Serikali ya mkoa wa Mwanza inabidi iangalie namna ya kudhibiti kundi kubwa la watoto wa mitaani ( chokoraa) na omba omba wenye watoto wadogo
Kiukweli ukipita maeneo mengi ya katikati ya jiji utakutana na watoto wengi wa mitaani ambao usiku wanageuka wahalifu hatari mi nishakabwa usiku mmoja na kuporwa pia mji umejaa kina mama na kindada ambao wanaendesha shughuli ya kuomba wakiambatana na watoto wao wadogo kiukweli inatia huruma kwa hawa malaika wanaozunguka kutwa na mama zao wanaoomba omba
Nawasilisha
Ndugu Wazabanga kuku hoja yako kwangu inamashiko tena mkubwa
Nakuja na Nchi mbili kama mfano waliopata ktk kupuuzia lundiko la watoto walio telekezwa mtaani ( Uganda 2000's-2012 na Liberia )
Uganda ilikuwaje 2000-2016
Kulizuka na kundi linalopingana serikali , likijiita LORD RESISTANCE ARMY ( LRA ) likiwa chini ya Mhasi Mkuu Joseph Kony
Je Kony alianzaje kuliunda hilo kundi , yeye aliwateka wanafamilia mbali mbali pia aliona fulsa mkubwa sana uwepo wa watoto wa mitaani walio kuwa Uganda kaskazini magharibi ,
Kony aliwachukuwa na kuwatunza kisha akaanza kuwalisha sumu ( pumba au ujinga ) kuwa selikali ndo adui wao kwa iyo wapambane dhidi yao , kweli Kony alifanikiwa na akawa kikwazo Uganda
HUYU JOSEPH KONY ALIMPIGA RISASI KAMANDA WAKE VINCENT OTTI , BAADA YA OTTI KULIDHIA HATI YA MAKUBALIANO YA AMANI NA SERIKALI ,
NDPO 2006 KUANZISHWA KWA MAZUNGUMZO YA " JUBA PEACE TALK " LAKINI HAWAKUFANIKIWA
Tukaangalie muvi inayoitwa JOHN MAD DOG ( JONI KICHAA )
KWA UPANDE WA LIBERIA
Ndugu Charles Taylor baada ya kusndwa uchaguzi yeye aliamua kukusanya watoto wa mitaani na watoto mateka na kuwafunza ukatili naye akafanikiwa
( siyo muvi ya chazi ila ni mfano wa Liberia ile muvi ya BLOOD DIAMOND )
Binafsi nimeishi Mwanza , nimepata kutembea sana pale mwanza hoteli na maktaba ya wahindi hawa madogo wapo wengi wana viwembe mda wa usiku , usiku wakikuomba pesa wape ondoka zako
Sasa watoto kama hawa hii sumu waliojipandkiza ni mbaya na hatarishi kwa usalama wa jiji la Mwanza