Tazama mpangilio wa ovyo wa jiji la Dar

Tazama mpangilio wa ovyo wa jiji la Dar

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
40,930
Reaction score
47,019
Hivi ni nani anawaruhusu watu kuharibu prime land kwa kujenga vibanda mbwa?!

USHAURI: NHC itwae ardhi yote iliyojengwa vibanda vya mbwa kwa nguvu na bila fidia yeyote ile, mipango miji wanyooshe barabara zote vizuri kwa grid system then NHC wafanye mambo!

IMG_0882-X2.jpg
 
Hii picha nimechekiiiii,nimeangaliaaaa sijaona tatizo, au mkuu una alergy na kona kona.
 
Serikali ya CCM imeshindwa kwenye kila Idara.Wizara ya ardhi kwa muda mrefu Wameshindwa kupima viwanja hata kwa kiwango cha chini kabisa.
Kazi yao ni nini hao wataalam wa miji?
Viwanja vilipaswa viwe vimepimwa kwenye maeneo yote ya pembezoni mwa miji yote nchini.
Hili ni tatizo la kutegemea serikali kusimamia kila idara badala ya kuruhusu taasisi binafsi zifanye kazi nyingine serikali ipate kamisheni tu au ushuru.
Wataalam wanohitimu chuo cha ardhi walipaswa wafungue ofisi binafsi za upimaji viwanja ili kuharakisha zoezi hilo na kupunguza urasimu uliopo.
 
jamani hamjasikia WACHINA WANAKUJA KULIPANGA JIJI.......? (serikali ya ccm imeshindwa hivyo imeamua kuwaleta) chanzo gazeti la mwananchi 2/2/2015
 
Hivi ni nani anawaruhusu watu kuharibu prime land kwa kujenga vibanda mbwa?!

USHAURI: NHC itwae ardhi yote iliyojengwa vibanda vya mbwa kwa nguvu na bila fidia yeyote ile, mipango miji wanyooshe barabara zote vizuri kwa grid system then NHC wafanye mambo!

IMG_0882-X2.jpg

Kuwa mkweli, sema CCM iwaue walalahoi uswazi NHC ijenge majengo mazuri yaliyopangiliwa!
 
Hivi ni nani anawaruhusu watu kuharibu prime land kwa kujenga vibanda mbwa?!

USHAURI: NHC itwae ardhi yote iliyojengwa vibanda vya mbwa kwa nguvu na bila fidia yeyote ile, mipango miji wanyooshe barabara zote vizuri kwa grid system then NHC wafanye mambo!

IMG_0882-X2.jpg

Unaposema bila fidia unamaanisha nini? Unaona ni halali kuwanyang'anya watu jasho lao
 
Hahahahahahahaha! Ningeshangaa kama usingekuja kumsifia prof tezi!!

Dar kwa mara ya kwanza tumeona mabadiliko ya jiji wakati wa Kikwete. Juzi nimesikia hata tabata linamwagwa lami na barabara imepanuliwa. Hapa sasa!
 
Uko hapa hapa Dar? hivi haujaona mji unavypbadilika sura toka kaingia Kikwete? hivi hujamsikia hotuba yale aliyosema kuwa mji unabadilishwa? hivi huwa hamna macho au mnayo lakini hayaoni?

Mambo yameanza na plan ilizunduliwa, moja wapo hii hapa: WELCOME TO THE PRIDE OF TANZANIA BLOG. [email]prideoftanzania@gmail.com[/email]: DAR ES SALAAM NEW CITY PARKS MASTER PLAN UNVEILED

Faida foxy hiyo link ina story za 2011. Mabadiliko unayoyasema ni tone dogo sana.

Tunahitaji radical changes sasa kuliko baadae
 
Last edited by a moderator:
Kwa bei ZA nyumba kama hizi hapa huwezi thibiti ujenzi holela. Over my dead body.ImageUploadedByJamiiForums1426017306.423070.jpg
 
  • Thanks
Reactions: rpg
Back
Top Bottom