Tatizo si Ufisadi kamwe

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Jana Rais Magufuli akiongea na Wazee wa Dar es Salaam, katika mambo mengi ya msingi aliyogusia na kusisitiza ni ufisadi. Kwamba nchi hii ni tajiri lakini watu wachache ndio WAMEIFIKISHA NCHI hapa ilipo (omba omba).

Yawezekana ni kweli lakini uhalisia ni kwamba kumekuwa na uzembe katika usimamizi wa shughuli serikalini na Taasisi zake. Hili linaweza kupimwa kwa viashiria/vigezo vifuatavyo:
(1) Ubora wa huduma za umma.
(2) Ubora wa utumishi wa umma na uhuru wake kutoka kwenye shinikizo la kisiasa.
(3) Ubora wa uundaji na utekelezaji wa sera, na
(4) Uaminifu na dhamira ya serikali kutekeleza sera zake.

Wananchi kwa sasa wana matumaini makubwa na Serikali ya Magufuli kwamba itasimamia, kwa nguvu zake zote, kufikia vigezo vinne hapo juu.

KUPANGA NI KUCHAGUA WAKATI NDIO HUU.
 
Haki ikitendeka na Sheria zikidhibitiwa Mengine ya tafuata mkondo !! Kila la haki na amani kwa jamii..
 
Ukiwa mvivu ni kosa kubwa
Kusahau wajibu wako ni kosa kubwa
Kizembea kazi ni kosa kubwa
Kutoa visingizio ni kosa kubwa
Vitendo bila ajizi ndo siri ya mafanikio
 
Tujipime na sisi wenyewe katika nafasi zetu za kazi kiasi gani tunawajibika kufikia malengo bila figisu figisu
 
Back
Top Bottom