lipi limetekelezwa katika haya? Lipi limewekwa kwenye bajeti hii?NISHATI
MUHTASARI WA ILANI YA UCHAGUZI YA 43.
(b) Kufikisha umeme katika miji mikuu ya Wilaya za Bukombe, Kilindi, Simanjiro, Kibondo, Kasulu, Mbinga na Tunduru na kuanza hatua za kuipatia umeme miji mikuu ya Wilaya nyingine mpya.
(c) Kuongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini utakaoshirikisha sekta binafsi na wahisani.
(d) Kuweka mkakati wa uzalishaji umeme wa kutosha na wa gharama nafuu zaidi kwa lengo la kuongeza ufanisi viwandani.
(e) Kuiunganisha Mikoa ya Kigoma na Ruvuma na gridi ya Taifa.
(f) Kuendelea kutafuta wawekezaji wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
(g) Kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika uzalishaji na usambazaji wa umeme.
(h) Kuendelea kutafuta mafuta kwa kasi zaidi.
(i) Kuanzisha mradi wa gesi kwa matumizi ya nyumbani kutokana na gesi ya Songosongo kwa lengo la kupunguza matumizi ya kuni na mkaa majumbani.
MUHTASARI WA ILANI YA UCHAGUZI YA Barabara
(c) Kuendelea kuimarisha barabara nchini zitakazounganisha nchi yetu na nchi jirani kwa barabara za lami; zitakazounganisha Makao Makuu ya Mikoa yote pia kwa barabara za lami na kuunganisha Makao Makuu ya Wilaya zote kwa barabara zinazopitika wakati wote;
(d) Kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara zifuatazo:-
Tunduma-Sumbawanga;Marangu-Tarakea-Rongai; Minjingu-Babati-Singida; Rujewa-Madibira-Mafinga; Mbeya-Chunya-Makongolosi; Msimba-Ikokoto-Mafinga; Arusha-Namanga; Tanga-Horohoro; na ukarabati wa Barabara ya Kilwa (DSM), Barabara ya Mandela (DSM) na Barabara ya Sam Nujoma (DSM).
(e) Kuzifanyia upembuzi yakinifu na usanifu barabara zifuatazo kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami: Maganzo-Maswa-Bariadi-Mkula-Lamadi; Babati-Dodoma-Iringa; Sumbawanga-Kigoma-Nyakanazi; Musoma-Fort-Ikoma; Korogwe-Handeni-Kilosa-Mikumi; Nzega-Tabora-Sikonge-Chunya; Mtwara-Masasi-Songea-Mbamba Bay; MUHTASARI WA ILANI YA UCHAGUZI YA Manyoni-Itigi-Tabora; Ipole-Mpanda-Kigoma na Bagamoyo-Saadani.
(f) Kuhimiza maandalizi na ujenzi wa Daraja la Kigamboni chini ya uongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kuunganisha Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam;
(g) Kuhakikisha upatikanaji wa kivuko kipya cha Kigongo-Busisi (Mwanza);
(h) Kukamilisha ujenzi wa daraja jipya la Mpiji ambalo litawezesha njia mbadala ya Dar es Salaam-Tanga.
(i) Kufanya upembuzi yakinifu, usanifu na ujenzi wa daraja la Mto Kilombero na kukamilisha ujenzi wa daraja la Mto Mwatisi katika Mkoa wa Morogoro.
(j) Kufanya usanifu wa daraja jipya la Ruvu;
(k) Kuendelea kuandaa mazingira mazuri ya kuishirikisha sekta binafsi katika ujenzi na matengenezo ya barabara kwa kutumia mfumo wa Jenga, Endesha na Kabidhi (BOT).
(l) Kuanza ujenzi wa Daraja la Umoja (Tanzania na Msumbiji).
(m) Kuanzishwa Programu ya Taifa ya Usafiri Vijijini.
(a) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa lengo la kulipa uwezo wa kutoa huduma bora kwa bidhaa na abiria wa ndani na wa nchi jirani. Pia, Shirika litaendelezwa kama muhimili wa mpango wa maendeleo wa eneo la Ukanda wa Kati.
(b) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) ili liweze kuhimili kwa uwezo mkubwa zaidii majukumu ya kuboresha huduma kwa bidhaa na abiria na kusaidia shughuli za uendelezaji wa mpango wa eneo la Ukanda wa Mtwara.
(c) Kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli mpya za Arusha-Musoma, Isaka-Kigali na eneo la Ukanda wa Mtwara ambayo itaunganisha Bandari ya Mtwara, Songea, Mbamba Bay, Mchuchuma na Liganga.
(d) Kuimarisha Bandari za Kigoma na Kasanga. (g) Kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe na kuimarisha Viwanja vya Ndege vya Kigoma, Tabora na Shinyanga.
(h) Kutekeleza mradi wa mabasi ya usafiri wa haraka jijini Dar es Salaam.
(a) Kuwawezesha wananchi mijini na vijijini kupata maji safi, salama na ya kutosha kwa matumizi yao ya kawaida karibu na sehemu wanazoishi na kwa mahitaji ya kiuchumi. Lengo ni kuwafikishia huduma hiyo asilimia 90 ya wakaazi wa mijini na asilimia 65 ya wakaazi wa vijijini ifikapo mwaka 2010.
(d) Kukamilisha miradi mikubwa ya maji ambayo ni pamoja na Mradi wa Maji toka Ziwa Victoria kwenda Wilaya za Shinyanga Mjini na Kahama, Mradi wa Maji wa Chalinze katika Mkoa wa Pwani na Mradi Kabambe wa Kufufua Mifumo ya Maji Safi na Maji Taka Katika Jiji la Dar es Salaam.
Ahadi kuu kuliko zote na ambayo haijatekelezwa hata kwa 1% ni ya kuleta "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!"
Kuhamia Makao Makuu Dodoma
125. CCM itaendelea kusisitiza na kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa kuhamishia Dodoma Makao Makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kipindi cha 2005-2010, hatua zifuatazo zitachukuliwa kwa lengo la kuzidisha kasi ya kuhamia Dodoma:-
(a) Kutunga sheria ya kuitambua rasmi Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali na kuweka utaratibu wa Serikali kuhamia huko.
(b) Kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Iringa-Dodoma-Arusha na kukamilisha ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam-Dodoma-Mwanza kama mkakati wa kuendeleza mji wa Dodoma ili uweze kuvutia vitega uchumi.
(c) Kuweka vivutio kwa sekta binafsi ili ishiriki katika uwekezaji kwenye ujenzi wa miundombinu inayohitajika katika ukuaji wa mji, na katika uwekaji wa huduma mbali mbali zinazokidhi mahitaji ya watumishi wa Serikali na wananchi kwa jumla.
(d) Kuongeza kasi ya Wizara za Serikali kuhamia Dodoma, kwa kuwa sasa Serikali inajenga nyumba nyingi za kuishi watumishi.
Chama kilichojaa porojo, CCM
Kuhamia Makao Makuu Dodoma
125. CCM itaendelea kusisitiza na kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa kuhamishia Dodoma Makao Makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kipindi cha 2005-2010, hatua zifuatazo zitachukuliwa kwa lengo la kuzidisha kasi ya kuhamia Dodoma:-
(a) Kutunga sheria ya kuitambua rasmi Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali na kuweka utaratibu wa Serikali kuhamia huko.