TBC,kwa nini hamtaki watu wajifunze?

TBC,kwa nini hamtaki watu wajifunze?

Toosweet

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Posts
2,140
Reaction score
1,983
Sijui nani wanamiliki TBC.Siku ya tarehe 18 Aprili kuklikuwa na mdahalo uliorushwa na TBC moja kwa moja na nilikuwa nikimsikiliza Profesa Palamagamba Kabudi akiwasilisha mada.Alikuwa akiongelea mchakato wa mabadiliko ya katiba toka mwaka 1962,1977,1984.Alipofika kwenye mchakato wa sasa hasa eneo la muundo wa serikali na kusema kuwa muundo wa Serikali Mbili au Tatu hautavunja Muungano bali Serikali ya Mkataba ghafla mitambo ikakatika.Wakaweka kipindi cha kumbukumbu ya Maalim Gurumo,historia ya Muungano baada taarab.Kwa nini TBC hawapendi watu wajue siasa na maendeleo ya nchi yao?Tumewachoka!
 
TBC unaimiliki wewe na mimi kupitia kodi tunazolipa. Tabia na uhuni wanaoufanya kusema kweli unasikitisha sana, mengi yamesemwa kuhusu TBC lakini imekuwa ni kama kutwanga maji kwenye kinu. Jamii ya watanzania inatakiwa itafute uamuzi wa kuidhibit TBC kwa kuweka mkakati maalumu ikiwa ni pamoja na wanaotaka kurushiwa vipindi live kuwasusia na kuwanyima matangazo ya biashara ili washike adabu kwani bado kuna vituo vizuri tu vya TV ambavyo vinaweza kurusha matangazo muhimu na wananchi tukayapata kwa ukamilifu mfano ITV, STAR TV, nk....ni maoni yangu
 
Yule kiongozi wa hicho kituo....., haoni kwamba anawajibu kwa UMMA zaidi ya matakwa ya watawala?

Very bad....!
 
Wana malizia muda wao maana mwakani ccm wanang'oka na watangazaj wote tbc wanaondoka wakajiunge uhuru fm na clouse fm
 
Back
Top Bottom