Tausi ni mzuri ila kasuku kakamilika

Tausi ni mzuri ila kasuku kakamilika

aduwilly

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
1,191
Reaction score
320
Jamaa mmoja alimuomba rafiki yake ampeleke mombasa kununua ndege aina ya Tausi, basi kila walipopita walikuta panauzwa Kasuku tu, wakaamua kumuuliza muuzaji ni wapi panauzwa Tausi, basi yule muuzaji akaamua kuwadanganya kuwa hakuna sehemu inayouzwa Tausi. Basi kasuku akawaambia wale jamaa, ninunueni mimi ili niwapelekeni sehemu wanayouza Tausi, Jamaa wakakubali kumnunua yule Kasuku.

Basi walipoondoka wakamwambia Kasuku awapeleke mahali wanapouza Tausi, kasuku akaanza kuwaonesha njia, gafla jamaa mmoja alipita na kumgusa mmoja wa wale jamaa wawili sehemu mbaya, jamaa alipotaka kuja juu kasuku akamwambia "usimaindi mkuu, hii ndiyo mombasa bwanaaa"

Jamaa akamwambia mwenzake turudi zetu nyumbani tu, Tausi ni mzuri ila Kasuku kakamilika
 
Back
Top Bottom