TBC Mikocheni imekuwa branded na StarTimes

TBC Mikocheni imekuwa branded na StarTimes

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
710
Habari nilizozipata hivi punde zinaeleza kwamba majengo ya Shirika la Utangazaji Tanzania (Tanzania Broadcasting Corporation) yaliyopo Mikochen, Barabara ya Ali H. Mwinyi, yamebadilishwa muonekano wake kwa nje.

"Kama unafika pale kwa mara ya kwanza unaweza kudhani umepotea kwani hakuna hata kabango kadogo kenye nembo ya TBC", kilisema chanzo cha habari hizi na kusema habari zaidi zitapatikana pamoja na ushahidi wa picha.

Itakumbukwa kwamba jengo la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia liliwahi kupakwa rangi ambayo ilikuwa mchoro wa nembo ya kampuni ya simu ya Vodacom, jambo ambalo liliweka taswira mbaya mbele ya jamii.

Lakini hili la Startimes linaashiria kuvuka mipaka ya uvumilivu, kwani linaitambulisha TBC kuwa ni ama kampuni tanzu ya Startimes au ndio Startimes yenyewe.

Haiyumkini uongozi wa TBC ulikuwa katika hali gani kukubali jengo lake kubatizwa jina la Startimes na utambulisho wote wa TBC kuondolewa.

Je, walighafilika?

Tutazidi kuwaletea habari zaidi za tukio hili.
 
Yawezekana hakuna ufahamu. Bali ninachojua Tbc ni mmiliki mwenza wa kampuni ya startime tanzania.
Hivyo sidhani kama ni vibaya
 
Hilo shirika hata majengo yote yangepigwa full black bila cha nembo wala nini ni sawa tu. Hawa ni sehemu ya wabakaji wa demokrasia hawahitaji kutambuliwa kwenye jamii.
 
Na ndio maana kwa mkulima wa kawaida ulimwengu wa digital anajua kama ni startimes pekee,wakati Ting,digitek,dstv n.k wamo humo humo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Na hii nayo ni Breaking News? inawezekana umepitia kwa Ma-drug dealer pale Lumumba na kupata kitu chako
 
kawaida tushazoea siyo breaking wala chochote just normal.
 
hiki ni kioja kingine cha mwaka kama siyo cha mwezi.
 
Kama ikulu ilibinafishwa hadi akina Kova kusachiwa na Mbwa wa Kimarekani, itakua TBC ccm.?
 
Jengo la TBC kuwa branded Star times haishangazi hasa kama unajua Tanzania ilipo sasa na kama unajua hilo jina Star Times lina ashiria nini.Kwa bahati mbaya hatujitaabishi kujua mambo.
 
Picha ziko wapi?!

262430.JPG
 
Yawezekana hakuna ufahamu. Bali ninachojua Tbc ni mmiliki mwenza wa kampuni ya startime tanzania.
Hivyo sidhani kama ni vibaya

So unamanisha kwa kuwa Exim Bank wanmiliki Hisa NMB , Basi wahamie Majengo ya NMB na Kuyapaka Rangi ya Exim Bank.
 
Hilo shirika hata majengo yote yangepigwa full black bila cha nembo wala nini ni sawa tu. Hawa ni sehemu ya wabakaji wa demokrasia hawahitaji kutambuliwa kwenye jamii.

tangia wabadilishe jina la ubatizo ndo kabisaa wamezidi kuwa matangazo ya vificho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom