Tatizo linalosababisha usifanikiwe...

Tatizo linalosababisha usifanikiwe...

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2012
Posts
5,352
Reaction score
7,668
This is from the biblical point of view...lakini naomba nitoe 'disclaimer' kwamba uzi huu hautaambatana na mistari ya bibilia kusupport nitakayoyasema kwasababu mazingira niliyopo sio rafiki kui access bibilia. Ila iko hivi...

Ziko siku mbili tu muhimu kwa mwanadamu hapa duniani:

(1) Siku ya kuzaliwa, na

(2) Siku ya kugundua ni kwanini ulizaliwa (una kipawa/karama gani), kwa maana ya kwamba Mungu alitaka uje duniani kufanya nini ili kulitukuza jina lake. Aidha alitaka uwe dereva, daktari, msusi, mtangazaji, n.k.

Siku ya kifo ni ukamilisho tu na wala si muhimu kwasababu inaambatana na majonzi, tofauti na siku ya kuzaliwa ambayo huleta furaha kubwa, au siku ya kugundua kipawa chako na kukiishi.

Sasa wote tumeshazaliwa, lakini tulio wengi bado hatujagundua ni kwanini tulizaliwa (hatujagundua vipawa vyetu). Tunadhani tumekuja kuzurura.

Inaaminika kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo, wala hakuna mtu mbaya wala mzuri, halikadhalika hakuna kazi mbaya wala nzuri.

Hivyo basi, kama Mungu alikusudia uwe msusi na ukawa msusi kweli baada ya kugundua kusudi hilo kwako, basi kwa hakika ususi utakufanikisha kwa viwango vya juu sana, lakini kama ukiwa mwalimu na yeye alikusudia uwe msusi, kwa hakika utaifanya kazi ya ualimu kwa viwango vya chini mno, hapa ndio pale unakutana na mwalimu analalamikiwa hawezi kufundisha. Kwa kifupi ni kwamba tunalizimisha vipawa vya wenzetu maishani mwetu.

Ufanyeje ili ugundue kipawa chako? Sala zinazoambatana na kufunga hasa chakula, yaani kujinyima, na Mungu atakufunulia kwa namna zake mwenyewe, kama ndotoni n.k.

Unaweza ukafunuliwa leo baada ya kuifanya kazi ya uhandisi kwa miaka 7 ambayo haikua kusudio la Mungu kwako, ukahamia kwenye kusudio lako (labda ualimu) baada ya kufunuliwa, ukapata mara mbili ya mafanikio uliyoyapata kwa miaka 7 ya uhandisi ndani ya muda mchache. Nawatakia jioni njema na utekelezaji mwema wa niliyoyaainisha hapa. Asanteni.

Ni mimi kijana wenu,

Amicus Curiae
 
kijana.... nikigundua leo kuwa kusudio langu lilikuwa ni kubeba zege au kutembeza mayai ya kuchemsha itakuwaje?
Technical question[emoji3]...ila kimsingi hunabudi kuliishi kusudio lako, Mungu ana namna zake mwenyewe za kukuvusha. Na ndo mana nikasema hakuna kazi nzuri wala mbaya.
 
Technical question[emoji3]...ila kimsingi hunabudi kuliishi kusudio lako, Mungu ana namna zake mwenyewe za kukuvusha. Na ndo mana nikasema hakuna kazi nzuri wala mbaya.
haya bana ngoja nianze kufunga.... ila nikigundua kusudio langu lilikuwa ni kucheza mpira sijui itakuwaje
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom