NnyaMbwate
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,678
- 1,204
Hivi hili haliwezi kuleta mkanganyiko hususani wa kimaadili ya vyombo vya habari?...
Maana kwa tafsiri ya haraka ni kuwa Star TV imetumika kuiponda TBC, hata kama Ndg Machali kaeleza ukweli
Acha uzushi wewe!Tena mtangazaji alifanya juhudi kumkatisha Machali asiendelee kuiponda TBC lakini Machali alikomaa.Hivi hili haliwezi kuleta mkanganyiko hususani wa kimaadili ya vyombo vya habari?...
Maana kwa tafsiri ya haraka ni kuwa Star TV imetumika kuiponda TBC, hata kama Ndg Machali kaeleza ukweli
Anataka kualikwa akatie shombo? Kama mtu haipendi TBC1 asiangalie
Akiongea katika kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na Star tv,mh.Machali amekiponda kituo cha tetevision cha umma cha TBC 1 kuwa kina tabia mbaya ya kualika watu wenye mtizamo wa chama kimoja na hapa alikuwa akimanisha wafuasi wa CCM ndio wanaoalikwa.Mh machali ameongeza kuwa anakatwa kodi kuiendesha TBC na kile ni chomba cha umma.
Wakati huo huo,Machali ameisifu Star tv kwa kualika wageni bila kupendelea upande wowote,ambapo leo amealikwa yeye pamoja na mh.Assupter Mshana kutoka CCM kama wageni kujadili yanayojiri katika bunge la katiba na mada ya leo ikihusu uhakisi wa Tanzania kwenye Hati ya Muungano.
MY TAKE:
TBC kweli wana tabia mbaya.
Kama serikali ya CCM inaonekana kuitumia TBC kwa sababu za kisiasa,je huu si ushahidi wa kimazingira wa serikali ya CCM kutumia vyombo vya dola(polisi) kwa madhumuni hayo hayo?
Swali la kujiuliza hivi ni kwanini TBC1 wanakwepa kuwakaribisha wazungumzaji wenye mitazamo tofauti (Wanaotaka serikali 2 v wanaotaka serikali 3). Je ni kweli kwamba TBC1 wameshagundua kwamba wanaotaka serikali 2 hawa HOJA bali VIOJA, hivyo kuwashindanisha kwa HOJA na wanaotaka serikali 3 itakuwa ni kumvua nguo MFALME? Hivi katika zama hizi za TEHAMA ki/viongozi wanaweza kuficha UDHAIFU wao kwa njia hii? Just thinking aloud
Acha uzushi wewe!Tena mtangazaji alifanya juhudi kumkatisha Machali asiendelee kuiponda TBC lakini Machali alikomaa.
Machali ametoa maoni yake, na kwa vyovyote si maoni ya STAR TV.
Hivi si unafahamu kuwa kuna Uhariri wa habari?
Swali la kujiuliza hivi ni kwanini TBC1 wanakwepa kuwakaribisha wazungumzaji wenye mitazamo tofauti (Wanaotaka serikali 2 v wanaotaka serikali 3). Je ni kweli kwamba TBC1 wameshagundua kwamba wanaotaka serikali 2 hawa HOJA bali VIOJA, hivyo kuwashindanisha kwa HOJA na wanaotaka serikali 3 itakuwa ni kumvua nguo MFALME? Hivi katika zama hizi za TEHAMA ki/viongozi wanaweza kuficha UDHAIFU wao kwa njia hii? Just thinking aloud
CCM daima ni waoga kuukabili ukweli!
Hawapendi wapingwe hata kama wanapotosha....
Hili halijaanza leo... fuatilia hata kwenye midahalo mbali mbali
Wakijua kuna hoja nzito zinapingana na zao basi wanaingia mitini! (Ref: Kikwete, mchakato majimboni, BMK, n.k)
Hivi si unafahamu kuwa kuna Uhariri wa habari?
Umenishangaza kwa kiwango kikubwa! Wewe ulitaka "mhariri" aingie kichwani mwa Mh. Machali na kumkataza asiseme alichosema? Jamani tusiwe wepesi wa ku-criticize bila kutafakari hoja za wenzetu!