mutant gene
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 876
- 326
Watanzania tuna tatizo sana la kujielezea au kutoa ufafanuzi wa jambo fulani au nini kifanyike juu ya jambo fulani. Ukitaka kukubaliana na mimi angalia vipindi vya kwenye television au radio ambavyo vinahoji Watanzania au hata humu JF unaweza ukathibitisha.
Unaweza kupigwa butwaa mtu anavyojibu au anavyoelezea jambo mpaka unajiuliza hivi huyu anaelewa anachoongea/kuulizwa au anaongea na ye aonekane ameongea! hili tatizo si kwa wale wasioenda shule pekee bali hata waliofanikiwa kupata elimu.
Najiuliza sana hii hali inasababishwa na nini? kutojiamini, kukosa ufahamu, uvivu wa kufikiri, kujifanya tunajua sana wakati hatujui au ukosefu wa lishe bora toka utotoni umedumaza akili za watanzania wengi?! na kama tumerogwa basi alieturoga, ameturoga pabaya. tuna safari ndefu sana! Kwa ufupi hili taifa kuja kufanikiwa ni ndoto ya saa sita mchana.