Tatizo la Watoto wa Mitaani : Nini Kifanyike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la Watoto wa Mitaani : Nini Kifanyike

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VoiceOfReason, Aug 12, 2011.

 1. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Wakuu kila mara nikipita mitaani na kuona watoto wamejaa mitaani naona "Time Bomb" tunatengeneza majambazi wa kesho na watu ambao hawana skills wala mbele wala nyuma.

  Ni mengi yamefanywa kama ifuatavyo:-

  • Kutengeneza NGOs za kuwalea watoto (ingawa hizi nyingi zimekuwa kama njia ya wachache kujipatia kipato)
  • Jamii kusaidia kulea watoto yatima (kuna jamaa yangu mmoja alijitolea kumchukua mtoto wa mitaani na kumsomesha lakini huyu mtoto alitoroka akamuibia na kurudi mtaani
  Hivyo basi kama hayo yote hapo juu hayafanyi kazi ni nini kifanyike?
  Sababu hawa watoto bado ni wadogo inabidi maamuzi magumu yafanyike, inabidi kama jamii tutengeneze homes zenye ulinzi mkali wa kuwaweka watoto huko (kuhakikisha kwamba hawatoroki) na huko wapewe elimu, wafundishwe attitudes nzuri, na skills tofauti (we are loosing a lot of talent) na wakae huko mpaka pale wakiwa wakubwa (graduate ndio waachiwe waingie mitaani) na kama serikali iwape first priority katika kazi tofauti. Na pesa na misaada yote iwe inapelekwa huko, na kuwa na ardhi ya kutosha kuwafundisha kilimo na ufugaji pia.

  Ninachomaanisha yaani hiki kiwe ni kama chuo cha kufundisha hawa ndugu zetu maadili mema ili tusaidiane nao kujenga taifa na sio kubomoa

  Any more Suggestions Please, sababu what we are doing now don't seem to work., na tusiporekebisha leo kesho itakuwa too late...
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  kwanza kabisa wajitokeze wanasheria au serikali iwe na wanasheria maalum wa
  kutetea watoto wanaodhulumiwa mali kama nyumba na ndugu wa wazazi..
  pindi wazazi wakishakufa
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Rule of "Law" and "Good" governance inaweza kupunguza idadi ya watoto wanaoishi mitaani!

  Kwa Tanzania - Sifahamu vizuri ni ipi kazi ya Wizara ya Ustawi wa Jamii? Kama hii Wizara "ingeshikia bango" - kisheria - wale wote wanaozaa na wanawake na kutelekeza watoto - wangepungua sana...

  Vyanzo viikubwa vinavyozalisha watoto wanaoishi wenyewe mitaani ni:-

  1. Mimba za "utotoni"
  2. Ndoa kuvunjika
  3. Wazazi kufariki - either mmoja or wote wawili"

  Yote hayo matatu hapo juu yanaweza kutatuliwa kama "watawala" watatoka usingizini na kusimamia sheria za malezi na makuzi ya watoto...
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii huenda ikapunguza wengine kuongezeka lakini vipi wale ambao bado tupo nao sasa hivi mitaani, pili sio kweli kwamba watoto wote wa mitaani ni yatima wengine tu wanapenda kukaa bila sheria..., kuna jamaa yangu ninamfahamu watoto wake walipotea kama wiki akaja kuwakuta wapo mitaani kisa tu ni kwamba alimfokea mtoto wake...

  Ndio maana nikasema kama tukiwa na homes za kutosha (ingawa wengine wataziita prisons) huku kutakuwa hakuna kubembelezana bali ni kufundishana maadili na skills tofauti na mtoto akishakuwa mkubwa tutakuwa tumempa zawadi ya ufunguo wa maisha
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu lakini watoto wakiwa wadogo wanaitaji zaidi mtu wa kuwafundisha what is right or wrong sababu bila hekima soon hao watoto wakifikisha miaka ya kujitegemea hata hizo mali watazipiga bei
   
Loading...