Tatizo lipo wapi?

Tatizo lipo wapi?

battle2

New Member
Joined
Aug 18, 2022
Posts
2
Reaction score
3
Huenda linaanzia hapa,

Wenye mamlaka hawajui kama wana-mamlaka wanabaki kulalama,
Wangetumia mamlaka yao wasingelalama.

Waliopewa mamlaka wanahisi wao ndiyo wenye mamlaka,

Na kutokana na ufahamu wao wanapambana kuwaaminisha wenye mamlaka kwamba wao ndiyo wenye maamlaka.

Kinachofuata ni maumivu, wanaoumia ni wenye mamlaka,
Wanabaki kulalama lakini wanakosa umoja,

Umoja unakosekana kwanini?
Kwasababu ya njaa na ushabiki,

Wapo wenye njaa lakini kutokana kupata kidogo mabaki yatokanayo na waliopewa mamlaka basi watalalama chinichini, hadharani watasifia.

Wapo wenye njaa wanaotaka na wao mabaki ya waliopewa mamlaka, hawa watajitahidi kuwapamba waliopewa mamlaka japo wengi wao huambulia patupu.

Wapo mashabiki, hawa ni mashabiki kindakindaki kama mashabiki wa timu za mpira,
Hata timu anayoshabikia ifungwe vipi atalalamika tu, ila hatoacha kuishabikia atabaki kuumia,

Lakini hii sio timu ya mpira, wanamatumaini lakini wamefadhaika,
Wanaowategemea wafanye yale wanayoyataka wanawaangusha,
Lakini hawakati tamaa, wanaamini wengine ni wabovu zaidi,
Chakushangaza ni utamjuaje ni mbovu wakati hujawahi kumpa nafasi?

Umoja utatoka wapi hapa?
Labda umoja wa chuma na mbao, chumvi na sukari, kuku na mwewe au maji na moto

Umoja hakuna,
Matabaka yanatamalaki,

Mwenye nacho hamkumbuki asiyenacho, anapambana kukilinda alichonacho ikibidi hata kwa kumuumiza wasionacho.

Anayetumia usafiri wa ndege anasifia usafiri wa basi lenye abiria wanaolalama kero ya usafiri huo wa basi.

Mwenye macho haambiwi tazama,

Lakini anaweza kuzibwa macho asione,
Ila kumzuia ni kwa muda tu, labda umtoboe macho.
Siku akifanikiwa kuona basi utatamani usione kile atakachokifanya.

Ukifanikiwa kupata mwenyewe ni furaha,
Lakini furaha huongezeka zaidi mnapopata wote,
Kwakua hakutakua na wa kukuomba chakwako.

Ni kheri kua na mwanzo mbaya kuliko kua na mwisho mbaya.

Naamini mawazo yangu ni sahihi, lakini mawazo ya wengi huenda yakawa sahihi zaidi.
Kuwasikiliza na wao itanifanya nitambue yupi yupo sahihi kuliko kupambania yangu yawe sahihi na kuishia kuvuruga kabisa.
 
Back
Top Bottom