TBC and ITV on YOUTUBE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBC and ITV on YOUTUBE

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by epigenetics, Mar 14, 2009.

 1. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kwanini vyombo vya habari Tanzania havina youtube channels? I mean, putting news clips online on youtube for Tanzanians in the diaspora would be a great idea.........

  Watani wetu wa jadi kwa mara nyingine wanachangamka zaidi yetu:
  YouTube - NTVKenya's Channel

  YouTube - mwambaocom's Channel

  Please, tech savvy Tanzanians hold this matter record news for us and post them for us online....
   
 2. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hakuna 10%.
   
 3. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hili jambo ni jema kwa wenzetu wa TBC na ITV na Tv nyinginezo za Tanzania kulivalia njuga.
  Tuamke, tusisubiri kusema "Wenzetu wametuzidi".
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Tusiwe na haraka sababu watani wa jadi wameanzisha si unajua walivyo kimbelembele, tusibiri fibre optic project then we can start it. Tatizo jingine ni sisi wenyewe IT at Managerial Level hawako update. but with time we will reach there
   
 5. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  sio siri na wala si kutaka kulinganisha na watani wa jadi,lakini wabongo TUMELALA tena FOFOFO...!hwa TBC wenyewe hata website hawana(at least kwa jinsi nnavyojua),sasa tunategemea waanzishe you tube channel?ukiangalia hata radio streaming pekee hatuna,zaidi ya jamaa wa dullenet wanotusaidia kila siku kutuwekea matukio mbalimbali ya nyumbani>bado mambo tunafanya kienyeji sana.inabidi tuamke kwa kweli kwani inasikitisha sana....
   
 6. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Our lack of innovation is like a curse, it needs to be broken
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  mhhh wewe jamaa uko shalow sana........endeleeni kusubiri optic yaani kuwa na account youtube na kupost news zao mpaka msubiri fibre optic my ass......

  ....leo hii hata eio hamna online.....kisa mnasubii fibre......na uwezo wa kuhost zeutamu mlisubiri fibre?
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Hapa pia kuna hatari ya kuvitwika vyombo hivi lawama nyingi lakini ukweli ni kwamba
  hata wananchi wa kawaida wanaweza kufanya hivi katika spirit ya "Wikinomics"

  Ukiwa na computer, na video card inayoweza ku capture content from TV, internet connection nzuri unaweza ku capture content na ku upload kwenye u tube.Angalau taarifa za habari au/na matukio muhimu pamoja na vipindi vya mahojiano moto.
  ?
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Basi wafunge vituo vyao vya redio na tv...maana wananchi wanaweza kuwa na redio zao kama mwanakijiji na magazeti yao kama blogs na tv zao kama youtube....
   
 10. A

  Audax JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi ni mtanzania ambaye nipo nje ya nchi,nasikitika saana juu ya hili,TBC na ni television ya taifa kuwa nyuma kwa kila kitu maana yake nini? Kwenye u-tube unakuta wanyama tu hamana cha zaidi,watu wamepost shughuli za kilimo,uwekezaji, michezo na mambo mengine mengi saana, mpaka tunaona aibu kutaja nchi yetu,.Kwa mtindo huu kupata wawekezaji ni ngumu saana,ukionyesha wanyama tu haitoshi kwani hata hela yenyewe haiwanufaishi wananchi inayolipwa na watalii. Hapa la muhimu ni kutangaza sector tofauti,maendeleo yaliyopo,matarajio na namna ya kuborsha,shughuli za uzalishaji na mambo mengi,Naomba tuamke,we are lagging more than 60 degrees uknow.!! I don't like it!!

  Huko cnn ndo ucseme,nchi zinazojitangaza zinatuzidi nii sisi? Ebu mimi cshangai ila alichokisema yule billionea aliyehudhuria mkutano wa IMF ni kweli kabisa,tunapoteza muda kuomba omba na c kuweka misingi imara ya kuondokana na kuomba omba, angalia jamani kama billigate peke yake anamiliki pesa ambayo ni budget ya tanzania kwa iaka zaidi ya sita,yeye yupo peke yake na sisi tupo 45 million,ujue hapo kuna tatizo tena kubwa saana.
   
 11. Iwindi_Mbalizi

  Iwindi_Mbalizi Member

  #11
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 1, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mimi nipo China na two weeks ago nilikuwa hapo Tanzania,Nafikiri in Tanzania Internet is still not a priority kwa Watanzania wengi ikiwa ni pamoja na wale ambao wamejaliwa na kuwa na uwezo wa kuweza afford Internet.Nguvu nyingi sana imewekwa katika matumizi ya Mobile phone ambalo kwa mimi naona ni kosa kubwa kwa dunia ilipofika leo hii.Matumizi ya mobile phone ni very Expensive hapo nyumbani but still kila mtu ana mobile,But nobody remembers Internet or even kumiliki Computer isiyo na Internet.Wafanya biashara wengi hapo nyumbani wanatumia simu kuendesha biashara zao kitu ambacho hakiwezi kumleta katika ushindani na mfanyabiashara wa dunia ya leo.Na ndiyo maana hata bei za vitu vinavyokuwa Imported hapo nyumbani ni Expensive sana,au ni Feki.
  Kwa kutumia Internet mambo mengi mtanzania anaweza fanya na mfanyabiashara mwingine aliyepo popote hapa Duniani na wakati mwingine
  haina haja ya yeye kufungasha mipesa yake katika kiroba na kuja China
  kufunga vitu feki,wakati anageweza kaa Ofisini kwake na akamwagiza mtu
  amletee mali safi plae alipo na akamlipa pale pale.Au kama ana kitu kizuri cha kuuza angemwonesha kwa picha tu mtu aliyepopote Duniani na akafuata kitu
  chake pale Bongo na kununua.
  Haya mambo yote ya kama habari kuwekwa katika mitandao nafikiri yanatokana na watu walioachwa na Dunia ilipofika kubakia kuwa ndiyo wafanya maamuzi na wale wenye uwezo wa kubadili haya mambo kutopewa nafasi za kuleta mabadiliko ili Tanzania nayo iweze kuwa sawa na Dunia ilipo sasa.
  Ninawajua rafiki zangu kibao ambao najua wana uwezo wa kubadili mambo lakini hawajapewa nafasi za kufanya hivyo hapo nyumbani.Wengine wamesoma
  ng'ambo Masters za IT na kadhalika lakini wakienda omba kazi watu wanawakwepa kuogopa nafasi zao kupotea,na wengine wanaishia fanya vishughuli vyao vidogo ambavyo haviwezi saidia badili nchi yetu.
  Anyway suggestion yangu ni kuwa wananchi wa kawaida kila mtu ajitahidi
  kumpeleka mtoto wake shule hadi atleast ngazi ya chuo kikuu,hapo ndiyo utaona mambo automatically pole pole yanabadilika maana hata mtu abane vipi kila mtu atakuwa amefunguka na anajua Dunia inaendaje na sisi watanzania tunatakiwa tuendeje.Mfano mzuri ni mimi na watanzania wenzangu nilio nao karibu hapa China,ni nguu kufikiria kuwa nikirudi nyumbani nitaishije bila internet,kwa hiyo ninaamini kama 100 kati yetu tutarudi nyumbani basi angalau 40 watahakikisha hawakosi Internet wakiwa Tanzania na ndiyo mabadiliko yatakavyotokea pole pole Habari zote zitakuwa katika Mitandao.
  Mwisho kila mtu asiishie kulaumu bali pale alipo aangalie yeye binafsi anaweza changia vipi kuleta mabadiliko![​IMG]
   
Loading...