TBC mnawabeba CCM lakini hawabebeki

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,231
Taarifa ya habari ya 20hrs naona TBC walikuwa wakionesha ufunguzi wa kampeni kwa CCM nashangaa wakawa wanonesha watu kwa mimbari ie Mkapa na Kafumu wakihubiri bila kutuonesha watu mara wakachomekea umati wa watu ghafla alafu wakaendelea na speech.

Mbaya zaidi watu waliokuwa wakijibu wakati mkapa na Kmfumu wanahutubia zilikuwa sauti hafifu kabisaaaa ambayo ilikuwa tofauti na nyomi feki walioichomekea.

Naona turn up ya watu itakuwa ilikuwa ndogo am sure.
 
Chadema ilikuwa na watu kama mara 5 ya wale wa ccm.Halafu jamaa yangu kaniambia hao wa ccm wamebebwa na mafuso 7 toka wilaya mbalimbali
 
Acheni kujifurahisha nyie cdm umati jumatatu asubui mbumge wetu kafumu atapokelewa kwa kishindo jijini dar
 
Siku zinavyosonga mbele ufanisi na utendaji wa hili shirika la umma unazidi kuzorota..vifaa vya kichina wanavyotumia kurushia matangazo ni vibovu kupindukia,kila siku ktk taarifa ya habari lazma vigome..TBC inakufa!
 
Tunaposema kuwa tbc1 haiwakilishi watanzania bali ipo kwa maslahi ya CCM, leo imezidi wamezidi kujipambanua.
Mtangazaji alitangaza habari ya kampeni za CCM za kuhitimisha,ikaonekana picha hazikuwa tayari akatangaza habari ya wazee kuhusu mambo ya malipo ya pension.

PICHA ZILIZOONYESHWA NI ZA KAMPENI ZA CCM HUKO IGUNGA cha ajabu zaidi ni kuachwa hzo picha kwa muda mrefu bila kukatizwa. Mtangazaji na watu wake walipojiridhisha kuwa wa2 wameshaipata CCM ndo wakazitoa hizo picha na kutoomba msamaha.

SI WAITE CCM TV badala ya tbc
 
Hizi zilikuwa ni shangwe au kelele za wana CHADEMA baada ya chopa ya wapinzani ikipaa kwenye viwanja vyao hakika kulikuwa na umati wa kufa mtu maana nyomi ile ilikuwa ni noma.

Magamba na kafumu wametia aibu umati haukuwepo kamera zimewaonesha wao tu, TBC wamejitahidi kuchakachua lkn wameshindwa wameonesha sijui umati wapi ule mpaka aibu jamani.
 
Yaani jamaa aliendaa ile news kajitahidi sana kuficha picha ya watu waliojaa ila sauti ndo zimemuangusha maana Ben akaisema CCM oyee watu wanaoitikia ni wachache naona angeweza amplify izo sauti CCM wangeula sana kwa news ila technologia imewavuta shati ali kadharika kesho kura zaweza waponyoka.

All the best wana Igunga kuiinua au kuiangamiza Igunga kazi ni kwenu
 
Chadema ilikuwa na watu kama mara 5 ya wale wa ccm.Halafu jamaa yangu kaniambia hao wa ccm wamebebwa na mafuso 7 toka wilaya mbalimbali

Saa 12 kasoro hivi Wa Jikoni alinipigia simu na haya ni maneno yake (nanukuu):

"Nkwingwa sina salio tu, lakini ukweli nkwingwa hapa niko kwenye mkutano wa Chadema. Kuna umati mkubwa sana, yaani watu ni wengi kama mamilioni....sijui nisemeje".

Mwisho wa kunukuu.

Nikamwambia akate simu nimrukie hewani.

Ukweli usio na chembe ya unafiki wala ushabiki:

CCM na CUF hawakuwa na watu leo. Watu wote walikuwa kwenye mkutano wa Chadema. Wa Jikoni alikuwa anafika mahala anashindwa kuzungumza ananiachia nisikilize mwenyewe.

Ilikuwa ni shamrashamra za ushindi mkubwa zikiambatana na sauti ya ukombozi, "Peoples Power".

Kwa mujibu wa Wa Jikoni,

Narudia tena, kwa mujibu wa Wajikoni, ambaye pia ni mpigakura halali mwenye shahada halali, aliyekuwa anataka kumpigia Mahona, lakini nikafanikiwa kumwambia CUF ni CCM B na kuhamia kwa Kashindye,

kwa mujibu wa WA Jikoni................

Chadema kimeshinda Jimbo la Igunga.
 
Haukuona tu hata Mkapa hakuwa hata na ule ujasiri anaokuwa nao siku zote. hata hivyo namwogopa sana huyu mzee kwa rafu za kuchakachua. Kule Moshi mwaka 2000 alikwenda mara mbili kwa ndege ucku kutaka Ndesa asitangazwe - akakwama.

Mwaka jana ndiye aliyeipa ushindi CCM kule Zanzibar dhidi ya CUF kwenye uchaguzi wa urais. Mwanzoni matokeo yalikuwa yanatangazwa moja kwa moja alipoona maji shingo aliingilia kati. Tume wakasimamisha. Walipokuja kuanza kutangaza tena mambo yakawa safi kwa CCM

Naamini timu ya CDM imekaa safi kudhibiti rafu za huyu mzee. Bila kusita - Naitakia CHADEMA ushindi!!!
 
Hakika umati ulihoneshwa wa CDM tbc habari, wana igunga wameipokea CDM 100%
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CDM.
 
Hawakuwa na jinsi kwani ilikuwa ni lazima cc ionekane, remember sio wote waliopo TBC wanaifagilia cc. But kimsingi wamejitahidi kuwa fair kwa kutoa habari nzuri ya CDM nawapongeza kwa hilo.
 
Acheni kujifurahisha nyie cdm umati jumatatu asubui mbumge wetu kafumu atapokelewa kwa kishindo jijini dar

nikweli jumamatatu kafumu atapokelewa akiwa ameanguka maana matokeo sidhani kama atakuwa kayapata
 
Acheni kujifurahisha nyie cdm umati jumatatu asubui mbumge wetu kafumu atapokelewa kwa kishindo jijini dar

Makupa kweli akili yako imetulia ? Yaani Mbunge wa Igunga anakuja Dar tena baada ya kutangazwa ?Nimeshangaa mno kwa mwendo huu CCM basi hakuna kitu .
 
Saa 12 kasoro hivi Wa Jikoni alinipigia simu na haya ni maneno yake (nanukuu):

"Nkwingwa sina salio tu, lakini ukweli nkwingwa hapa niko kwenye mkutano wa Chadema. Kuna umati mkubwa sana, yaani watu ni wengi kama mamilioni....sijui nisemeje".

Mwisho wa kunukuu.

Nikamwambia akate simu nimrukie hewani.

Ukweli usio na chembe ya unafiki wala ushabiki:

CCM na CUF hawakuwa na watu leo. Watu wote walikuwa kwenye mkutano wa Chadema. Wa Jikoni alikuwa anafika mahala anashindwa kuzungumza ananiachia nisikilize mwenyewe.

Ilikuwa ni shamrashamra za ushindi mkubwa zikiambatana na sauti ya ukombozi, "Peoples Power".

Kwa mujibu wa Wa Jikoni,

Narudia tena, kwa mujibu wa Wajikoni, ambaye pia ni mpigakura halali mwenye shahada halali, aliyekuwa anataka kumpigia Mahona, lakini nikafanikiwa kumwambia CUF ni CCM B na kuhamia kwa Kashindye,

kwa mujibu wa WA Jikoni................

Chadema kimeshinda Jimbo la Igunga.

ubarikiwe milele kwa taarifa hii tamu ajabu
 
Back
Top Bottom