Tatizo la watu kushindwa kujielezea

Tatizo la watu kushindwa kujielezea

Hivi nyie mnaosema inawezekana mleta mada ni mmoja wao mmesoma mkaelewa alichoandika? Au na ninyi ndio mifano halisi ya alichokisema?! Someni vizuri, mleta mada kasema mwanzoni pale "Watanzania tuna shida....." kama ni mtu unajua kiswahili utaona kwamba hata yeye kajiweka katika hilo tatizo
 
Nawalaumu sana wazazi wangu.Kitu kidogo unafokewa.Kitu kidogo kichapo.Kitu kidogo huwezi.

Washukuru wazazi wako wewe maana ninavyokufahamu wasingekudunda leo ungekuwa mtu wa ajabu sana
 
Watanzania tuna tatizo sana la kujielezea au kutoa ufafanuzi wa jambo fulani au nini kifanyike juu ya jambo fulani. Ukitaka kukubaliana na mimi angalia vipindi vya kwenye television au radio ambavyo vinahoji Watanzania au hata humu JF unaweza ukathibitisha.

Unaweza kupigwa butwaa mtu anavyojibu au anavyoelezea jambo mpaka unajiuliza hivi huyu anaelewa anachoongea/kuulizwa au anaongea na ye aonekane ameongea! hili tatizo si kwa wale wasioenda shule pekee bali hata waliofanikiwa kupata elimu.

Najiuliza sana hii hali inasababishwa na nini? kutojiamini, kukosa ufahamu, uvivu wa kufikiri, kujifanya tunajua sana wakati hatujui au ukosefu wa lishe bora toka utotoni umedumaza akili za watanzania wengi?! na kama tumerogwa basi alieturoga, ameturoga pabaya. tuna safari ndefu sana! Kwa ufupi hili taifa kuja kufanikiwa ni ndoto ya saa sita mchana.

Kama hakuna reading culture kwenye critical matters unategemea nini, jamaa kusoma mpaka awe na mitihani au assignment ya kazini, na kujazana kwenye baa kila jioni!!
 
Washukuru wazazi wako wewe maana ninavyokufahamu wasingekudunda leo ungekuwa mtu wa ajabu sana
Niwashukuru wa nini sasa?.Vitu vingi walikuwa wananiambia siwezi hata kama ninaweza.
 
Naulizwa swali ninalolijua na mgeni ile nataka kujibu tu,mzazi anajibu "hawezi huyo".

may be mzazi alitaka utambue protocol kwenye kujieleza na sio unaongea kila jambo tu kwakuwa unalijua.

mfano christiano ronaldo anajua mengi kuhusiana na real madrid lakini hawezi kuulizwa swali linalomhusu meneja wa timu akajibu yeye
 
may be mzazi alitaka utambue protocol kwenye kujieleza na sio unaongea kila jambo tu kwakuwa unalijua.

mfano christiano ronaldo anajua mengi kuhusiana na real madrid lakini hawezi kuulizwa swali linalomhusu meneja wa timu akajibu yeye

Haishii hapo tu,mzazi ni chanzo cha kutojiamini kwa mtoto.Mbaya sana.
 
bado kuna mambo lazima yawe controlled na mzazi

Wazazi wana makosa kwa sababu hawamsomi mtoto wao.Mtoto mwingine ukimcontrol kwa kumpa adhabu hii unamuathiri,na mtoto mwingine ukimpa adhabu hiyo hiyo haathiriki.Mzazi anatakiwa kumtambua mtoto wake katika adhabu ya kumpa.
 
Kula chakula aina moja too much inasababisha speech disorder.
 
Umeongea kweli mkuu, labda nitoe mfano hai kabisa niliouona kwa macho yangu.

Wiki mbili zilizopita msanii RECHO alikua anaojiwa na mtangazaji wa BBC Chazi Hilary.

Aliulizwa 'kuna changamoto gan katika muziki unaofanya'
Jibu alilotoa ni 'Anatongozwa sana na wanaume wengi wakitoa ahadi ya kumpa fedha.

Nilitegemea kua angesema labda soko bado liko chini au wizi WA kazi ni mkubwa na udhibit ni mdogo.

Hapo kwenye nyekundu ni kweli?ha ha haaaa nimecheka sana
 
Baada ya kuulizwa swali tunaanza kwa kujibu "mimi hapa.....mimi hapa yaani binafsi yangu....... " kazi kwelikweli. Aliulizwa Nyandu (Dogo Hamidu) gari analotembelea alinunua kwa pesa kiasi gani, akatoa majibu mareefu kuwa vijana wanahustle ili watoke, mara hili gari nimelinunua kwa jamaa zangu (akawataja) huwa wanaagiza magari toka nje......mwishoni ndio akajibu swali kuwa hawezi taja kiwango cha pesa, khaaaa!!
 
Back
Top Bottom