yeye ni msomaji tu, ila hata hivo kama ingekuwa ni wachezaji wa timu za england sidhani kama angeiburuza tuu habari ile.
  Hapa ndio natilia mashaka kwa msemo wao wa "ukweli na uhakika".
  Tumetoa mwito mara nyingi kwa hasa tbc (tv na radio) kupunguza huu uingereza ambao unapandikizwa sasa kwa watoto wetu.
  Naiomba wizara ilione hilo hii ni sumu kwa utamaduni wetu.
   
Loading...