Tawala ulimwengu wako ili ukuoneshe picha unayoitaka

Tawala ulimwengu wako ili ukuoneshe picha unayoitaka

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,497
Reaction score
6,215
Angalau kila binadamu anaweza kuuona ulimwengu wake ndani yake. Jambo hili ni jambo linalompa Mwanadamu uwezo mkubwa sana wa kuamua juu ya maisha yake.

Furaha au huzuni ni picha za kiakili ambazo Mwanadamu anaweza kutengeneza ndani yake kwa kujua au kutojua ila angalau anao uwezo wa kuamua kuangalia kile anachokitaka.

Hakuna kinachotoka nje ya Mwanadamu, karibu kila hali tunazokutana nayo katika maisha yako ina uhusiano mkubwa na ndani yako "ulimwengu wako".Unaweza ukaamua kuona shida hata kama kila mmoja naona furaha au unaweza kuamua kuona furaha na ushindi katikati ya shida na taabu nyingi.

Angalau huu ni uwezo wa kipekee tuliojaliwa wanadamu wa kujua na kutawala mwenendo ya ulimwengu wetu ndani yetu kabla ya matukio katika ulimwengu wa vitu.

Maisha yako ni yako na siyo ya mtu mwingine yeyote yule. Unapaswa kuwajibika kwa asilimia Mia moja juu ya ulimwengu wako wa ndani kwa sababu matokeo yake yanakuathiti wewe mwenyewe kwa asilimia kubwa zaidi kuliko wengine.

Tazama ulimwengu wako. Angalia kile unachokiona na kama hukitaki unao uwezo wa kukataa kabla hakijatokea au kukubali na kukiachia kukua na kuchukua umbile ambalo hatimaye hujidhihirisha katika maisha yako ya kila siku kama tukio au hali halisi ya maisha yako.

Kataa usiyoyataka ndani yako na siyo nje yako. Nje yako ni sehemu ya udhihirisho tu na siyo sehemu ya uumbaji.Ndani yako ndiko uumbaji na urekebishaji mkubwa wa ulimwengu wako ulipo au unaofanyika. Usipende sana kulaumu na kulalamika kwa kuonesha vidole kwa wengine (nje yako) jimulike kwa kina utaona namna ulivyo.

Usijionee huruma unapotaka kujikosoa ili kujirekebisha kwa sababu yapo makosa mengi sana unayojisababishia wewe mwenyewe na unapolaumu wengine ni kama unajitafutia huruma ambayo haitokusaidia.

Jikosoe mara nyingi zaidi unapokuwa peke yako kuliko unavyowakosoa wengine kama una nia nzuri na ulimwengu wako. Hauwezi kuwa sahihi hata pale unaonekana kwa wengine upo sahihi ikiwa analiangalia kwa kina ili kuboresha ulimwengu wako.

Hakuna bahati katika kuumba ulimwengu wako.Angalau kila mmoja aliwahi kuyaona maisha yake ndani yake kabla ya wanachokiona katika ulimwengu wa vitu.Hayupo wa kufanya kazi hiyo kwa asilimia mia kwa ajili yako.

Kukata katika kujiumbia picha nzuri kulingana na matakwa yako ni sawa na kukubaliana na unachokiona bila kufikiri kwa kina na kukichunguza. Au kwa kutumia mfano kukata tamaa ni sawa na kuwa katikati ya barabara na kuona gari inakuja kwa kasi mbele yako na wewe kuamua kuzira kukwepa kwa kukubaliana na hali itakavyokuwa aidha dereva apunguze spidi akustue uvuke au akugonge uumie au ufe kabisa.

Unao uwezo wa kusimama katika maisha yako na kuangalia kwa kina ni nini linakuja mbele yako na unataka kije namna ipi kama ukiamua kwa dhati kuwa utawala na siyo kutawaliwa. Maisha yakikuitawala huwezi tambua maana yake.

Usishangae kukutana na mtu akisema kuwa maisha hayana maana ingawa inawezekana kabisa anayedai hayana maana akawa hajui hata maana ya uwepo wake.

Simama amua kuumba tunayoyataka achana na kutunza vinyongo, chuki na wivu. Hivyo vitakusimamisha na kukufanya ukate tamaa au ujizire na uone huna maana wakati maana ipo ila ukaamua kuitafuta.
 
At the midst of this tragedy " COVID-19 " we can still look at what we like.
Never give up
 
Hayupo anayeweza kuisimamisha furaha au huzuni yako kama ukiamua mwenyewe kufanya hivyo.
Simama imara juu ya maisha yako.
"Stop worrying" vuta picha nzuri ya maisha yako hata kama unalala chini kwenye mashimo.
 
Ni ulimwengu wa kiakili unaofanya kazi ya kuumba yanyotokea katika ulimwengu wa vitu.

Plato alijaribu kumuona binadamu kama "Dualist crature" yaani anaweza kuishi katika ulimwengu wa vitu " material world na pia ulimwengu wa kiakili "Intellect world".

Angalau katika ulimwengu huo wa kiakili Binadamu anaweza kuamua kitu kiwe namna gani kabla hakijapata umbile na kuwa kitu katika ulimwengu wa vitu.
 
Angalau tunapata uwezo wa kuona matokeo kabla hayajabeba umbile halisi katika ulimwengu wetu wa ndani.
 
Back
Top Bottom