TBC Mnakera sana!

edinajailos

Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
22
Reaction score
18
Jamani hiki Chombo cha utangazaji kinachojiita Cha Umma kimepoteza sifa ni bora kiitwe chombo cha CCM.Nasema hivyo kwa sababu hakitendi haki kwa watanzania kwa mfano vipindi vingi vya mahojiano kama Jambo asubuhi wanaohojiwa ni makada wa CCM hasa ktk Mchakato wa katiba mpya.Wanachokifanya wanachukua kada wa CCM na wajumbe wale 201 ambao ni makada wa CCM mfano Kingunge na kuanza kuendesha mdahalo juu ya katiba mpya.Jambo ambalo linakuwa limeegemea upande mmoja.

Mie Sina chama lkn kitendo hiki kinachofanywa na TBC hakikubaliki kwani hili shirika linaendeshwa kwa kodi zetu ikiwamo kodi yangu.Mfano mzuri ni hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa kufungua bunge imerudiwa zaidi ya mara kumi,cha kushangaza hotuba ya jaji warioba haikurudiwa kama ya rais,wakati ya warioba ndiyo ilibeba sauti kuu ya watanzania. Hata taarifa za habari ziko katika mlengo wa CCM.Sikatai kuwa hotuba ya rais isirushwe bali ninachokisema ni kuwa kuwe na msawazo ktk kurusha habari.Igeni mfano wa STAR TV na ITV wanajitahidi kuweka check and balance ktk midahalo yao.

Napendekeza hiki chombo kibadilishwe jina na kisiwe Shirika la Utangazaji la Taifa maana hakibebi maudhui ya watanzania bali kinabeba maudhui ya kisiasa zaidi.

-------------


 
TBC imejaaa kunguni na mende.. Ukiwa Professional kama Mhando unaonekana adui.. Siasa ilibidi ziwe kwa maslahi ya taifa mfano tatizo la Rwanda na Tanzania sasa wao wanaleta siasa zenye kufisha maslahi ya taifa.. ila maslahi ya kikundi flani. Halaf ndo tunaambiwa kauli mbiu iwe Tanzania kwanza.. Mbona wao wanafanya Tanzania baadae...?? Tunatengeneza taifa la wasaliti na watoto wetu watajifunza usaliti..
 
nakupa pole kwa kuwa na moyo wa kuendelea kuangalia icho kituo, mie nilishaacha kukiangalia siku nyingi, acha wale kodi yangu kwa upuuzi wao wa kuegemea upande mmoja ila nilishawatoa kwenye mawazo yangu, bora niangalie zangu vituo vingine vya habari, kuangalia TBC ni sawa na kusoma gazeti la habari leo hakuna jipya zaidi ya kujipendekeza kwa serikali hata kwenye mambo ya msingi ambayo watanzania wanataka waone mawazo ya aina zote ili kupima hoja za msingi na kufanya maamuzi sahihi.
 
Duh kumbe hili linagusa wengi, kwakweli TBC wanatuma kufanya kampeni za CCM kwenye mchakato wameenda mbali zaidi hata watu wanaojidai kuwahoji mitaani nao ni CCM. Kiukweli wanashindwa/kwa makusudi hawataki ku balance story. Hovyooo, tena bora yule cjui nani aliekuwepo mwanzoni kwenye kipindi cha jambo Dodoma alikuwa anahoji maswali ambayo CCM wanatakiwa kujibu.

Lakini huyu Mama ni kama sanamu kaletwa pale hana mbele wala nyuma, huu wizi wa kodi zetu kuna siku mtazilipa bila kupenda.
 
naipongeza sana tbc kwa vipindi vyake murwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, sio kama tv station zingine vipindi vyao ovyoooooo
 
Umechelewa kulibaini ndugu,ila afadhali umegundua.tukisema tunaonwa sisi ni cdm,hawajui kuwa tunataka kupata maoni ya upande mwingine pia
 
huna hoja, zaidi unalalamika tu
 

kwanzia hii siku niliwaogopa tbccm
 

Attachments

  • 954792_645536985501218_735193061_n.jpg
    10.1 KB · Views: 326
Pole ndg mimi nilishasau kama kuna chanel inaitwa TBC, tangu wasitishe mchakato majimboni kama wewe bado unaangalio uko ulimwengu wa giza totoro wajanja tunaamka na Tuongee asubuhi na star TV Baada ya hapo tuangalia taarifa motomoto na ITV daimad
 
Na nyie mmezidi uchokozi, mtu makini kama wewe unatafuta nini tbc? Mimi na familia yangu vipindi pekee tunavyo angalia tbc ni hivi hapa, Ze comedy, chereko na bunge basi kabla na baada ya hapo mwendo ni super brand, Channel 10 na Star Tv basi, vinginevyo maigizo toka Nigeria!
 
Pole ndugu,

Bado unaangalia TBC? Mm nilishaacha muda mrefu saana. tafuta vituo vya maana uangalie..


 
Wewe unaakili nyingi sana sana MUNGU akupe ujasili zaidi fata njia kuu acha tbccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…