Tatizo la watu kushindwa kujielezea

Tatizo la watu kushindwa kujielezea

mtoa mada kasema, pengne sbb ni lishe duni.

hii inawezekana.
maana njaa mbaya sn inaleta utumwa na mawazo tegemezi.
 
Mleta mada naona bado unaliendeleza tatizo hilo hilo, badala ya mwishoni kuja na suluhisho au mapendekezo wewe unaelezea tatizo mwanzo mwisho
 
Huu mjumuisho huu eti "watanzania" , ni wewe mwenyewe mleta mada na nyinyi mliokubali ndio hamjui kujieleza!

umefanyia wapi research?
mjinga sana wewe mutant gene sababu mdomo wako mzito, unafikiri kila mtanzania yupo hivyo!

Invisible au Moderator naomba ubadilishe heading isomeke 'tatizo la watu kushindwa kujieleza' ,
 
Last edited by a moderator:
au ukosefu wa lishe bora toka utotoni umedumaza akili za watanzania wengi??!
nimewahi kusikia hilo japo sijalisoma kwenye chambuzi zenye mamlaka, yani tafiti za kitaalam.

Dhana yenyewe ni kwamba wakati ule wa vita na pia vijiji vya ujamaa nchi iliingia umasikini na njaa kubwa, watu wakadumaa miili na akili. Angalia jinsi Watanzani tulivyo wadogo wadogo, na pia bongo ndani ya vichwa ni ndogo ndogo. Ukisoma mambo ya binadamu wa kale, kina Zinja, utaona ma anthropologists wanapima akili kwa ukubwa wa ubongo. Bongo zetu, kama miili yetu, ilidumaa, na hatuna akili za kutosha.

Ndio maana vitu vingi watu wakisema havi make sense. Rais anasema huyu mtuhumiwa namuweka kiporo ili tumpe haki yake baada ya kumchunguza zaidi. Kiporo maana yake unategemea kuja kukila, kwa maneno mengine umeshamhukumu, kwa hiyo usituambie unaenda kumchunguza, hai make sense.

Taasisi ya Hali ya Hewa ikatangaza majuzi hapa kwamba kuna "mvua kubwa isiyotabirika" inategemewa kunyesha sehemu mbali mbali za nchi siku za karibuni. Kama mvua haitabiriki umejuaje itanyesha na kwamba ni kubwa na ni sehemu mbali mbali na ni hivi karibuni???????
 
Nadhani hata wewe una shida ya kujieleza pia. Daima anza na herufi kubwa mwanzoni mwa kila sentensi.

Wewe ndio una tatizo zaidi maana hata kueleza yaliyoandikwa huwezi. Mleta hoja katumia neno ''TUNA'' maana yake hata yeye kajitambua kuwa ana tatizo hilo, sasa wewe unapooanza kumueleza kuwa na yeye ana tatizo hilo inakuwa ni mwendelezo wa kuthibitisha kuwa hakika kuna tatizo hilo.
 
Watanzania tuna tatizo sana la kujielezea au kutoa ufafanuzi wa jambo fulani au nini kifanyike juu ya jambo fulani. ukitaka kukubaliana na mimi angalia vipindi vya kwenye television au radio ambavyo vinahoji watanzania au hata humu JF unaweza ukathibitisha. unaweza kupigwa butwaa mtu anavyojibu au anavyoelezea jambo mpaka unajiuliza hivi huyu anaelewa anachoongea/kuulizwa au anaongea na ye aonekane ameongea!! hili tatizo si kwa wale wasioenda shule pekee bali hata waliofanikiwa kupata elimu.

Najuliza sana hii hali inasababishwa na nini? kutojiamini, kukosa ufahamu, uvivu wa kufikiri, kujifanya tunajua sana wakati hatujui au ukosefu wa lishe bora toka utotoni umedumaza akili za watanzania wengi??! na kama tumerogwa basi alieturoga, ameturoga pabaya. tuna safari ndefu sana!! Kwa ufupi hili taifa kuja kufanikiwa ni ndoto ya saa sita mchana.
Usiseme watanzania sema baadhi ya watanzania.
Wakorea,wachina na wajapani ndio wanaongoza duniani kwa uwezo mdogo wa kujieleza kimpangilio lakini wako mbali kimaendeleo.
Ni watu waongeao maneno machache mno tena yasiyo na mpangilio mzuri kiradha ya lugha.

Tanzania kabila la wakinga wana hilo tatizo ila ni wafanyabiashara wakubwa.
 
Mkuu mutant gene tatizo linaanzia shule, hatujengwi kuwa na confidence ya kuuliza maswali na kujiamini kujibu maswali, ukiwa unamuuliza mtu swali au unamjibu huku ukiwa unamuangalia unaambia huna adabu au heshima. Wee angalia akitokea mtu kumuuliza maswali magumu kiongozi ataambiwa hana adabu au anamvunjia heshima Kiongozi. Kwa hiyo tatizo lipo kwenye confidence. Nchi za wenzetu wanajengwa wakiwa wadogo tena wakiwa chekechea jinsi ya kuuliza na kujibu maswali huku wakiwa na confidence bila ya kuogopa. Angalia watoto wadogo wakitembelewa na viongozi wao mashuleni mwao wanawauliza viongozi wao maswali huku wakijiamini bila ya woga sio shule zetu huruhusiwi kumuuliza swali kiongozi.
 
heading in offed watanzania wote kwa ujmla, please Moderator wekeni sawa heading! sio watanzania wote hawajui kujieleza!!!
 
Mkuu mutant gene tatizo linaanzia shule, hatujengwi kuwa na confidence ya kuuliza maswali na kujiamini kujibu maswali, ukiwa unamuuliza mtu swali au unamjibu huku ukiwa unamuangalia unaambia huna adabu au heshima. Wee angalia akitokea mtu kumuuliza maswali magumu kiongozi ataambiwa hana adabu au anamvunjia heshima Kiongozi. Kwa hiyo tatizo lipo kwenye confidence. Nchi za wenzetu wanajengwa wakiwa wadogo tena wakiwa chekechea jinsi ya kuuliza na kujibu maswali huku wakiwa na confidence bila ya kuogopa. Angalia watoto wadogo wakitembelewa na viongozi wao mashuleni mwao wanawauliza viongozi wao maswali huku wakijiamini bila ya woga sio shule zetu huruhusiwi kumuuliza swali kiongozi.
Nadhani shule ni baadae mno.... tatizo linaanzia nyumbani. Mtoto wa Kitanzania unatakiwa uondoke sebuleni wageni wakija. Ukishaamkia unaambiwa haya nendeni mkacheze huko....! Huna nafasi ya ku interact na wakubwa na kukomaza verbal reasoning yako.

Mtoto wa Tanzania anaona Rais wake anatangaza kwenye runinga leo ni sikukuu ya uhuru wa Tanzania. Huruhusiwi kumuuliza Baba Tanzania ilipata uhuru lini? Rais na babaako wanajua ni uongo lakini huruhusiwi kudadisi. Kwa hiyo hatujifunzi ku reason kwa sababu haturuhusiwi ku interact na wakubwa wala kuuliza maswali sebuleni wala shuleni.
 
Umeongea kweli mkuu, labda nitoe mfano hai kabisa niliouona kwa macho yangu.

Wiki mbili zilizopita msanii RECHO alikua anaojiwa na mtangazaji wa BBC Chazi Hilary.

Aliulizwa 'kuna changamoto gan katika muziki unaofanya'
Jibu alilotoa ni 'Anatongozwa sana na wanaume wengi wakitoa ahadi ya kumpa fedha.

Nilitegemea kua angesema labda soko bado liko chini au wizi WA kazi ni mkubwa na udhibit ni mdogo.


Jk akiwa France aliulizwa kwa nini nchi yake maskini! Majibu aliyotoa, mfano wako ni bora zaidi!

Mama tibaijuka alivokuwa anajielezea khs escrow, nimepata ukweli wa huu uzi!

Ukiwaskiliza wabunge wetu mle ndani, Daaah....
 
kuna baadhi ya wananchi wana malengo sana ya nchi hii lakin wapuuz wachache wanavunja wenzao mioyo ya kujiamini kwa kile wanachotaka kukifanya
 
Kama wewe mtanzania umegundua hili, basi kwa wageni kutoka mataifa yaliyoendelea wanaona makubwa zaidi na ndio maana hawakawii kuwahadaa na kuwadharau watanzania, iwe ni katika mikataba mibovu au mambo mengine yote.

Tunahitaji sana watanzania kujibidisha sio kwenye elimu ya madarasani tu, kunyanyua ufahamu wetu kwa mambo yote.
 
Jk akiwa France aliulizwa kwa nini nchi yake maskini! Majibu aliyotoa, mfano wako ni bora zaidi!

Mama tibaijuka alivokuwa anajielezea khs escrow, nimepata ukweli wa huu uzi!

Ukiwaskiliza wabunge wetu mle ndani, Daaah....

Mimi Huwa nasemaga kuwa Tanzania hakuna viongozi wanaoweza kujieleza, % kubwa ya wabunge wa Tanzania ukiwasikiliza unapata jibu kuwa hawa ni zaidi ya wapuuzi kwa majibu na maswali wanayoyauliza, hasa wabunge wa kile chama cha kuiiba kodi na rasilimali zetu ndio wanongoza. Huwa nakiita chama cha wapuuzi chenye wafuasi vipofu na viziwi wakipewa wali na nyama basi wanaona ndio wamesaidiwa kutatua matatizo walionayo. hata Mwenyekiti wao pia ni wahovyo ndio maana huwa natoa hotuba za mipasho
 
umetoa mada ya hamasa ila hujatolea mfano wapi ili tujua unachoongelea ni baadhi ya watanzaia walio wachache au walio wengi, ninachotaka kukuambia ni kuwa maarifa ya mtu yanapofikia kiwango hutumia maneno kama sisi watanzania ni watu wa ajabu sana au unasema mm ningeomba ujue kila mafanikio ni uongozi bora, ukiona familia ya fulani ina maendeleo ni msimamo na uongozi bora wa familia hiyo ukiona nyingine haina lolote ni mfumo dhaifu wa familia hiyo, sisi kuendela ni uongozi uliopo madarakani sio watanzania, tunawasomi wengi wanokubalika kimataifa mfano Profesa Muhongo, amechukuliwa nje ya nchi, Dr, Balali alichukuliwa nje ya nchi ila watanzania, majungu ni upeo mdogo wa kufikiria na sisi tunataka tuweke kelele kwenye sayansi ili gesi ibadilike iwe tindikali, hebu jaribu unapoandika title yako mpe msomi aihariri ili ipendeze kwa kila rika.
 
aina ya elimu tunayoipata watanzania wengi ni elimu maliza ujitegemee, hivyo inapeleke wengi kutoitafiti elimu wanayo ipata hivyo kupelekea uelewa kuwa mdogo katika kuchanganua mambo mengi wanayokutana nayo
 
Nawalaumu sana wazazi wangu.Kitu kidogo unafokewa.Kitu kidogo kichapo.Kitu kidogo huwezi.
 
Back
Top Bottom