TBC Mnatuvunja Moyo Jamani

Wakati mishahara yao inategemea kodi zetu
 
Mubashara ni exclusive kwa ajili ya Mr Jiwe tu, hata bunge haliruhusiwi.

Tuna ziara ya siku 8 Mbeya huko ndiko kilipo kipaumbele cha Tbc kurusha matangazo mubashara.
Watuonyeshe kila tukio siyo wana katakata hata pale Jiwe atakapo imbishwa nyimbo za kuisifia cdm
 
Kweli Madaraka matamu. nikikumbuka makala za Dr. Ryoba kwenye magazeti mbalimbali enzi hizo, sikutegemea kabisa angeshindwa kusimamia Shirika la habari kwa kiwango duni kiasi hiki........
Inawezekana ndiyo sheria zao hao matbc zilivyo ukiingia lazima uwe bubu
 
tatizo wanafanya kazikwa kumfurahisha mtu na mtu huyo kaisha wambia hataki kusikia majanga kabla hajatokea. yeye anapenda pesa michango ya waathirika.
 
Achana na upuuzi wa Tbc, unajivunja moyo mwenyewe....wenye akili hatuna habari nayo kabisa..... Wake up mjomba.
 
Tbc ni uozo na pengine kosa kubwa ni tcra kuzifungia kampuni nyingine kutangaza habari
Tbc iliyoaminiwa haina uwezo huo, sijui tunafanyaje hapa.... Tunapitwa na vitu vingi mno
 

Wako mubashara nchi jirani we ujui Leo uzinduzi wa soko la tumbaku kule kupita kwa kina mwaki
 
Kodi zetu zinatumiwa vibaya jamani
 
Mpaka pole pole akizuru huko ndo wanatangaza! Hopeless media
 
Watazungumza Je bila kuweko wa kusifiwa na kuabudiwa ?!. Kwa hakika walitakiwa wawe update kwa kila hatua kupitia TMA na hata mashirika ya nje
 
Tatizo sio wafanyakazi ama Ryoba nafkiri shida ni serikali haiwekezi vya kutosha napia inawawekea vimasharti flani.
Kuhusu mtwara pengine hakuna kilichotokea ndiyo maana wamepotezea. Watabiri wetu wahali ya hewa nao wanashida zaidi ya kutabiri 'kutakua na mingurumo ya radi mawingu kiasi na mvua za hapa na pale' hamna utabiri mwingine wanaouwezea.
 
Mhando kaondoka na TBC yake yote anayotakoni mfukoni wamuombe radhi tido mhando
 
Ingekuwa habari inayohusu ccm ama magufuli ungewaona wa kwanza kuirusha, yaani hio habari ya mtwara kwao sio habari, ni bora wapige muziki wa bongo fleva watajiona wamefanya kazi, natamani tbc ingefutiliwa mbali itoweke kwenye uso wa dunia
 
Hapa naona tatizo kubwa lipo kwenu mnaotazama hiyo TBC..

Binafsi huwa sitazami hiyo TV, kwa hiyo hizi frustrations siwezi kuzipata kamwe.
 
Kutoa taarifa ya kimbunga hicho wanaogopa itaonekana kama magufuri kakileta. Wanasubiri aende kuwapa pole ili watege makamera yao kuonyesha kwamba amekidhibiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…