Tatizo ni simu au Memory card?

Tatizo ni simu au Memory card?

Finder boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
608
Reaction score
150
Natumia Nokia 6300, tatizo ni kwamba nikidownload music, video au photos naambiwa "file format not supported", hata nikirushiwa nyimbo kwa njia ya bluetooth tatizo linabaki "file format not supported", nikitoa memory card na kuiweka kwenye simu nyingine nadownload kila kitu na ninaweza kupokea kila kitu kwa njia ya bluetooth, lakini nikiirudisha memory card kwenye simu yangu mafaili ambayo yalikuwa yanasoma kwenye simu nyingine kwangu naambiwa "file format not supported". Nikirushiwa nyimbo kwa njia ya bluetooth na kuingia kwenye phone memory tatizo hilo hutoweka, ila punde ninapo hamisha kwenda kwenye memory card tatizo hubaki "file format not supported". Muda mwingine hata nikidownload vitu kwenye phone memory tatizo hubaki "file format not supported".
Naombeni msaada wenu kwa yeyote anayejua tatizo ni nini? na pia solution ya tatizo lenyewe. Asanteni!
 
Unaelewa maana ya file format?
Kwenye mafaili ya muziki kuna .mp3, .wmv, .ogg, n.k.
Video kuna .mp4, .3gp, .3gpp, n.k.

Fanya uchunguzi wa ni mafaili ya aina gani yapo supported na simu yangu, mem card haina shida.
 
Unaelewa maana ya file format?
Kwenye mafaili ya muziki kuna .mp3, .wmv, .ogg, n.k.
Video kuna .mp4, .3gp, .3gpp, n.k.

Fanya uchunguzi wa ni mafaili ya aina gani yapo supported na simu yangu, mem card haina shida.

Yap! Embu atazame ni mafile gan yapo suported na simu yake.Ila hyo ya hata nyimbo kwa njia ya bluetooth inagoma,labda kuna tatzo.
 
VIRUS hao wameshazama kwenye simu,jaribu kuiformat hiyo memory card na kufuta kila file kwenye phone memory ndio uirudishie memory card!
 
Unaelewa maana ya file format?
Kwenye mafaili ya muziki kuna .mp3, .wmv, .ogg, n.k.
Video kuna .mp4, .3gp, .3gpp, n.k.

Fanya uchunguzi wa ni mafaili ya aina gani yapo supported na simu yangu, mem card haina shida.

photo/images/picture zinazosoma kwenye simu yangu format yake ni JPEG, Video ni 3GP, Music ni MP3.
Je hapa nifanye nini nisolve tatizo?
 
kwakuwa memory card ilikubali kwenye simu ingine nadhani tatizo ni simu, ingiza hizi codes *#7370# ufanye hard format ya drive c ya simu (itafuta kilakitu)...hop itasaidia,,,
 
Back
Top Bottom