tatizo lafoleni TZ ni udogo wa barabara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

tatizo lafoleni TZ ni udogo wa barabara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Mar 20, 2010.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu mimi nilibahatika kwenda Tanzania mwaka jana, na niliona kwa macho yangu tatizo la foleni. Tatizo kubwa kwa mawazo yangu ni udogo wa barabara, barabara ni nyembamba sana. Tatizo si magari kuna mtu alinidokeza Tanzania nzima magari hayazidi 1.5 million. Hii idadi ni ndogo kuliko magari yaliyopo Houston, Texas zaidi ya 2 million. Mimi kwa sasa naishi hapa Texas na ninakubaliana na hili tatizo kubwa ni barabara nyingi ni ndogo sana. Hapa Texas ninaweza kuendesha kwa speed ya kawaida ya 60 m/hr ambayo ni sawa na 100km/hr lakini hii speed ni kubwa sana kwa Dar. Kwa ufupi magari yanaenda polepole si kwa sababu ya wingi wa magari pekee bali udogo wa barabara, hata kama barabara nyeupe ni vigumu kukimbiza gari kwa sababu magari yanapishana kwa karibu sana na gari moja likisimama mbele linasimamisha watu wote wa nyuma. Tanzania inatakiwa ifanye jitihada ya kupanua barabara na endapo wakijenga barabara mpya ni lazima iwe pana kwa sababu barabara kuwa nyingi haitakuwa solution kama barabara ni ndogo
   
 2. K

  KGM Senior Member

  #2
  Mar 20, 2010
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa BONGO magari si mengi ila, bara bara ndio pamoja na kuwa ni nyembamba mno, ni chache na hazijaunganika.

  Pamoja na kikwete kutembelea nchi nyingi kupita kiasi, alichojifunza ni sifuri, sana kututia aibu tu kwa kuimba kila mara kuwa nchi yetu maskini.
   
 3. m

  miner Member

  #3
  Mar 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ujumbe umeeleweka pamoja na kuchanganya matumizi ya maneno udogo, nyembamba na pana lakini hoja ya msingi ni foleni ya magari Daressalaam hakika barabara kuwa nyebamba zisizo na upana unaokidhi mahitaji ya leo ni moja ya sababu aidha mlundikano wa shughuli zote za kiuchumi na kiutawala kuwekwa katika eneo dogo na kulazimisha kila kukicha magari mengi lazima yaelekee katikati ya jiji ama kufuata huduma za kibiashara au za kiutawala kuanzia ofisi ya mtendaji wa mtaa mpaka Ikulu achilia mbali hata ukihitajia samaki feri.

  Ongezeko la magari pia ni sababu nyingine hata kama si mengi kama Texas lakini ni ukweli usiopingika magari yameongezeka . Tatizo ni wataalam wetu ambao wanaendelea kutoa vibali vya ujenzi mpya wa majumba ya vioo na marefu katika eneo lilelile ambalo halina miumdombinu ya kutosha kukidhi mahitaji ya leo zikiwemo barabara ni kuongeza idadi ya maofisi na wakazi bila kujali athari zitokanazo na maamuzi yao ni pamoja na foleni tunazoshuhudia leo.

  Tatizo la foleni kwangu mimi ni matokeo ya kuwa na wataalam ambao wanashindwa kutumia taaluma zao ipasavyo Mipamgo Miji, wahandisi ambao wanatekeleza maagizo ya watoa maamuzi (Wanasiasa) badala ya kutumia taaluma zao
   
 4. K

  Kinnega Member

  #4
  Mar 20, 2010
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Endapo wakijenga," kina nani wakijenga?

  Usiniambie tukutanulie barabara ili siku "ukipata bahati" ya kwenda kwenu utanue.

  Una jukumu, sio "ukipata bahati," una wajibu wa kwenda kujenga ardhimama yako!

  Kipaumbele chetu cha kwanza sasa hivi sio kutanua upana wa barabara. Usiwe nje ya mguso. Tunajaribu kujenga barabara kuu nchini za matope ziwe za lami!

  Magari ya Tanzania milioni 1.5 ni machache kuliko ya Huoston, kwa hiyo? Huoston, kwa hiyo? Ni sehemu zote za Huoston ambapo mwendokasi ni maili 60 kwa saa? Hata maeneo ya makazi na katikati ya jiji? Kumbuka jamvi hili linapitiwa na mashahidi kutoka nyuzi 360 za dunia, si rahisi kutufunga wote katani. Na 60m/hr ndio nini? Ulitaka kusema maili kwa saa? Herufi "m" ni kifupi cha mita, sio maili.

  Tatizo la msongamano Dar-es-Salaam halitokani na "vigumu kukimbiza magari." Huo muono wa picha za ki Jemsi Bondi-Jemsi Bondi na Nait raida-Nait raida utatuangamiza, hautufai.

  Kuna msongamano Dar-es-Salaam kwa kuwa:

  1) magari ni mengi kushinda barabara
  2) maeneo ya maofisi yamejirundika sehemu moja
  3) kuna upungufu wa taa za kuongoza magari (na askari wanaongoza magari wanaongeza tatizo)wanalegalega
  4) uvunjaji wa sheria za barabarani uliokithiri
  5) ujenzi hafifu, upeo mdogo wa wajenzi (mfano, barabara ya Ally Hassan Mwinyi, njia ya kati, haieleweki ni nani ana haki.)
  6) Misafara mirefu isiyoisha ya viongozi (japo hili si tatizo maeneo yangu Kwa Mnyamani Vingunguti, hawasogei ukanda huu, tuna ghadhabu!)

  Saidia kujenga zenu, barabara za Huoston sio zako, Muha wa Kasulu!
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Naomba msamaha kwa kukosea Title ndugu zangu nilikuwa kwenye ndege. Kwa ufupi bababara ni ndogo sana tatizo kwa mawazo yangu si uchache wa barabara.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Mar 21, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Labda tatizo ni ukubwa wa magari?
   
 7. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,839
  Likes Received: 20,859
  Trophy Points: 280
  LOL teh teh teh teh....mzee umenivunja mbavu...uwiii
   
 8. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuna uhusiano gani wa wewe kuwa kwenye ndege na kukosea kwako title?
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Khe khe khe ... ...... .... tatizo la foleni sio kuwa na magari mengi tu ni pamoja na mipango mibovu hakuna planning, I mean ni Kanyaga twende, unategemea nini wakati kila fedhuli aliyopewa dhamana hiyo anaangalia tumbo lake? Magari yanachangia lakini kama kungekuwa na planning nzuri kusingekuwa na foleni.

  Kuna magari ambayo hayatakiwi kuwa barabarani lakini unayakuta yamo tu hakuna lolote ni Upwagu na Upwaguzi tu.

  Mfano Port access Road sifahamu kama wamebadili jina (beside being there recently huwa siangalii sana haya majina but I think you know what I mean) kwenye makutano na Morogoro Road, Kilwa Road na Pugu Road wangeweza kuinua na kuwa na underpass pamoja na junction iliyoko Buguruni kwenda Tabata kama sikosei. Vile vile barabara nyingi tu ambazo zilikuwa designed kabla ya kupata Uhuru bado ziko vile vile .... .... AIBU.

  Jambo jingine ni kuondokana na usafiri mbovu wa daladala nakumbuka enzi za daladala zilianzishwa na hayati Sokoine ni takriban miaka 30 kama sikosei, sasa wakati ule ilikuwa sahihi Je, tumewezaje ku-improve au ku-develop the scenario 0 (sifuri).
   
 10. N

  Ngala Senior Member

  #10
  Mar 21, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli tuna ufinyu wa barabara na ufinyu wa bongo zetu.All mwinyi asubuhi toka mwenge kwenda town inajaa magari ilihali toka town kwenda mwenge inakuwa nyeupe. Jioni inakuwa ni kinyume chake town to mwenge mafuriko.Hali ni hiyo hiyo moro nyerere mandela na kilwa road.town tangu dahari ilijengwa kwa viwango vya bombay tulipaswa tujenge mji mpya ili kutawanya maeneo ya huduma. Mipango bado wanaruhusu upanuzi wa jiji kule kule kusikoingilika. Matumizi mabaya ya barabara nalo linachangia sokoine na samora zilifanya kuwa oneway ona upuuzi sasa kila mwenye biashara eneo hilo anajimegea na engesho tangu asubuhi hadi jioni matokeo ni kusudio la kupitisha gari mbili kwa uelekeo mmoja ni ndoto.NINI KIFANYIKE.(l)Ondoa maegesho yote barabarani kwa kushusha na kupakia abiria tu. (2) simamisha ujenzi mpya katikati ya mji badala yake vibali vya ujenzi vitolewe kibamba kinyerezi boko ili tuwe na town mpya zenye kukidhi matakwa yote. 3 isiwe lazima kwa kila mwenye saloon car aingize town asubuhi nazitumike zaidi town ice au grand taxi japo ni kero na ni msumari kwa wengi.haĆ­ingii akilini familia inayokaa pamoja na kufanya kazi eneo moja kila mtu akurupushe gari yake. Adhabu wanaipata maana wa kimara tegeta ili awahi foleni kila mtu anamka saa ll matokeo yake saa l2 tayari foleni. Nitachangia panapo majaaliwa
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Huezi kumtumainia mwanasiasa atatue matatizo ya kiufundi wajameni. Ukitegemea kuvuna madafu kwa kupanda chelewa nadhani wewe ndio mwenye matatizo.
   
 12. L

  Lukwangule Senior Member

  #12
  Mar 21, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha kulinganisha upuuzi wa dar es salaam na miji iliyoenda shule wewe. unajua kweli mambo wewe?@ nini unalinganisha nini ahhhh nataka mpaka kutapika. Dar si ufinyu wa barabara ,mbona venice ni finyu na hakuna hekaheka za kipuuzi. Mji huu hauna mwenyewe bwana! meya kachukua sabatical leave,mameya wa manispaa wanafikiria kugombea ubunge unadhani watafikiri na kuiamrisha serikali kuu kuacha upuuzu wa kuruhusu majengo marefu katikati ya jiji ahh nimechemsha sicty ndio wanaotoa kibali ahh upuuzi mtupu kudiskas dar hawana mipango
   
 13. L

  Lukwangule Senior Member

  #13
  Mar 22, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji kudadadeki umedata! umenifanya nicheke duhh! Najua umekasirika kwa sababu watuw anazungumza pumba na wewe ukasema hawa wanaongea ntu labda tuseme magari ni makubwa? ha ha ha ha mwanakijiji hakika umedata. lakini tazama huu ukubwa wa magari unaambatana na uzezeta wetu wa kutojua nini cha kufanya. Dar ilitakiwa katika mazingira ya kawaida kuwapo na Old dar na majengo yasiyoenda juu na ikaanzishwa new Dar yenye taratibu zote za kisasa na watuw akaacha kutia tumboni fedha za watanganyika. Naam nasema hivi kuna mtu alisema kwamba pale tazara pale kungeliweka mambo ya kupishana kwa anga! miaka 50 na ushehe wa uhuru hakuna anyefikiria hilo. Jingine kwanini sote tuende mjini? kwanini tutoe kibali cha kufumua majengo ya zamani na kujenga mapya yanayostahili kuakomodate thousands halafu miundo mbinu ya kawaida ni ya mkoloni na hatuwezi kubadili kwa sababu ndivyo ilivyokuwa? Ndio maana watu ambao wako nje wanachofikiria kupanua barabara. Huu tena upuuzi mwingine ndio maana unasema magari ni makubwa.kwani toka kariakoo mpaka posta ni kilomita ngapi? Unatanua barabara ili iweje? shauri ni mji uac hwe kama ulivyo na majengo yanayotanuliwa sasa yajengwe nje ya mji na kama mtu anajenga jengo jipya basi aambiwe anataka watu wangapi na ajenge ama underground ya kuwekea magari au ghorofa moja la kuwekea magari si kuanika magari barabarani na kuzuia wengine kama ilivyo katika barabara ya samora. Kuna mambo mengi na ndio maana mimi huamini meya wa jiji la dar es salaam yule aliyemkabidhi rais jezi kweli anacheza na sana sana yupo sabatical leave na wakati huu wa Ubunge kuwa wa maana watu wanajikusanyia vijisenti kwenda kuwania ubunge. Fikiria bwanausi wa temeke ameshasema anaenda kuusaka ubunge huko kwenye asili yao unadhani atafikiria kwamba temeke ile barabara ya kodi za wajapan inayokwenda Mbagala rangi tatu ishakuwa kero opale mbagara rangi tatu na ishakuwa kero kubwa pale bendera tatu? Kule Mbagara mashimo na ghafla unaingia katika njia moja na hamad unageuza mabasi manake ndio mwisho wa mabasi hata staili yenyewe haipo.pale bendera tatu jambo dogo sana kabla hatujafikiria kujenga flyover kutuvuisha hadi posta, kutia lami ili yale mashimo ya kwenye njia za reli yamalizike ili watu wakanyage mafuta. mimi sijui mawazo ya kupanua barabara watu wanayapata wapi? unaegesha wapi? na kwanini hawa City waisanzishe usafiri wa uhakika w apublic ili watu waondokane na kutumia magari yao na kuongeza bei ya mafuta kwa sababu ya supply na demand sheria? Ahh kweli mwanakijiji tatizo ni ukubwa wa magari labda!
   
 14. L

  Lukwangule Senior Member

  #14
  Mar 22, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahh wacheni hizo mtu ana miaka minne tu halafu mnasemasema saana kwani imekuwa safari za nje nongwa nini. hii aibu ya umaskini si yako pia. huenda ukawa si tu umaskini wa midolari bali umaskini wa mawazo ndio maana watu wa dar es salaam wanasubiri rais aende Japan anarudi anawaambia nyie mipango miji vipi hii foleni?Suala si uanasiasa! Kwani yeye ndiye everything?Wacheni hizo watu walioajiriwa kama mabwana na mabibi mipango miji wanafanya nini?wakazi wa dar hatuchagu madiwani waliokwenda shule na wenye uchungu matokeo yake baraza la madiwani hopless kisha meya aliyepagawa na kukusanya fedha za kujilimbikizia utajiri mpaka kwa wajukuu zake na mwisho kabisa kuwa na jiji linafanya mipango kihanithi kabisa. Ndio rais mwaka jana alienda nje na alipotembelea dar aliwauliza hivi kwanini hawafikirii namna bora ya kuondoa kero ya usafiri kama kujenga maflaiova? Sasa kama kila kitu ni Rais basi sisi kama hatuna shida ya kufikiri tunashida ya kubebwa na jazba zisizokuwa na maana,sisi ni wasumbufu rais hawezi kuwa everthing! watu wanajikalia tu kutengeneza madili ya misaada na kupeana zabuni za kukusanya kodi zisizojulikana zinafanya nini na hili si suala la rais ni mabaraza ya madiwani kuhoji na kama tulichagua mabomu haya ndio matatizo yake.Miji yote duniani haiendeshwi na serikali kuu ni serikali za watu bisheni basi manake hata Obama alimpigia simu meya wa mji wake akamwambia hampendi jinsi anavyomsaidia yeye kama mpiga kura wake(si kama Rais wa Marekani) tuweni sober tuyaone makosa foleni haikuja ghafla.
   
 15. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hali ilikua hivi hivi kule Lagos, Nigeria. Msongamano kila sehemu. Ikafika mahali mambo yakashindikana afu mji mkuu ukahamia Abuja.

  Wiki ijayo nakwenda kutafuta kiwanja Dodoma.
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Tuhamishe ikulu kwa vile kila mtu natataka kuwa karibu nayo...
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  na leseni za kuletewa home nazo zinachangia sana foleni, na automatic cars nazo. ni kwamba enzi manuals mtu lazima apitie driving school kwanza ndo kweli ujue kuendesha gari, lkn hizi zama za automatic, mtu anaagiza gari haju a wala b ya udereva, gari ikija anatoa alfu stini anapata leseni kesho yake anaingia barabari ili mradi anajua kunyosha stelingi, breki na kupiga honi, hapo tayari dereva. hawa sasa hata uwe kwenye zebra crossing atakupigia honi, badala ya yeye kusimama akusubiri wewe upite, sheria zote za barabarani hazijui.
   
 18. P

  Preacher JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani UKUBWA WA MAGARI - ina ukweli ndani yake - kuna malori yanabeba cement kutoa kiwanda cha Cement Wazo kwenda maeneo mengine ya mji - mh! lorry linaoccupy urefu wa barabara halafu liko slow - mara limeharibika njiani - yaani kwa kweli Dar es Salaam ni Bongo - land -

  Narudia tena barabara zina kiwango cha kuendeshea baiskeli, pikipiki etc. sijui nani anahusika na planning ya mji?? ni Serikali Kuu au Halmashauri?? wanachojua ni kutoza kodi, kutoza malipo ya parking etc. ila kwa vile viongozi wakipita wote mnasimamishwa sidhani wanaona adha za barabara Dar -
  Fedha zote Rais wetu anazotumia kutembea nje ya Tanzania pamoja na jopo lake -ambayo ni kazi ya Waziri wa mambo ya nje - zingetumika basi kuanza kutatua tatizo la Barabara - sijui itakuwaje - Budget ya kulipa watakaobomolewa, budget ya ujenzi wenyewe etc. itengwe jamani - Nchi yetu tunaipenda sana Tanzania ila tukimbilie wapi jamani??? WATANZANIA TUNAISHI KWA KUKABILIANA NA MATATIZO NA SIO KUTATUA MATATIZO - hivyo hivyo tunasonga mbele hadi YESU ATARUDI ATATUKUTA KWENYE FOLENI ZETU - Mungu atupe amani moyoni akija atukute tuna imani bado!
  Tumpe kiongozi gani kura atakayetatua mambo ya msingi kama haya???? nikitazama na kuchunguza na kufikiria SIONI HATA MMOJA - someone advise please
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Goood point Mkuuuu!

  Nadhani ndivyo watakavyo iwe hivyo. ila mie nasema tatizo ni udogo na ufinyo wa akili wa hawa viongozi wetu wanao jitia wanaya jua madaraka vyema kumbe ni bomu kabisa hata mipango miji hawajui kazi kujirundika mji mmoja Dar.

  Kila jambo sielewi wanataka kulifanya liwe la kisiasa siasa
   
Loading...