TB Joshua akamatwa!

Status
Not open for further replies.
Joined
Aug 16, 2014
Posts
59
Reaction score
48
Tangu tukio la kuanguka jengo litokee, TB Joshua ameonekana kuwa mwenye uchungu sana hali iliyopelekea awe mbele za Mungu kwa wakati wote.

Kitendo hicho kimepelekea TB Joshua kukamatwa na nguvu ya Mungu mara dufu, sasa anatisha sana! Shetani anasota mno, hata akikuombea kwa TV tu unapokea nguvu ya ajabu hapohapo. Hatari sana! Karibuni naangalia ujumbe wake wa jumapili ya tukio alioutoa.

Emmanueeeeeeeeeel-God with us!
 

Tizama jambo hili
Shetani ni mungu wa dunia hii na ana nguvu kuliko!!
pamoja na nguvu alizo nazo hawezi kumushinda Yesu
Hebu fuatilia vizuri matukio ya maangamizi katika bible .Ukweli ni kwamba maangamizi yote yalitokea pale ambapo Shetani alikusanya watu na kuwaposha na maangamizo hayo yalifanyika kama onyo
Sasa tafakali ni wapi ambapo Mitume walikunya watu kwa ajili ya Neno harafu wakaangamia?????
Hakika nakwambia hilo ni onyo kwa walimwengu na kama umeuona upako kwa TB Joshua na hujamuona Yesu ndani yake jihadhari
 
Ndugu wa mtu anayedaiwa kuwa ni mlemavu wa akili, Galus Focus Nguruwe (35) ambaye ni mwalimu wa sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship lililopo Boko Magengeni jijini Dar kuwa wamemfunga mnyororo ndugu yao huyo kwa miezi nane mfululizo.​
Mwalimu Galus Focus Nguruwe akiwa amefungwa mnyororo
Kwa mujibu wa dada wa Galus, Piencia Focus, ndugu yao huyo alichukuliwa na mke wa mtoto wa dada yao waliyemtaja kwa…​
Ndugu wa mtu anayedaiwa kuwa ni mlemavu wa akili, Galus Focus Nguruwe (35) ambaye ni mwalimu wa sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship lililopo Boko Magengeni jijini Dar kuwa wamemfunga mnyororo ndugu yao huyo kwa miezi nane mfululizo.​
Mwalimu Galus Focus Nguruwe akiwa amefungwa mnyororo
Kwa mujibu wa dada wa Galus, Piencia Focus, ndugu yao huyo alichukuliwa na mke wa mtoto wa dada yao waliyemtaja kwa jina la Doreen kutoka Songea mkoani Ruvuma Januari, mwaka huu bila kuwataarifu ndugu, jambo lililowafanya wamfuatilie na kugundua alipelekwa kwenye kanisa hilo kwa madai ya kufanyiwa maombi.​
Dada wa Galus, Piencia Focus akiwa kanisani hapo
Dada huyo alisema kuwa aliamua kumtafuta ndugu yake hasa baada ya kupata taarifa kuwa aliko amekuwa akishinda huku amefungwa mnyororo mguuni, hali inayomfanya ajisaidie na kula papohapo.
"Japokuwa alikuwa na matatizo ya akili tangu zamani, lakini alikuwa akitumia dawa zake na alipata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa akifundisha shule moja ya sekondari Morogoro," alisema Piencia Focus.​
Kaka wa Galus,Peter Focus akizungumza na waandishi wa habari.
Naye kaka wa Galus, aliyejitambulisha kwa jina la Peter alisema baada ya kupata taarifa kwamba mdogo wake yupo kwenye kanisa hilo aliamua kufika kwa ajili ya kumchukuwa kistaarabu lakini cha kushangaza alijikuta akiangukia kwenye mikono ya waumini hao wakidai yeye ni gaidi na wakamkwapulia fedha zake.
Peter alisema alipoachiwa alikimbilia Kituo cha Polisi Wazo Hill ambapo alifungua jalada lenye Namba za Kumbukumbu WH/RB/6364/14 WIZI TOKA MAUNGONI.
Waumini wa kanisa hilo wakijibizana na ndugu wa Galus kanisani hapo.
Peter alisema alilazimika kuungana na dada yake kwa kushirikisha na vyombo vya usalama ambapo walifika kanisani hapo kwa mara nyingine ili kumkomboa ndugu yao na kuwatia mikononi waumini waliomwibia fedha zake.
Waandishi wetu waliokuwa karibu na eneo hilo walizinyaka taarifa hizo na kufika kanisani hapo ambapo waliwashuhudia ndugu hao wakiwa na polisi wakimchukuwa mmoja wa watuhumiwa waliodaiwa kumshambulia Peter na kuondoka naye.​
Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship kwa muonekano wa mbele.
Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kitendo cha polisi hao kumwacha Galus akiwa bado amefungwa kwenye nguzo na mnyororo kanisani hapo wakidai watamfuata baada ya kumpeleka mtuhumiwa wa unyang'anyi kituoni, jambo ambalo halikuwa la kweli kwani hawakufika kwa siku hiyo.
Waandishi wetu walishuhudia timbwili la aina yake kanisani hapo kati ya waumini wa kanisa hilo na ndugu wa Galus waliorejea kwa lengo la kumchukuwa ndugu yao baada ya awali kumpeleka kituoni mtuhumiwa wa kumshambulia Peter.
Waandishi wetu walipoomba kuzungumza na uongozi wa kanisa hilo ilishindikana na kujikuta wakishambuliwa kwa maneno huku wakitakiwa kuondoka mara moja katika eneo la kanisa hilo.
Waandishi: Hamida Hassan, Gladness Mallya, Chande Abdallah na Deogratius Mongela.
 
Wewe unajiita mtumishi wa Mungu halafu unaandika kihuni kama tapeli flani hivi,
Sasa akamatwa, halafu kwenye habari eti akamatwa na nguvu za Mungu, huu ndio ugoro gani, huwa unaandikia magazeti ya udaku au?!
 

Mtumishi, kichwa cha Habari kimeshtua sana! Sikutegemea km ww ndio umeanzisha hii post!!!!!

Yaani umeleta taarifa kiu-daku sana utafikiri wewe sio mtu wa Mungu au utadhani ww ni wale wanaomuombea TB Joshua mabaya!!!!
 
Hahahaha shetani anataabika mno kuona mshambuliaji namba 9 mgongoni TB Joshua anapefa kitaa tu! Jina la Yesu lihimidiwe!
 

sasa haya kanisa yameshakuwa ni biashara kama kuuza nyanya
 
Wewe unajiita mtumishi wa Mungu halafu unaandika kihuni kama tapeli flani hivi,
Sasa akamatwa, halafu kwenye habari eti akamatwa na nguvu za Mungu, huu ndio ugoro gani, huwa unaandikia magazeti ya udaku au?!
Mimi nilitaka anieleze ni wapi katika bible ambapo Mtumishi wa Mungu alikusanya watu harafu wakauawa???
Hapo utajua TB ninani??
Hilo ni angalizo tu !!
Chukeni hatua na tahadhali
 
mi nilivyoona umeandika kakamatwa nkajua kakamatwa na polisi sa kuja kusoma habar tofauti kabisa kama coca na fanta jarbu kuwa unalink na habar na kchwa cha habar n hayo tu mkuu
 
Hahahaha shetani anataabika mno kuona mshambuliaji namba 9 mgongoni TB Joshua anapefa kitaa tu! Jina la Yesu lihimidiwe!
Ndungu yangu wamekufa watu zaidi ya 100 hapo .
Je Mungu anawezakuachia hilo lifanyike kwa Mtumishi wake??
Wewe huwezi kujifunza hapo??
Yaani watu wakusanywe kwa ajiri ya Neno la Mungu harafu wauawe hapo??
Tunajua watu waliokufa kama hapo ni wale wa Sodoma na Gomora, Gharika, Babeli nk. Sasa unapaswa kufikiria mara mbili hapo kwa TB kuna dhambi gani??
 

Tatizo unadhani na hii ni mijadala ya katiba hahaha! Ya ulimwengu wa roho huyawezi hahaha.
 

kweli nzi kufia kwenye kidonda sio ujinga ni kupenda..
 

Wewe kibaraka wa TB Joshua unayekesha hapa kujaribu kumsafisha TB Joshua, nakuambia unajidanganya mwenyewe. Mungu hadhihakiwi, kama udanganyifu wa Babu wa Loliondo ulivyofikia kikomo, vivyo hivyo udanganyifu wa TB Joshua umefikia kikomo. Mungu wa kweli ameipiga chini huduma ya nabii huyu feki, wala haiwezi kusimama tena!!! Biashara yake ya kutabiri maafa, na biashara yenu ya kuuza maji yake ya upako wa Ibilisi, imedoda!!!! Tafuteni biashara nyingine!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…