Tayari nimepanga kutembelea vyombo zaidi vya habari

Status
Not open for further replies.

Honey K

JF-Expert Member
Sep 14, 2008
629
72
Wakati mwingine nasikitika sana kwa mambo yanayoendelea kuipa sura hii jf, inanisikitisha. Pamoja na yote yanayoendelea na kusemwa kote JF bado ni mahali ambapo ukipita utapata kitu, hutatoka bila kitu ndivyo nilivyozoea au tulivyozoea wengi wetu, lakini hali inayoendelea kwasasa inatutia uvivu wengi kuja hapa na si ajabu wako wengi ambao wameshakata tamaa ya kuja hapa kwasababu ndio forum inayoongoza kwasasa kwa habari za kutunga na kuzusha, hatuitendei haki jamii na wadau wakubwa wa forum hii.

Kila kukicha watu hapa wana tunga uongo na kuzusha kama vile ni kweli na wana hakika na wanayoyasema, si ndo maana kuna sehemu ya tetesi basi walau kama huna hakika?

Nimesoma thread ya vita dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na lile la ziara yangu kwenye vyombo vya habari. Nimejaribu kujibu lakini naona mara tu baada ya kuingia threda zile zinahamishwa mara hii huku ukirudi unakuta imeshapelekwa kwingine hivyo mtirirko wa hoja unakuwa tabu.... Hizi ni hoja mbili tofauti na ndo maana nimeamua kuanzisha nyingine maana mkanganyo unaozungushwa kule sijajua ni nini?

Lakini kwa kifupi, tumeandika barua kwenye vyombo vyote vya habari(news rooms) kuzitembelea wakiwemo mwananchi, na ratiba ilishapangwa kuwatembelea, na hata hao tanzania daima nitakwenda na ratiba ipo muda mrefu, sasa huu uzushi mara ooh nape kapeleka sijui taarifa gani kwenye kikao unatoka wapi? Swala hili hata kwenye kikao halijafika ni mpango wa kazi wa ndani ya idara, hichi si chama cha mfukoni hii taasisi kila idara ina mipango yake, sasa hicho kikao cha wapi?

But naamini watu wako kazini zaidi, lakini hata kama ni kazi ya propaganda huwa haifanywi hivyo, uongo wa wazi kabisa na kujaribu kupandikiza chuki'''''' hii imepitiliza.......

Tusiharibu hadhi ya forum hii kwa kuzusha maneno ya siyo na ukweli hata chembe..... Kweli ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huviwezi.......
 
Nnauye Jr. wewe ni moja wapo uliyepandikiza watu kuja humu kuchafua jukwaa na kulishushia hadhi,inasikitisha kwamba muliazimia kwenye kikao chenu pale movenpick kuhakikisha jamvi hili lina kosa hadhi kwa kuwaweka vijana wengi wenye kuleta taarifa za uongo kiasi cha kwamba mumefanya JF isiwe tena source of information,na modes nadhani wakiendelea kuweka kila mwanaJF anayezusha mambo bila facts nitajua nawenyewe chama cha magamba mumewanunua
 
vipi mkuu ni chama gani kinaongoza kwa kuwa na wanachama na viongozi wake ambao ni mafisadi?pili vipi kuhusu ccj ulioiasisi ilikuwa na malengo kama ya ccm ?
 
malipo n hapa dunian,upo kwenye propaganda then beba yote yawe machungu matamu.vumilia acha uwoga ndo ccmagamba mlivyozoea kulilia tu na bado had miguu yako inene
 
Nnauye
je wewe unatumia uongo upi????kama umegundua kuna watu wanatumia uwongo wa waz?????
 
Nape jitahidi kuwalipa vijana wako unaowaleta hapa jf na uwalete wenye akili timamu maana hapa kuna ma great thinkers wa ukweli .pili acha kulialia kama mwanasiasa mchanga pambana kiume kizazi hiki si cha vijana wa kuwatisha wakatishika?pole ukipanda bangi utavuna bangi ,ulichopanda ndo
Unachovuna
 
Nape anashangaa watu kuzusha?!!

Kuzusha mbona ndio hulka ya wakubwa zake kwenye chama chake! Ajiulize Mwenyekiti wake wa CCM alifikaje hapo alipo kama si kwa kuwazushia wenzake? Mbona hata wale walioendelea kuliko sisi kama kule Marekani wanazusha sana. Mara Obama ni Muislam mara hana cheti cha kuzaliwa Marekani. Ni mambo ya kawaida. Unazima uzushi kwa kutoa majibu sahihi.

Nape waingereza wanasema " if you can't stand the heat get out of the kitchen". Kazi uliyopewa na chama chako ni ngumu hasa katika wakati huu. Inabidi uwe na ngozi ngumu sio kulia lia.
 
yaani ukitaka kujua hii topic ni utumbo angalia trend ya replies

sijui huyu jamaa anataka ku address kitu gani
 
Naamini siasa ni mchezo mchafu sana leo unakupandisha na kesho unakudondosha.

Ni mawazo yangu kuwa wanasiasa wengi hapa Tanzania ni wanafiki na kweli wametusahau wananchi wa kawaida. Haiingii akilini wanasiasa kuongea mambo ya kitoto yasiyo na tija yoyote katika kumkomboa mwananchi wa kawaida dhidi ya gharama za maisha zinazopanda kila siku na jinsi gani ataweza kuiona kesho.

Labda kuwa wa wanasiasa ambao hawana chama na tuwape uongozi ili tuone waongee kuwananchi wananchi sio misimamo na umbea wa kichama.
 
Nnauye Jr, vipi kuhusu jengo lile pale UVCCM. Harakati zako zillishia wapi? Naona linakaribia kumalizika kujengwa! Au sasa hivi umeshanyamazishwa na kupewa kazi ya kugundua mishahara ya akina Dr. Slaa? Au na huu utasema ni uzushi?
 
Wakati mwingine nasikitika sana kwa mambo yanayoendelea kuipa sura hii jf, inanisikitisha. Pamoja na yote yanayoendelea na kusemwa kote JF bado ni mahali ambapo ukipita utapata kitu, hutatoka bila kitu ndivyo nilivyozoea au tulivyozoea wengi wetu, lakini hali inayoendelea kwasasa inatutia uvivu wengi kuja hapa na si ajabu wako wengi ambao wameshakata tamaa ya kuja hapa kwasababu ndio forum inayoongoza kwasasa kwa habari za kutunga na kuzusha, hatuitendei haki jamii na wadau wakubwa wa forum hii.

Brother ni kweli hapa kuna matatizo yake, mengine yana muda mrefu mengine mengi yameanza kuonekana baada ya ninyi kuazimia 'KUUVAMIA' mtandao mliouita kuwa ni wa 'CHADEMA'. Lakini kusema kuwa ndiyo mtandao unaoongoza kwa habari za kutunga, naomba uweke wazi umepata wapi hiyo conclusion, maana ili tuweze kuipima kama ni valid or invalid, sound or unsound lazima uweke inferences, ambazo bila shaka zitakwenda sambamba na comparison za forums zingine ambazo kwazo umeamua kui-rank JAMIIFORUMS kuwa inaongoza kwa 'uzushi'

Kama ulijua kuwa JF ni mahali pa 'nondo' mpaka ukapaheshimu kiasi hicho, ilikuwaje ukawaacha wale wazee (actually Chama Chenu Cha Magamba) eti kwenye utafiti wenu na kwenye majukwaa MKAROPOKA kuwa JF ni mtandao wa CHADEMA. Wakati wewe umekata tamaa kuja kupata fikra kinzani hapa na mawazo mbadala ambayo mengine unayaita uzushi kwa sababu umezoea KUZUSHIANA ukiwa kwenye chama cha magamba, Watanzania wamechoka na CCM, kama ambavyo Misri walimchoka Mbarak, Tunisia wakamchoka Beni. Syria wamemchoka

Kila kukicha watu hapa wana tunga uongo na kuzusha kama vile ni kweli na wana hakika na wanayoyasema, si ndo maana kuna sehemu ya tetesi basi walau kama huna hakika?

Jaribu kutoa mifano basi kaka...

Nimesoma thread ya vita dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi na lile la ziara yangu kwenye vyombo vya habari. Nimejaribu kujibu lakini naona mara tu baada ya kuingia threda zile zinahamishwa mara hii huku ukirudi unakuta imeshapelekwa kwingine hivyo mtirirko wa hoja unakuwa tabu.... Hizi ni hoja mbili tofauti na ndo maana nimeamua kuanzisha nyingine maana mkanganyo unaozungushwa kule sijajua ni nini?

Lakini kwa kifupi, tumeandika barua kwenye vyombo vyote vya habari(news rooms) kuzitembelea wakiwemo mwananchi, na ratiba ilishapangwa kuwatembelea, na hata hao tanzania daima nitakwenda na ratiba ipo muda mrefu, sasa huu uzushi mara ooh nape kapeleka sijui taarifa gani kwenye kikao unatoka wapi? Swala hili hata kwenye kikao halijafika ni mpango wa kazi wa ndani ya idara, hichi si chama cha mfukoni hii taasisi kila idara ina mipango yake, sasa hicho kikao cha wapi?

Kwa nini umeamua ku-mention Mwananchi na TZ Daima, tena unasema wakiwemo MWANANCHI...hata hao TZ Daiam, this means a lot in argument.

But naamini watu wako kazini zaidi, lakini hata kama ni kazi ya propaganda huwa haifanywi hivyo, uongo wa wazi kabisa na kujaribu kupandikiza chuki'''''' hii imepitiliza.......

Tusiharibu hadhi ya forum hii kwa kuzusha maneno ya siyo na ukweli hata chembe..... Kweli ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huviwezi.......

Hizi para 2 za mwisho zinaonesha namna gani unavyoweza mipasho.
 
yaani ukitaka kujua hii topic ni utumbo angalia trend ya replies

sijui huyu jamaa anataka ku address kitu gani

LAT-I always salute you,we are proud of you kamanda..You are the one made Chadema to be as it is to people.Keep it up for what you are doing in the parliament!!!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Nape unashindwa kuvumilia mambo madogo kama haya! DR Slaa muulize anawezaje kuvumilia pamoja na kashfa alizopewa na akina makamba tena kipindi cha uchaguzi!
 
lengo lako ni nini katka ziar zako hizi.......halafu unajua wewe ni kigeu geu sana..sasa acha kulia tulia unyolewe kijana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom